Sio T.R.A tu, mamlaka za kodi dunia nzima zinaogopeka na hazina "urafiki" na walipa Kodi, moja kati ya hizo ni "TRA" ya Marekani, inaogopwa mno!

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Mamlaka za kodi ni "polisi wa mapato" inachukua halali ya serikali, na kawaida, ni jbo gumu kwenda kuchukua kwa mtu fedha yake, lazima alalamike.

Watanzania hatujiulizi kwa nini makusanyo Sasa ni trilioni mbili? Wakati mwanzo ilikuwa trilioni moja na bilioni 200? Nani hawa walikuwa wanakwepa Kodi ya bilioni 800 Kila mwezi? Ni nani hawa? Ndio hawa wanaolia?

Wanachofanya TRA kukusanywa mapato, hata halmashauri, kinafanyika Dunia nzima, na mamlaka za kodi duniani kote, hazijawahi "kupendwa". Ukiona zinapendwa, ujue Kuna ufisadi. Ukiona zinachukiwa, Kuna watu wamekaziwa "nati".

Wana uhalali wa kuangalia risiti zote kujiridhisha, haiwezekani uuze mzigo wa milioni 500, uandike risiti ya milioni tano, halafu TRA unataka pale nje ya duka wasikague mzigo, au imefika kibaha, dodoma, usikaguliwe.

Watanzania ....siku tukikubali "urafiki" wa TRA na wafanyabiashara, tumekwisha. Hatukatai masikilizano, na reasonableness. Lakini mipaka iwepo.

Makadirio ya Kodi yenye ubishani yaundiwe sub committees, asiachiwe Afisa mmoja, na TRA waende digital, anything communicated kwa mlipa Kodi isomeke mpaka makao makuu ili asipate fursa ya kucheza mchezo, anything iwe communicated digitally.

Tunataka fair play, kama umeuza halali, kwa nini hutaki waone ulivyouza?

All in all, nchi zinahitaji Kodi, na wa kulipa ni sisi.

 
Na wao wagome

 
TRA ya marekani,ungesema tu mamlaka ya mapato ya marekani ila sio TRA
 
TRA ya Marekani inafanyia kazi kodi za Wamarekani huku kwetu zinapigwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…