Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

MUSHEKY asante kwa mchango lakini sidhani kama umenisoma na kunielewa nilichoandika.. Hiki unnachoita mahaba sijui ulimaanisha nini hapa... Jaribu kusoma mtiririko wote tena wa kile nilichoandika pengine unaweza kupata maana halisi

Jr[emoji769]
 
Chadema haiwezi kufa kwa hoja za watu wanaolipwa kwa kuichafua , tumeonya mara nyingi sana kuhusu hilo , huwezi kuichafua chadema huku ukiwa na malipo kwenye bahasha ya Khaki .

Chama makini hakitoweza kufa ikiwa viongozi wakuu wana mshikamano ( Katibu na Mwenyekiti ) , Baada ya Mashinji kupigwa chini njama zote zilizopangwa dhidi ya Chadema kabla ya uchaguzi zikazimika mithili ya mshumaa jangwani , iko siku nitaandika kuhusu hili , wengi hawaelewi msingi wa kibwagizo cha #MWAMBA TUVUSHE .
 
sisi wengine tunaposimama kati na kuwaambia upinzani ni moja mbili na tatu,mnatuona wajinga mnatupa majina ya ajabu ajabu,mara buku 7,praise team,mara mataga its ok.

upinzani sio chama,ni itikadi ambayo ni lazima ijikite katika kutafuta matokeo mazuri,sio umaarufu.
haiwezekani mtu akawa hakubaliani na kila jambo.hatua hii ndio imefanya kuibuka na makundi haya mnayoyaona leo.

wenye itikadi za kweli wapo kati,wenye malendo yao mengine wapo kulia na kushoto.

mengine wacha nature ichukue mkondo wake.
 
MUSHEKY asante kwa mchango lakini sidhani kama umenisoma na kunielewa nilichoandika.. Hiki unnachoita mahaba sijui ulimaanisha nini hapa... Jaribu kusoma mtiririko wote tena wa kile nilichoandika pengine unaweza kupata maana halisi

Jr[emoji769]
Mkuu hapo kwenye "mahaba" nimemaanisha kua na mapenzi mazito na itikadi fulani kiasi cha kuiacha akili hatua moja nyuma

Kuna wakati flani kuna watu flani wanavaaga miwani ya njano

Mara nyingi hupita mtaani na kukenua kwa kua kila wanachokiona duniani ni cha njano

Watu hawa nawashauri wanapotaka kufahamu rangi halisi za ulimwengu na vilivyomo wavue kwanza miwani yao ya njano, laa sivyo wataendelea kuona kila kitu ni cha njano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi nataka CHADEMA kife,Ila ukiniuliza Kwanini Kwasina majibu nabaki natumbua macho tu,naomba Msaada wenu wenzangu na mimi tunaotaka CDM kife,nikiulizwa kwanini nataka kife nijibu nini? Maana ile hoja kwamba CDM inatumika na mabeberu inaonekana ni propaganda tu za chama changu CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upinzani kwenye taifa hai ni mhimu sana. Bila upinzani hakuna demokrasia wala maendeleo. Sharti la jamii hai ni "existence of opposites".
 


Mkuu NONDO and CO's ni wa lini ?
 
Hakuna cha kulialia hapa, kitakufa kama chama vingine vya upinzani. Baba wa Taifa aliishatwambia upinzani wa kweli utatoka CCM na sio kwenye vyama vya kuganga njaa!
 
Hakuna cha kulialia hapa, kitakufa kama chama vingine vya upinzani. Baba wa Taifa aliishatwambia upinzani wa kweli utatoka CCM na sio kwenye vyama vya kuganga njaa!
What a wasted manure

Jr[emoji769]
 

Lakini sasa kwa mtazamo wako yule aliyeishia la saba na anataka uwanachama au uongozi, anayajua hayo ya mrengo upi CHADEMA inasimamia? Sio kila mwanachama ana degree in political science.

Ukiachana na CCM survival, CHADEMA ina banwa na mivutano ya ndani kuliko ya nje. Mivutano ya matumizi ya fedha, mivutano ya uwongozi, hata mivutano ya fursa za kuwania nafasi za kiutawala kwenye jamii ubunge udiwani nk. Ukisema CCM ndio inaikwanisha CDM unakuwa umechukuwa njia fupi ya kutafuta mchawi wa mbali wakati kumbe mchawi yuko ndani ya nyumba yako.
 
Sasa ndugu yangu, unaweza kusema hata kupata utawala bora ndani ya chama inashindikana kutokana kubanwa kisiasa? Hata kuwa na mahesabu na vitega uchumi vinavyotambulika huko nako ni kutokana na kubanwa. Usuniekewe vibaya, hata mimi ningependa kuona CDM inastawi, lakini ijikite kwenye siasa safi, uwongozi bora na utumishi wa umma. Kuliko ilivyo sasa kwamba inatoa nguvu nyingi kwenye utumishi wa chama.
 
Ok ok sawa nimekuelewa vizuri

Jr[emoji769]
 
Ni kweli lazima tukubali kuwa CHADEMA ndicho chama mbadala wa CCM, hivyo uwepo wake na uimara wake ndio chachu ya uimara wa CCM, hivyo wale wanaoitabiria mabaya wajuwe kuwa hawalitakii mema Taifa letu!..Hawa ni kundi moja na wale wadanganyifu wenye vipaji wanaopenda kuse CCM ndio chama pekee cha kutuletea maendeleo, lakini wanasahau kama CCM ndio chama kilichokuwa madarakani tangu tupate uhuru, Lakini Dar es salaam tu tu ambayo ndio imekuwa kama makao makuu ya chama na serikali tangu tupate tuape uhuru mpaka leo, lakini kila mwaka mvua ikinyesha tu ni maafa! Si huko tu Kule Zanzbar nako uchaguzi wa mwaka 2015 uliunda Bunge na serikali ya CCM tu je matatizo yamekwisha?..Wanaoiona CHADEMA ni dhaifu wajaribu kwanza kupima nguvu ya fedha na nguvu ya dola inayotumika kupambana na chama hiki chama, Karibu mihimili yote ya dola imetumika kama silaha kuangamiza chama hiki lakini kipo! Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makamanda wa polisi nchi nzima ni sehemu ya jeshi na timu inayotumika kuangamiza chama hiki lakini bado kipo! Kama hapo una namba ya RPC piga simu mwambie CHADEMA wanajiandaa kufanya mkutano wa hadhara hapa mtaani kwetu, Haraka mno polis watafika hapo na magari huku wakiwa na mabomu na silaha nzito! haya mambo sio ya kuombea yaje kuitokea CCM iliyozowea siasa nyepesi, mtakujalia na kusaga meno! Wamepandikizwa mapandikizi ndani ya CHADEMA wasaidie kukitafuna chama kwa kuanzisha migogoro isiyo na kichwa wala mkia, lakini wakawama!....Kilichopangwa na Mungu mwanadamu hawezi kupangua!..Ni muda tu utaamua, nina uhakika kama mazingira ya haki yakiwekwa sawa , huko tuendako tutashudia CCM ikipiga story kwenye kijiwe cha vyama vya upinzani!
 
Kila mpenda maendeleo ya ukweli angependa kuona vyuo vyetu vinazalisha vijana wenye mawazo mbadala yaliyo huru ya kijasiri, uzalendo na yenye kuchanganua mambo kwa uwazi na ukweli. Lakini kwa hali ilivyo sasa ni vigumu kupata vijana wa vyuoni wa aina hiyo kwa sababu walimu wanawoga kwa kutoa elimu ya aina hiyo kwani kuna "NYOKA' wengi wamejaa vyuoni. Hii kwa mujibu wa Mwalimu moja wa UDSM
 
Kwahiyo CHADEMA kimezuiwa kufanya shughuli za kisiasa za majukwaani na mivutano ya ndani ya chama ?

Zile kesi za kubambikiwa zinazowakabili viongozi wa CHADEMA nazo zinatokana na movutano ya ndani ?

By the way mivutano ya ndani ya CHADEMA si ingekuwa nafuu ya ccm mbona bado kinatumia mpaka vyombo vya dola kuikandamiza CHADEMA?

Hivi unadhani kama kusingekuwa na mbeleko ya vyombo vya dola ccm kingekuwa bado hakijatolewa madarakani ?

Itikadi zetu zisituzibe macho tukashindwa kuiona hali halisi ya kisiasa nchini tutakuwa tumepotoka mno kama taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Upinzani ni haki ya kisheria ya chama chochote cha upinzani, wanalipwa ili watoe njia mbadala ya suluhisho ya matatizo nchi yetu. Ikifikia mahala wanapinga hata maswala muhimu kwenye ustawi wa nchi kama elimu, afya nk. Hapo unajiuliza kama ni kweli hawa wanania njema au ndio tamaa ya uwongozi. Ikifikia mahala chama kinaweka mikakati ya kushawishi wabia wetu wa maendeleo wasitishe misaada au mikopo ambayo ingesaidia hata wana Chadema. Kwangu mimi huo sio upinzani.

Unakosea kusema fedha ya walipa kodi sio fedha ya serikali, serikali imewekwa na wananchi kusimamia mambo yote yanayoihusu nchi, kodi ikiwa ni mojawapo ya mambo iliyokabidhiwa kuiangalia. Kumbuka hakuna anayeilaumu Chadema jinsi inavyotumia pesa zake, hilo ni swala la wana CDM wenyewe kulisema. Lakini kama kweli unataka kwenda na uhalisia wa nchi ilivyo, huwezi kutumia pesa ukidhani kama walipa kodi hawaoni. Walipa kodi sio CDM peke yao, hata vyama vingine navyo vinachangia kodi na wanahaki ya kujiuliza kama kweli mchango wetu kwa chama fulani inatumika ipasavyo?

Wala sina haja ya kuingilia kununua viongozi maana ni hoja isiyo kuwa na ushahidi wa aina yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…