Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

Pamoja sana. Hoja yangu humu jf tuna wajadili watu, wajadili matukio na wajadili hoja. Wewe Mkuu Mshana, you belong kwenye wajadili hoja.

Kwenye bandiko lile nimeweka hoja, ila wengi wanamjadili mleta mada badala ya hoja.
Pamoja sana.
P
 
Chadema siyo chama cha siasa ila ni saccos ya Mtei na Mbowe usidanganye na watz wakiwemo wabunge wenu wameshang'amua! Subirini kifo cha mende October!
 
Pamoja sana. Hoja yangu humu jf tuna wajadili watu, wajadili matukio na wajadili hoja. Wewe Mkuu Mshana, you belong kwenye wajadili hoja.

Kwenye bandiko lile nimeweka hoja, ila wengi wanamjadili mleta mada badala ya hoja.
Pamoja sana.
P
Noted kaka....!!!! You have my respect...!!!

Jr[emoji769]
 
Mi naunga hoja ya Mshana Jr. Kushabikia kufa kwa vyama vya upinzani Ni uzuzu usiopimika katika mambo ya siasa za mfumo wa vyama vya siasa.

Changamoto za kuwa na mfumo wa chama kimoja Ni nyingi kuliko kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Tunaipongeza serikali iliyoundwa na chama Cha mapinduzi kwa Kazi nyingi nzuri inayofanya ya kimaendeleo lakini Ni kwa sababu ya msukumo wa hoja na Nguvu za kiupinzani. Tusipokuwa na chama cha upinzani chenye nguvu ya kuihoji serikali pale yanapoonekana madudu Basi Taifa Hili litaenda kurudi nyuma km ilivyokuwa miaka ya 1980's

Na Sasa hata waandishi wetu wa habari wasisimame kushabikia hata mambo ambayo hayana misingi kwa kuwapotosha wananchi waamini vitu ambavyo havina mantiki.
Uandishi wa habari ambao unadhalilika Ni wa hapa Tanzania kuliko hata nchi zingine, kwasababu wamejaa unafiki,kushabikia kwa kujaji Maslahi yao kwa mambo Yale ambayo hayana tija.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
salama yao ni mwenyekiti abadilike ama apishe kunusura chama.
sera ya chadema ya kupambana na ufisadi ilikufaje au ufisadi umekwisha ?
chama hakina sera kimebaki chama cha kudandia matukio kama ngazi ya kujitangaza kisiasa.ccm inapiga ngoma wao wanacheza hakiwezi fanikiwa kamwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama kinakufa kutokana mfumi wana na uendeshaji wake pia aina ya wanachama wanaokiendesha! Sasa CDM inaendeshwa kama saccos ya kikundi cha watu fulani. Hivyo kufa lazima by the way kuna vyama vingine vitaibuka kwani lazima CDM iwepo? Tulikuwa na NCCR ikavurunda ikadorora!
 
Mkuu DenooJ, kwanza nikupongeze una kupaji cha uandishi na una uwezo wa kuandika maana umeshuka na para 7 aa nguvu.

Nakushauri tuu, ili kukilinda kipaji chako na kiandika kitu cha maana kwa kirefu,
  1. Jifunze kusoma, penda kusoma mada, ukikuta link fungua link ili ujue kitu kinachozungumzwa, ndipo uchangie kwa kirefu.
  2. Unaruhusiwa kumjua mtu, information is power hivyo ni kweli unamjua sana Pasco na umewasaidia wengine kujua.
  3. Jee unaijua Katiba ya Chadema na taratibu za kumfukuza mwanachama kwa makosa ya nidhamu?. Jee utaratibu huo zilifuatwa?.
  4. Kwenye bandiko nilizungunzia video, kumbe ni video ya kutekwa kwa Lwakatare!, Duh...!. Kumbe Lwakatare aliwahi kutekwa?!.
  5. Kumbe ni Mwigulu Nchemba alijitokeza hadharani akasema anayo video ya Lwakatare kutekwa, na Mwigulu alisema hivyo makusudi kwasababu za kisiasa, but mpaka leo hii, Mwigulu Nchemba hakuwahi kuonesha umma wa watanzania hiyo video?!.
  6. Umejuaje mimi naujua ukweli? ukweli gani?, wa kutekwa kwa Lwakatare au video ya kutekwa kwa Lwakatare?.
  7. Nitauzingatia ushauri wako.
La mwisho, kama ukisoma kitu na hukuelewe, usijibu kwa kirefu ili kuonyeshea kuwa wewe ni mwelewa, unajua watu kama unamjua Pasco, na unajua vitu, kama unavyojua kuhusu kutekwa kwa Lwakatare, sasa wanaojua video ni ya nini na nani ndio alikuwa atekwe, watakuona mjinga!.
P
 
Haupo huru; nakuona bado mtu aliepo kifungoni, huwezi kujadili mambo kwa uwazi unaotakiwa, naamini unajua kifungo kilitokea wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakin wakienda ccm wanapewa vyeo haraka sana mambo mengine hayaitaji akili kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…