Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

Unajiuliza nyerere angetumia hii kauli ungekuta sahivi familia yake yote ni mbailionea, ni kauli ya kibinafsi
 
Na ukizingatia hii corona imefanya mapato ya nchi kupungua hio ndo project ya jiwe, wagombewa wa chadema wengine watatekwa kabla ya kurudisha fomu, wengine watanyanganywa fomu kinguvu, na wengine fomu zao hazitapokelewa
 
Siyo kweli kama Chadema hawakubali madhaifu yao na wanasababisha vurugu je vyama vingine mbona viliuawa kwani navyo vilikuwa na vurugu?

Je wabunge waliopendekeza kwamba Zzk auawe walikuwa wanachochea Amani au vurugu? Na walikuwa wabunge wa Chadema?

Kiongozi aliyevamia Clouds Fm alikuwa wa Chadema? Leo haitwi mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika mkoa husika?

Aliyempiga risasi Akwilina ni kiongozi wa Chadema? Au waliompiga risasi Mh Tundu Lissu ni chadema?

Kama kudai haki ni vurugu basi tukubaliane kuwa mnyonge hana haki, ni hayo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabombe wewe ni mbunge utupe ushahidi wa mambo hayo uliyoyaandika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

unajichanganya boss: hakuna mtu ambae hatamani kuona maendeleo kila mtu anataman nchi iende na mambo yake yaende, katika vyama hapa Tanzania vyote vina mapungufu ndo maaana kuna sehem nmesema ni vyema chadema wakafanya kila wanavoweza kujisogeza ili ccm tukiwachoka kunakua hakuna kuwaza mara mbili

tuseme leo ccm wameharibu mbaya kama awamu ya nne, lazima tutafute suluhisho sehem ingine na ukiangalia uchaguzi wa 2015 watu walikua wameichoka ccm, lakini angalia maamuzi waliyofanya sasa chadema, kule kule tunapopakimbia ndo wao wao wanarudi, sasa wewe unadhan kuna upinzani hapo ambao tunaweza kuwaamini? huu ni mfano mmoja tu

kuhusu sjui kupigwa risasi, sjui tundu lissu izo ni siasa sio sera za vyama! hapa tunaongelea nguvu ya chadema, kwa sasa mtu kama mm ambae nataman kue na upinzani dhabiti nabaki kusema tu bora ccm waendelee kuliko chadema, imefika mpaka hatua nataman kuona NCCR wanakua wapinzani wakuu, sio kwa sababu nna chuki na chadema bali kidogo ndo chama ambacho naona hata kikichukua madaraka wanawza kuja na hoja zenye msingi, leo hii chadema hakuna cha maana mnaongea kila sku mnakuja na jipya la kuvuruga badala ya kujenga!
 

Mshana akili kubwa sanaa
 
Ni kweli lakini Kumbuka kipindi kile kulikuwa na operation mbalimbali zilizoanzishwa na mikutano mingi ya kisiasa ilipelekea watu kupata msisimko wa kujiunga katika siasa wakiwemo vijana wasomi.

Vijana wa CHASO wanazuiwa hata kufanya mahafali yao, hapa siyo kwamba siasa zimepoa bali kumekuwa na uminywaji wa demokrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna huyu anafurukuta kutoka kaburi la kisiasa!
 
Mtu akisoma hii coment yako aweza akuone unaakili nyingi sana na anaweza pumbazika.
Lakini ulichoongea ni kama unaanza jifunza siasa za tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana yakitokea haya jua ni KAMA!

Ikumbukwe kuwa Walioihujumu NCCR ni hao hao Chadema tangu enzi za vikao vyao vya Siri Miaka ile ya 1994

Watafute Dr. Tenga, Prof. Baregu, Nsanzugwako kina Komu na wengine wengi wanayajua haya.
 
Kwahiyo kutofuata taratibu za kuwafuta uanachama ndani ya chadema , Je kunaweza kuwa Kinga ya wao kuendelea kuwa wabunge? Swali kwako Mr Pascal

Je walifutwa wamefanyaje mpaka Sasa kwa mujjibu wa Katiba yao . Wamekata Rufaa au wapo kulalamika kwenye vyombo vya habari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutofuatwa taratibu sio kinga, ya wao kuendelea kuwa wabunge. Wanaendelea na ubunge wao kwa powers za Spika.

Kwavile muda wa kukata rufaa ni 14 days, muda upo tusubiri.
P
 
Kausome ujamaa utaelewa hapo bado unapwaya, alikuwepo Nyerere na Paul Sozigwa since then hamna mjamaa CCM ndio maana awali nimekuambia unitajie mjamaa mmoja CCM kwasasa na sio ngonjera unazoleta.

Kuhusu urusi na China walishavuka kwenye Siasa za kijamaa tangu Gorbachev alivyoisambaratisha USSR, ukomunist ni kwa ajiri ya kutawara na si katika uchumi na vinginevyo likewise hapa ujamaa unatajwa ili watengeneze marobbot ya kuyakremisha upuuzi, maana katika ujamaa kiongozi ni "mungu" ndio maana ujamaa unakana uwepo wa Mungu.

Kuwa Hata muasisi alikuwa mjamaa kweli bado haijadhihilika maana turnaround ya JK Nyerere 1966 haieleweki kuwa kwanini ujamaa ulianza kujadirika mala baada ya mapinduzi ya 1964?

Jk Nyerere alikuwa bepari in the beginning mind you!

CCM bado ni cha laghai! Au LA mtaje mjamaa mmoja huko
 
Moja ya tatizo kubwa linaloiuwa CHADEMA ni wao kudhani adui yao mkubwa ni CCM pekee. Yes, CCM ni adui wa CHADEMA na wanataka leo hata kesho chama hiko kife. Lakini hata hivyo, CHADEMA pia ni adui wa CCM na wao wangependa kuiona CCM ikifa leo hata kesho. Na hii ndo tunaita SIASA, kila chama lengo lake ni kushika dola kwa gharama yoyote Ile. Kwahiyo, CCM kuitakia CHADEMA mabaya siyo DHAMBI bali ni SIASA. CHADEMA kikifa leo, kitakuja chama kingine kwani upinzani ni fikra na mitazamo ya watu siyo chama. Ndo maana tulikua na vyama vyenye nguvu kama NCCR, CUF na leo tuna CHADEMA. Kwahiyo, CCM hata ifanyaje haiwezi kuua Upinzani.

Lakini hebu tuangalie kwa undani zaidi bila kuleta ushabiki wowote wa kivyama. Hivi haya yanayotekea CHADEMA leo CCM haikuwahi kuyapitia? CCM haikuwahi kukimbiwa na wabunge wake? CCM haikuwahi kukimbiwa na Madiwani wake? CCM haikuwahi kushindwa kwenye chaguzi ndogo za ubunge? CCM haikuwahi kukimbiwa na Wanachama wake waandamizi wenye ushawishi kwa Jamii? Jibu ni NDIO. Tena vizuri umetolea mfano mpaka wa kina Mrema hapa sijataka kuyataja yaliyotokea 2015 kila mtu anajua kilichotokea CCM. Lakini bado chama hicho kiliendelea kuwepo na kushika dola.

Jambo kubwa ambalo CCM inavishinda vyama vingine vya Upinzani inapopitia kwenye migogoro ni uwezo wake wa kuweza kujibadilisha kulingana na wakati. CCM ya nyerere siyo sawa na CCM ya Mwinyi wala Mkapa. CCM ya Kikwete ni mbingu na ardhi na CCM hii ya Magufuli tunayoiona sasa. Lakini kwa vyama vya Upinzani ni tofauti kabisa, Viongozi tulio nao ni wale wale, mbinu wanazotumia kupambana na CCM ni zile zile. Huwezi kupambana na CCM ya Magufuli kwa kutumia mbinu ulizokua unatumia kwa Kikwete lazima utafeli. Ili Vyama vya Upinzani viweze kuwa imara muda wote ni lazima na vyenyewe viwe na uwezo wa kujibadilisha kimfumo na kiungozi kama ilivyo CCM ili kuweza kupambana nayo.

Kinachoendelea kwa sasa CHADEMA, kwa kiasi kikubwa kinasababishwa na migogoro ya ndani ya chama hicho tena ya muda mrefu. Hivyo, CCM inachofanya ni kutumia mwanya huo kuhakikisha chama hicho kinasambaratika jambo ambalo siyo DHAMBI bali ni SIASA. Migogoro ya ndani ya CHADEMA ilipaswa kutatuliwa kwa busara na hekima za kiuongozi badala ya kutumia mihemko na ubinafsi. Na hiki ndicho kinachoiua CHADEMA kwasasa.

Sasa kama tunakubali chama kina mapungufu katika uongozi wake, lakini badala ya kuona ni namna gani ya kuondoa mapungufu hayo, Sisi tunasema eti mapungufu hayo waliyonayo viongozi wetu ni ya kibinadamu hivyo yapaswa tuwavumilie kwasabbu wamekifanyia mambo mengi mazuri chama chetu. Tunasahau kwamba, mapungufu haya waliyonayo viongozi wetu ndiyo yanayotumiwa na CCM kuvibomoa vyama vya upinzani. Hata Nyerere aliifanyia mengi mazuri nchi yetu, lakini ilipofika wakati changamoto za nchi zilivyozidi ilibidi ang'atuke kupisha fikra nyingine ili nchi iweze kuendelea.

Tutaendelea kuilaumu CCM inayofanya SIASA zake ili kuendelea kushika dola, tukidhani ni DHAMBI kubwa kutaka CHADEMA ife kumbe CHADEMA inajimaliza yenyewe.

Alamsiki.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Kitu pekee ccm inavishinda vyama vingine ni kwamba vyombo vya dola ni ccm na tume ya uchaguzi ni ccm.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa ccm Bashiru Ally alisema ccm itavitumia vyombo vya dola kushinda uchaguzi, je huu ndiyo uwezo wa kujibadilisha wa ccm ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…