Sioni dalili njema kwa wapinzani hapa Dar es Salaam

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
651
Reaction score
2,246
Dar es Salaam ndipo tulitarajia iwe ngome kuu ya upinzani Nchi hii KUSTAWI ajabu inaelekea kuwa sivyo.

Mwenendo mzima wa aina ya upepo wa kampeni za uchaguzi mkuu huu kwa hakika haupo kabisa mwamko na hamasa za ki harakati zilizo chanya kwa upinzani.Kumepoa!

Dalili ni njema hasa kwa wagombea wa CCM kwa jiji hilo kuu hapa nchini.Sioni wagombea hasa wa majimbo ya Dar es Salaam wa upande wa upinzani wakifua dafu kwa wenzao wa CCM hali hii ni tofauti kabisa na uchaguzi uliopita.

Anyway, muda huwa Mwalimu mzuri acha na mimi nijipe muda pengine lolote hapo katikati linaweza kutokea.
 
I second you on this one, dalili zikisha onekana wakati wa ufunguzi wa kampeni.
 
Selikali NEC tunaomba muheshimu Maamuzi ya wananchi.

Huu ni wakati wetu wa kuchagua kiongozi tunayemtaka siyo kuchaguliwa na Magufuli Nec Polisi Ts, wakurugenzi nk.

Tuepuke udanganyifu.
Haki huinua Taifa
 
Huoni wewe umeongea na watu wote wa Dar au hata Dar yenyewe hujawahi kufika unaandika ukiwa kwenu Iramba kwenye nyumba za tembe? Shame on you Dar haina watu wajinga kama uliko
Wewe si uko Babati au? Usitusemee sisi wana Dar.
 
ukiwaambia ukweli wanakuparua.

halafu wanasema magu anapenda sifa.
 
Dar ni jiji ambalo liko bize sana. Sisi wapiga kura wa dar tuko na access kubwa kuhusu wapiga kura na maamuzi lazima yatafanyika kama kawaida
 
Kumbe ni wewe
 
Mie nilikuepo Mbagala siku ya ufunguzi, lakini changamoto hakukuwa na promotion ya mikutano ndio maana ilidorora kidogo tofauti na siku Lissu anatua airport ambako ilikua imetangazwa mapema watu wamehamasishwa kujitokeza.

Pia watu ni kama wamekata tamaa ukizingatia walichagua upinzani alafu wakahamia CCM, unless Lissu arudi na upepo mzito baada ya momentum ya mkoani otherwise wapiga kura watakua wachache mnoo.
Sio CHADEMA tu hata CCM kampeni zao zimedorora mnoo na watu ni kama hawana muda na kampeni kabisa. Ila upinzani upo sana tu wanachohitaji ni hamasa kma ile siku ya kumpokea Lissu

Ukiweka kwamba ACT na CHADEMA wataungana kwa Dar hivyo natarajia mkutano wa Mwembeyanga utaenda fufua nguvu ya upinzani hapa Dar na kuendelea mpaka oktoba. All in all maazimio ya Mwembeyanga yataamua upepo wa kampeni za upinzani Dar.
 
Jitu linaishi porini huko chalte unazungumzia Dar shenzi kbs
 
Hizo dalili za CCM kushinda ndio zipi? mimi niko Kawe sizioni, hebu nitajie hizo dalili.
 
Kumbe ndio maana msajili ameanza kupiga mayowe!.
 
Hiyo ya Mwembeyanga msajili ameshakubaliana na huo ushirikiano? Maana naona anajaribu kuweka zuio lisilo hata na msingi. Yaani vyama vikiweka ushirikiano yeye homa inapanda. Nadhani kuna mmoja anayegombea ambaye ana nasaba naye.
 
watu wa Dar wana akili wanajua kabisa sio ccm wala wapinzani watakaobadirisha maisha yao ndio maana wapo busy na mambo yao kwani wanasiasa wote wanapigania matumbo yao
 
watu wa Dar hawana purukushani kama wa mikoa mingine..ila siku ya kura safari hii Magu hapati hata 30k
 


Ni kweli kwani wagombea wa CCM wamezowea hii hali ya kutoa kitu kidogo kwanza
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…