Sioni hasara yoyote CCM ikifa sasa! Ifike hatua hata aliyeko CCM mwenye mapenzi mema na Nchi, awe radhi kwenye hili!

Sioni hasara yoyote CCM ikifa sasa! Ifike hatua hata aliyeko CCM mwenye mapenzi mema na Nchi, awe radhi kwenye hili!

Nsanzagee

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2023
Posts
2,209
Reaction score
4,769
Kizazi cha wazalendo CCM kimeisha sasa, ndani ya CCM, kimezaliana kizazi cha mafisadi tupu na hakioni haya kufanya hivyo, wajukuu na vitukuu ambavyo vimekuta wazee wao wanajilimbikizia mali kwa wizi na ufisadi, vimeishi kwenye maisha hayo mpaka vimekuwa na kufikia hatua ya kuwa viongozi

Chama ambacho kimekuwa ni pango la mafisadi miaka nenda rudi hakiwezi tena kuacha tabia hiyo kwa sababu watoto wa watoto wao wamerithi tabia hiyo kutoka kwa wazee na mababu zao

CCM imefikia kwenye stage ya kila aliyeko huko ni fisadi kwa sababu kakulia na kulelewa kwenye huo

Sishangai kuona siku moja tukitawaliwa viongozi kuanzia ngazi ya juu mpaka ngazi ya ubalozi wote wakiwa ni mafisadi na hakuna anayemkemea mwenzake kwa sababu ndivyo walivyo

Kiashiria kikuu ni zile ripoti za CAG kutokufanyiwa kabisa kazi yoyote ya kiuwajibishwaji kwa wahusika, tenda ya Sugar n.k

Nani ataitetea tena TANZANIA ikiwa ccm itaendelea kubaki madarakani?

Ikifa CCM kuna Mtanzania yeypte atakayeumia?
 
Back
Top Bottom