I hope I am wrong lakini naona kuna possibility kubwa sana ya Bunge hili la katiba kusambaratika kabla ya kumaliza kazi. Unaweza kuliona hili kwa kuipitia kwa makini misimamo ya makundi katika bunge hili na kujaribu kuangalia uwekano wa misimamo hiyo kubalika. Nikiitazama kwa undani misimamo hii na makundi yake, ninachoona huko mbele ni giza tu....
CCM wakiwa na idadi kubwa ya wajumbe kwenye Bunge la Katiba na vile vile wakiwa na kiburi kwamba wao ndio wenye serikali, wanaona wanawajibika kuwapa watanzania kile wanachoamini wao ndio bora kwa watanzania, na hicho kwa mujibu wao ni muundo wa serikali mbili kwenye katiba mpya. Kwa upande mwingine UKAWA ambao nao wana ushawishi mkubwa, nao wameshikilia msimamo wa serikali tatu na hapa ingawa wao hawana serikali kama CCM, kile wanachokisimamia vile vile ndicho kilichopendekezwa na tume ya mabadiliko ya katiba. Naona ugumu sana, kuwatoa hawa vile vile kutoka kwenye msimamo huo haswa ukizingatia kwamba wana sababu zote za msingi za kudai kwamba maoni ya tume ni maoni ya wananchi !
Kwa hiyo hata kabla ya Warioba na Kikwete kuwasilisha, bado kama ambavyo wengi tunajua, issue ya muungano wa serikali katika katiba mpya ni issue ambayo ni very delicate na isipokuwa handled with care nadhani inaweza kutuletea matatizo huko tuendako. Baada ya Warioba kuwasilisha rasimu watu wengi including baadhi ya wanaCCM ambao hawakuwa na misimamo mikali walionyesha kuelewa sababu za Warioba kufikia conclusion ya serikali tatu. Ingawa uwasilishaji wa Warioba uli-boost UKAWA na kuwakera baadhi ya wanaCCM, kwa kiasi kikubwa hali ilikuwa shwari...
Hotuba ya Kikwete kwa kweli, ime-complicate kabisa process yote....Mimi ni kati ya watu ambao naona Kikwete amekosea kuikosoa rasimu ndani ya Bunge la Katiba kama vile yeye ni mmoja wa wajumbe wa Bunge wakati sie na haswa ukizingatia kwamba yeye ni Rais wa wote (UKAWA, CCM na wananchi wote kwa ujumla). Hata wale wanaosema kwamba Kikwete hajafanya makosa, hawawezi kupinga ukweli kwamba hotuba ya Kikwete imechafua hali ya hewa kiasi cha kutishia kulisambaratisha Bunge la Katiba..
Hoja ninayotaka kuiwakilisha katika huu uzi, ni kwamba baada ya kuitafakari misimamo ya makundi niliyoyataja hapo juu na kuiweka na hotuba ya Kikwete kwenye equation hii sioni namna yeyote ambavyo hili Bunge litamalizika kwa hali ya kawaida. Most likely litasambaratika. I hope I am wrong lakini indication zote zinanifanya niamini hivyo kwa sababu zifuatazo :
1. Baada ya hotuba ya Kikwete, CCM kwa namna yeyote ile hawatakubali serikali tatu. CCM watafanya kila liwezekanalo kufanikisha serikali mbili na kama wakishindwa ninaamini watakuwa radhi mchakato uharibike. Kwangu mimi itakuwa ni muujiza kwa serikali tatu kupita katika Bunge hili. Ni rahisi sana kwa mchakato kuharibika kuliko serikali tatu kupita haswa baada ya hotuba ya Kikwete.
2. UKAWA hawatakubali serikali mbili, kwanza kwa sababu wana-support ya tume, ambayo hata kwa wale wasiotaka ku-admit, maoni ya tume ndio kwa ujumla wake tunaweza kuyachukulia kwamba ni maoni ya wananchi. Kwa hiyo tunaweza kusema wanasimamia msimamo wa wananchi na wao hawawezi kwenda kinyume na hilo. Na kitendo cha CCM kutumia maridhiano na kufanya Kikwete ahutubie baada ya Warioba na kumjibu Warioba, naona kita-reinforce misimamo ya UKAWA kwani kwa kiasi fulani kitendo hiki kimewadhalilisha hata wao na kuona kwamba wamekuwa cheated. Ndio maana Mbatia amewaomba msamaha waTZ kwa kuwa sehemu ya maridhiano hayo.....
3. Pamoja na ugumu uliopo, kwa maoni yangu, naona kuna uwezekano mdogo wa CCM kutumia wingi wao na resources zao (ukizingatia wao ni chama dola), wa kufanikisha kupita kwa muundo wa serikali mbili. Most likely Bunge linaweza kusambaratika katika hatua hii, lakini inawezekana kwa purukushani nyingi serikali mbili zikapita.
4. Zikipita serikali mbili, rasimu lazima iandikwe upya, kwani ile ya Warioba imeandikiwa kwa kuegemea serikali tatu. Hapa sioni uwezekano wa Bunge kuendelea kwani UKAWA hawatakubali. Sioni uwezekano wa watu kukubali Bunge la katiba liandike rasimu nyingine. Hii maana yake hakukuwa na sababu kabisa ya tume ya Warioba kuwepo.Kwa mawazo yangu possibility ya Bunge kusambaratika hapa ni kubwa mno. Ndio maana nasema sioni possibility ya hili Bunge kufikia mwisho likiwa moja na kutoa katiba inayopendekezwa kwa wananchi...
Ninawakubali sana wale waliosema tangu mwanzoni, tuwe na kura ya maoni juu ya muundo wa muungano kabla hata ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. At the end of the day naona hilo halitaepukika !. Kura ya maoni juu ya muundo wa serikali na possibly juu ya kuwepo kwa muungano wenyewe haipukiki. Tunaweza kuitisha hii kura kwa hekima na busara au kwa kulazimishwa na mazingira baada ya kuvurugana sisi wenyewe.
Tumaini langu ni kwamba tutaamua sisi wenyewe bila kulazimishwa na mazingira kwa sababu mazingira hayo
yanaweza yakawa ni pamoja na machafuko ya kisiasa.