Uchaguzi 2020 Sioni wa kutuletea katiba sio Magufuli wala Mbowe

Uchaguzi 2020 Sioni wa kutuletea katiba sio Magufuli wala Mbowe

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Watanzania tunatakiwa kujitoa kuitafuta katiba na tume huru kwa udi na uvumba wanasiasa wetu mnawajuwa wenyewe. tunatakiwa kuingia barabarani maelfu kwa mamia kudai katiba ya warioba na tume huru ya uchaguzi.

Ni aibu sana kizazi cha 1980 kuja leo kuwa na katiba mbovu kiasi kile hata watu mil moja tukiingia barabarani kudai katiba kweli tutaumia lakini lazima katiba itapatikana.

Vyama wanaangalia maslahi yao tu hakuna cha maana wanaweza fanya katiba ya Warioba ipo tayari lakini miaka 5 imepita watu wameilalia pamoja na mabilion iliyotumia. nashauri tudai katiba kwa faida ya kizazi chetu na kijacho au warudishe pesa zetu walizotumia.

Miaka hii 5 hakuna mtu ambaye ajapata somo kwamba katiba bora ni muhimu kwa taifa.

Angalia tulivyozimiwa bunge kinyume, Watu walivyovunjiwa nyumba kinyume kimara na etc, bunge lilivyoendeshwa ovyo, CAG alivyofukuzwa kazi kwa dharau, Magufuli kavunja katiba mara kibao mpaka kwenye kuteua wabunge.

Bila kuacha uoga na kuingia street sioni katiba ya Warioba na Tume Huru.
 
Tangia ujiunge Jf Leo umeongea point hila we ongelea mambo mengine hila usimguse mh Mbowe mwamba wa kaskazini.
 
Watanzania tunatakiwa kujitoa kuitafuta katiba na tume huru kwa udi na uvumba wanasiasa wetu mnawajuwa wenyewe. tunatakiwa kuingia barabarani maelfu kwa mamia kudai katiba ya warioba na tume huru ya uchaguzi.
Kwanini?

Jenga hoja bwashee kuingiza watu barabarani siyo swala dogo!
 
Rasmu ya Pili ya Katiba si ipo wameiweka kabatini sijui kwa manufaa ya nani? wakati ilikuwa imefikia hatua za mwisho kabisa....Mungu anawaonaa.!!
 
Mods ingilieni kati hili suala mwenye hii ID wamehack acc yake hawa vijana wa Ufipa zaidi ya miezi 6 kila nikikutana na technically original analalamika michezo michafu ya bavicha
 
Kina lissu aliwadanganya wenzake wakasusia bunge la katiba

ha ha ha, mkuu acha mchezo kwenye hoja nzito...

nakumbuka wakati wa Rasmu ya Pili Mzee wa Msoga aliingia Bungeni (Bunge la Katiba) akabadilika kabisa kama siyo yeye - Katiba ikayeyukia hapo hapo kisa eti wenye nchi yao walimtisha tisha wakamwambia walimkabidhi nchi moja yaani Tanzania - sasa asisubutu wakati anaondoka awakabidhi mbili yaani Zanzibar na Tanganyika.

Mzee wa watu kama mjuavyo hanaga maugonvi na watu akaona akubali yesheee!! Rasmi hiyooo ikawekwa kabatini hadi wa leo.
 
Kwani Mbowe ndie mwenye mamlaka ya kuleta katiba mpya?

Sijaona popote ulipomuunganisha Mbowe kwenye hayo maelezo yako, zaidi ya kupachika tu jina lake ili u-balance story yako.

Always learn to stand on what you believe, no matter how many will support you, usiwe mwepesi wa kutafuta sympathy isiyostahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Linapokuja swala la Katiba mpya bado hatujapata Chama mbadala Cha kutuongoza kuidai.

Chadema ya Dr Slaa ilionyesha nia ya dhati kupata Katiba mpya na ilikuwa na hoja zenye ushawishi.

Ila hii ya sasa hata kufuata Katiba yake tu ni mgogoro.
 
Nafikiri tunakosea sana tunapoweka msingi wa hoja ya katiba mpya kuwa ni Kupata TUME HURU YA UCHAGUZI hili linafifisha sana hoja ya msingi ya kupata katiba mpya na kuifanya kuwa ni political agenda ya vyama vya siasa pekee.

Tunapaswa kutafuta katiba mpya kwa lengo la kuachieve SOCIAL JUSTICE na kuipa katiba yetu uhalali wa kisiasa (POLITICAL LEGITIMACY ) tukijenga hoja zetu katika msingi huu suala la katiba mpya litakuwa ni agenda ya taifa zima na siyo kundi dogo la jamii.
 
Tulieni makomredi tumedanganywa kwa hila.
Katiba mpya imeyeyuka kwa sababu hakuna utashi wa kisiasa.
Kutumia nguvu bila plan nayo ni shida,tutaishia jela kama China ya Deng Xiaoping na Tiananmen Square
Nani wa kumwamini kwa hili kama Jakaya Kikwete alielianzisha na akalitema nani zaidi yake leo?
 
Mods ingilieni kati hili suala mwenye hii ID wamehack acc yake hawa vijana wa Ufipa zaidi ya miezi 6 kila nikikutana na technically original analalamika michezo michafu ya bavicha
Wewe unijuwi vizuri naona
 
Back
Top Bottom