Sipendezwi na tabia ya watu kurudia maneno kwenye sentensi "Serikali kama serikali"

Sipendezwi na tabia ya watu kurudia maneno kwenye sentensi "Serikali kama serikali"

Manitoba

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Posts
240
Reaction score
17
Sasa hivi imekuwa kama kawaida kuona huu mtindo ndani ya sentensi. Mpaka wanahabari kwenye TV nao wamo. Jana tu nimesikia mmoja akiasa serikali kutoa dawa za bure kwa wenye kisukari akianza na "Serikali kama serikali inabidi ...".

Mifano mingine:

Serikali kama serikali inabidi iwajali watu wake.
Mwanafunzi kama mwanafunzi anatakiwa apende masomo yake.
Mtu kama mtu inabidi uwe makini.
Nchi kama nchi ipiganie amani.
Raisi kama raisi inabidi awasikilize waliomchagua.

Kwani wakisema hivi inabadilisha maana?
Serikali inabidi iwajali watu wake.
Mwanafunzi anatakiwa apende masomo yake.
Mtu inabidi uwe makini.
Nchi ipiganie amani.
Raisi inabidi awasikilize waliomchagua.

Unadhani hii imesababishwa na nini?

Mimi kwa maoni yango ni kwamba mtu anahisi sentensi anayotaka kuitoa haina nguvu sana, sasa anaona kama akiifanya iwe ndefu kidogo inaweza ikawa inanguvu zaidi. Na mara nyingi hii hutumiwa sana pale mtu anapotaka kuasa kwamba kitu fulani kifanyike. Bado sijasikia kitu kama "gari kama gari ikaondoka", maana ntaanguka. lol


Nimetafuta kwa google kuarasa zenye "serikali kama serikali", nikapata hizi:

Parliament of Tanzania

Parliament of Tanzania

http://watanzaniaoslo.blogspot.com/2008/01/jk-eleven-ivunjwe-yote-ansbert-ngurumo.html

http://tarishi.wordpress.com/category/uncategorized/

http://www.ipp.co.tz/ipp/alasiri/2005/02/16/32668.html

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/index.php?id=9433 (Waziri kasema)

http://www.raiamwema.co.tz/08/04/16/rioba.php

http://mjengwa.blogspot.com/2007/12/bao.html

http://www.bunge.go.tz/bunge/ContrLst.asp?vpkey=1189&pterm=2005-2010&index=9
 
check hii sentensi 'binafsi mimi mwenyewe ningetalajia rais kama rais atoe amri wausika wote wa Kagoda Agriculture wawekwe lumande kama hirivyofanyika kwa wausika wengine wa EPA'.
 
Umesahau Mimi kama mimi...

Tatizo la kutumia L sehemu ya R, na R sehemu ya L ni kubwa kuliko nilivyokuwa nikifikiri. Sio rahisi mtu mwenye tatizo hili kurekebika. Yaani ni ngumu kweli.

Kuna wakati huwa nabaki kucheka tu. Mfano mtu akisema "malupulupu" 🙂

.
 
Nadhani kuna umuhimu wa darasa, mwenye kukijua vizuri kiswahili tafadhali asaidie. Kitaalam (taaluma ya kiswahili) ni wakati gani nitumie u katika kuelezea kitendo? Mfano, kwa nini niseme unafanya badala ni hunafanya? huna maana nitaitofautishaje na una maana? n.k
 
Utaelewa nini mtu akisema "malapa wa kibongo"?

Umewahi kuona mtu akitumia R badala ya L au L badala ya R akiandika kwa kimombo? Nahitaji kuona mifano, maana sikumbuki kuona.




.
 
Back
Top Bottom