Sipendi kabisa kusikia ule ujinga wa eti "Simba kashusha kifaa hatari kutoka Nigeria"

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Haya mambo yanakera sana.
Tuliambiwa hivyo kwa Mugalu,Kanoute Bwalya na wengine wengi.Ila cha kusikitisha hao waliosifiwa hivyo wamekuwa wa kawaida sana kiasi kwamba hata vitimu vidogo vinaipania Simba na vinaiweza tu.


Kwa nini msisajili kimya kimya bila misifa miingi ya kudanganyia washabiki?
Hatupendi kudanganywa sisi,kama hamna hela na mnataka kusajili wachezaji kama anaosajili Azam,muache majisifa mfanye kimya kimya kama afanyavyo Azam.
Tunajua kwa sasa tuna mfadhili bahili,hata kama ana hela ni zake.
Ukweli mchungu ni kwamba matajiri wa kihindi ni mabahili na hakuna hata mmoja anayemiliki timu kubwa yenye mafanikio.

Kwa sasa ufalme tuwaachie yanga tu tuache kudanganyana kwenye mitandao,mtu anaingia na matumaini halafu anakutana na utopolo.Mjue mtaua watu kwa presha ni bora muwe kimya kama Azam ama Namungo.Siyo kutudanganya ooh mchezaji hatari kuliko Adebayor..sijui kiungo hatari kuliko Chama..na ujinga mwingi kama huo.
 
Hamia wananchi ndugu,huku hakuna mberenje mberenje,ukiambiwa kifaa kifaa kweli,fanya uamuzi upunguze msongo🏃🏃🏃🏃🤔🤔🏃🏃🏃🤔😂
 
Mmesema hamtaki hata kusikia usajili wenu wenyewe basi msisajili kabisa [emoji848]
Joyce kikuku na Aziz Kinyesi awa ni wachezaji wapya wa Yanga unawajua?,kama unawajua wazungumzie hawa kwanza tuwajadili.
 
Hamia wananchi ndugu,huku hakuna mberenje mberenje,ukiambiwa kifaa kifaa kweli,fanya uamuzi upunguze msongo[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji848][emoji848][emoji125][emoji125][emoji125][emoji848][emoji23]
Mwambie huyo haelewi kitu tuliambiwa kinashuka kifaa mugalu na tukaona balaa lake
 
Natumaini una cadi ya uanachama, kama huna acha malalamiko
 
ndo maana tumehamia yanga mkuu team inayoendeshwa kiuweledi na tajiri asiye na makandokando yenye wachezaji high class wanaoogopeka afrika nzima, hamia yanga mkuu
 
Kwa hiyo kama wamesajili mchezaji hatari wasiseme?
Si ndiyo hapo sasa! Mfano huyu Victor Akpan! Yaani ni bonge la kifaa kutoka Nigeria na Coastal Union!
Hakika simba ya msimu ujao itatisha sana pale katikati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…