Sipendi - Special thread

Window7

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
4,098
Reaction score
3,038
Kuna tabia ndogo ndogo ambazo zinakera kwenye jamii lakini unashindwa kumuambia mtu live Kutokana na umri hadhi au aibu juu yake lakini vinakukera kila siku.

Kupitia uzi huu naomba tufikishe ujumbe kwa woote wenye hizo tabia wajirekebishe.. Au tujirekebishe pia kama tupo humu.

Naanza na hizi;

1.Sipendi baba kumbeba mtoto wake huku anavuta sigara.

2.Sipendi kila ukifika usiku mtu anakutext umelala.

Mwisho tunasema "Acha hiyo ni tabia mbaya"
 
Sipendi mtu anakubeep alafu mnampigia anakuuliza wewe nani?
Sipendi mwanamke anakuomba salio una mpa alafu anakubeep tena ili akwambie asante.
Sipendi anapeng'a makamasi alafu anapukutia mikono.

Sipendi mtu umelala naye usiku alafu anakoloma kama chura.
 

Hahahaaa mkuu umenichekesha sana leo aisee jf member ni raha sana
 
Mi sipendi tabia ya mtu kuwa na id yake humu hachangii mada yoyote hata kusema "hi" lakini kazi yake kwenda pm za watu kuwatongoza sipendi kabisa hii tabia kama ni wewe badilika!!!!!!!!
 
.Sipendi watu wanaoshabikia vitu visivyo kuwa na faida kwake na kwa jamii kwa ujumla mfano mtu kushabikia vifo vya watu
Sipendi watu wajuaji hasa humu JF.. una kuta mtu anampangia mwenzie kitu cha kufanya wakati hata hajaombwa kumpangia..

Sipendi watu wanaochukia au wanaotenga wenzao kwa sababu ya dini, kabila, elimu nk.
Tena sipendi watu wanaoziona dini zao ni bora kuluko za wengine.. pumba....vu zaooo
 
Mi sipendi tabia ya mtu kuwa na id yake humu hachangii mada yoyote hata kusema "hi" lakini kazi yake kwenda pm za watu kuwatongoza sipendi kabisa hii tabia kama ni wewe badilika!!!!!!!!

Hi! nimebadilika mkuu
 
Sipendi tabia ya midume mizima kuomba omba bia bar.kama huna hela baki om upige story na wife.!

Ahaha hii inaboa sana kuna wakati mtu unataka kutoa lock tu mtu anakuwekea kibanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…