Sipendi wanaume mwenye uwezo mkubwa ni moja ya sifa ya mwanaume anaemtaka Wema Sepetu

Sipendi wanaume mwenye uwezo mkubwa ni moja ya sifa ya mwanaume anaemtaka Wema Sepetu

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Msanii wa filamu, Wema Sepetu ameibuka na kudai kwamba yeye si mwanamke ayependa wanaume wenye uwezo mkubwa kama tuhuma dhidi yake zinavyoeleza.
“Mimi napenda mwanaume anayejielewa,mwenye upendo na mchapakazi,

Ikitokea ana fedha itakuwa imetokea,lakini si mwanamke ninayependa pesa kuliko utu na mapenzi ya kweli,”alijinadi Wema Sepetu na kuongeza;“unajua pesa sio kikwazo katika maisha yangu, kwa sababu najua kuitafuta hivyo siwezi kubweteka kwa kutaka.

Mwanaume mwenye pesa, hilo kwangu halipo, ninachotaka awe na upendo na thamani kwangu awe mfariji na si maumivu hata hivyo, Wema alisema hatoacha kuomba kila kukicha Mwenyezi Mungu ampatie mwanaume mwenye sifa anazotaka ili roho yake isuuzike.
 
Alishindwa kutumia kichwa alipokuwa miss na still hot in town. Akaamua shortcut ya kudanga, nako pia alishindwa kujiweka vizuri.

Zile trip za Dubai na Clement, kukaa 5*hotel na kununua viatu vya $3,000 sasa ni Hadith
 
Sikuhizi ana rub shoulders na RC wa Dar
Anataka kupunguza makali ya kesi yake ya bangi. Mi niliwaambia watu miaka 5 iliyopita kwamba Wema hawezi kuwa na mwisho mzuri. Hao walikuwa wapambe wake wakati wanajiita team Wema. Nikawambia ninyi mnamdanganya maana kama kweli mnampenda mgempa ushauri ila naona kama mnazidi kumpoteza kwa kumulewesha sifa. Hawakunielewa. Sasa wapambe wamesepa, hawana habari naye.

Nililogundua wasichana wa rika la Wema walimchukulia Wema kama role model na wao walitaka wawe kama yeye na wengine kujaribu kuiga mambo yake. Ukweli haupingiki alikuwa na influence kwa wasichana wengi kimtazamo na kitabia. Naona wengi kama wamedoda na wanahaha kutafuta ndoa. Nyodo walizokuwa nazo nao kama zimeyeyuka na sasa hivi ni kama akili ndo zinawarudia baada ya kukaa uhamishoni kwa miaka kadhaa.
 
Wema na Martin Wangepiga pesa nzuri sana kwa influence waliyokuwa nayo. Angeweza kuwaona line yake ya nguo, balimi wa watoto yatima. Business empire kwa kifupi.
Fikiria kile anachofanya Hadija Mwanamboka, Wema asingeshindwa kuvifanya
 
Alitegemea vya kupewa sana. Hata kama angefanya bado angefilisika kwa matumizi yake ya pesa. Hiyo biashara ya kuweza kutawanya pesa namna hiyo l. Asingeweza kupata faida ya kumfanya aishi na standard aliyoitaka. Mwishowe angefilisika. Biashara inataka nidhamu na ndio maana unaona biashara zote alizoanzisha zilimshinda.
 
Wanaume wamestuka.. Hawataki mtu mwenye sifa kama za wema ndio maana ameamua kujinadi.. Endelea mamaa
 
Msanii wa filamu, Wema Sepetu ameibuka na kudai kwamba yeye si mwanamke anayependa wanaume wenye uwezo mkubwa kama tuhuma dhidi yake zinavyoeleza.
“Mimi napenda mwanaume anayejielewa,mwenye upendo na mchapakazi, ikitokea ana fedha itakuwa imetokea,lakini si mwanamke ninayependa pesa kuliko utu na mapenzi ya kweli,”alijinadi Wema Sepetu na kuongeza;
“Unajua pesa sio kikwazo katika maisha yangu, kwa sababu najua kuitafuta hivyo siwezi kubweteka kwa kutaka mwanaume mwenye pesa, hilo kwangu halipo, ninachotaka awe na upendo na thamani kwangu awe mfariji na si maumivu.”
Hata hivyo, Wema alisema hatoacha kuomba kila kukicha Mwenyezi Mungu ampatie mwanaume mwenye sifa anazotaka ili roho yake isuuzike.
Aache uongo, mbona alikopita hawako hivyo??
 
Umli ukisha kwenda ni kawaida kwa wanawake kurekebisha cv na kupunguza vigezo. Saikolojia ya mwanamke imekaa vibaya sana. Ni kuwahurumia tu sio kuwasema vibaya, hata mungu aliagiza wanaume kuwa mta watawala kwakuwa alijua mapungufu yao.
 
Back
Top Bottom