Siri 11 usizozijua za Maisha katika kufanikiwa kwako

Siri 11 usizozijua za Maisha katika kufanikiwa kwako

Kuwite94

Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
18
Reaction score
117
SIRI KUMI NA MOJA (11) USIZOZIJUA ZA MAISHA NA MARAFIKI ZAKO, KATIKA
KUFIKIA MAFANIKIO YAKO.

1. SIRI YA KWANZA

Tengeneza connection na watu usitengeneze urafiki, Iko siku marafiki uliowatengeneza watakugeuza Chakula Cha kula maana "kikulacho kinguoni kwako!", Siyo rahisi rafiki akakubali upate zaidi yake.

2. SIRI YA PILI

Usimwamini sana rafiki yako ,kwa sababu huyo rafiki yako ana rafiki yake ambaye Wewe si rafiki yako!, Kama hunielewi subiri siku umseme bosi wako akurekodi halafu amrushie boss wako then boss wako ukurushie. Utatamani kufa.

3. .SIRI YA TATU

Kuna njia tatu tu za kufanikiwa maishani. Njia hizo ni 1.bahati, 2.kipaji 3.bidii yenye akili!, Jitafute ulipo! Huna bahati, huna kipaji halafu unalala mchana?

4. .SIRI YA NNE:
Ukiwa na marafiki watano majambazi tegemea kuwa jambazi wa sita; ukiwa na marafiki watano wahuni tegemea kuwa muhuni wa sita, ukiwa na marafiki watano mabilionea tegemea kuwa bilionea wa sita; kasheshe ni masikini kumpata rafiki bilionea maana wahenga walisema ndege wanaofanana huruka pamoja.

5. SIRI YA TANO
Ukiona kila mtu anakurushia mawe usijifariji kwamba mti wenye matunda ndo unaopigwa mawe, kuna miti mingine inapigwa mawe kwa sababu ina nyoka! Kikubwa jitathimini pengine wewe ni Mfalme mwenye mkia ila hujauona.

6. SIRI YA SITA

Kuwa makini sana na watu wanaosema tuko nyuma yako maana ukigeuka unaweza usiwakute Kama kivuli chako mwenyewe ikifika usiku kinakukimbia vipi huyo mtu asiyekula kwako?

7.SIRI YA SABA

Ili ufurahie maisha, jifunze kujinyenyekeza na siyo kujikomba!, Unyenyekevu ni kiwango cha juu kabisa cha matumizi ya akili, kujikomba ni kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya akili! Moja ya madhara ya kujikomba ni kuishi maisha yako hovyo!

8.SIRI YA NANE

Kabla hujafanya maamuzi jitahidi kupata ukweli wa jambo kutoka pande zote. Leo hii watoto wengi hawana mahusiano na baba zao kwa sababu ya kusikiliza ufundi wa mama zao katika kusimulia mabaya ya baba zao! Huyajui ya mama yako kwa sababu baba yako.

alichagua kuyaficha! Kama unamchukia baba yako hebu muombe msamaha kwanza halafu mwambie akusimulie ya mama yako...(Inaendelea-1).


9. SIRI YA TISA

Mlango mmoja ukifungwa usihangaike kuufungua, unaweza ubomoa bure. Pita hata dirishani maana kisicho riziki hakiliki! Asiyekupenda muache aende.

zake, tena mpe na nauli.

10.SIRI YA KUMI

Hata kama umeishafika mbali kiasi gani, ukijua umepotea njia rudi kuliko kupotea jumla! Kuanza upya si ujinga. Bora uanze upya ufike salama kuliko kuendelea usifike.

11. SIRI YA KUMI NA MOJA

Haijalishi umri umekwenda kiasi gani kama una ndoto kichwani amka ukaitekeleze kwa sababu umri ni namba tu na uzee hisia tu. Haijalishi mashavu yamelegea kiasi gani ukitimiza ndoto watayabusu tu.
 
Wakuu nifundisheni namna ya kutengeneza connection, ili nami nifanikiwe.
 
Ahsante kwa miongozo, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
JF ni nyumba ya busara, Asante sana Founder of this platform.
 
Back
Top Bottom