Siri 5 Kuhusu Majambazi ya Amboni Tanga

Siri 5 Kuhusu Majambazi ya Amboni Tanga

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
IMEBAINIKA! Mapambano na wahalifu wanaosadikiwa ni magaidi kwenye Kitongoji cha Amboni jijini Tanga, yaliingia sura nyingine baada ya wakazi wa kitongoji hicho kuvujisha siri tano.

▶WALIKUWA NA WAPENZI
Kwa mujibu wa mkazi mmoja wa eneo hilo, wahalifu hao walishakuwa na wanawake kwenye eneo hilo, hivyo kama walikuwa na mpango wa kujua siri za Jiji la Tanga ilikuwa rahisi sana.“Wale watu baadhi yao walikuwa na wanawake Amboni. Na hilo limebainika baada ya kutokea kwa mapambano na wao kukimbia kwani na mmoja wao aliyekuwa na mwanamke hajaonekana tena,” .

▶WALIKUWA WAKICHENJI DOLA KILA BAADA YA SIKU MBILI
Habari kutoka kwa mkazi mwingine zilidai kuwa, baadhi ya wahalifu hao walikuwa wakienda mjini Tanga kila mara kwa shida ya kuchenji dola za Kimarekani.“Kuna wakati nilikutana na watu wakisema wanatafuta maduka ya kuchenji dola za Marekani, wakakosa na kwenda mjini. Wakawa nawaonekana mara kwa mara tena wakienda mjini,inasemekana kila baada ya siku mbili.

▶TABIA ZAO
Mjumbe wa nyumba kumi wa kitongoji hicho, Idd Suleiman alisema kuwa, kulikuwa na watu walioonesha dalili kwamba si wenyeji wa eneo la Amboni.“Mbaya zaidi, watu hawa walikuwa na tabia ya kuonekana nyakati za usiku, kama ni mchana basi si kwa uwazi mkubwa. Nilijaribu kuwafuatilia nikidhani ni wakazi wa mtaani kwangu lakini sikuwahi kuwajua,” alisema mjumbe huyo.

▶WENGI WAO NI WAREFU, WEMBAMBA, WEUSI
Mjumbe huyo alizidi kusema kuwa, watu hao waliokuwa wakionekana maeneo hayo ni wembamba, wengine ni warefu na weusi lakini walionekana wakakamavu muda wote.
“Kusema kweli kama sisi wananchi tungekuwa watafiti sana na kutoa taarifa polisi labda wangekamatwa mapema kwani watu hao walikuwa hawafanani na sisi wakazi wa eneo hili ambao tunajuana,” alisema.

▶NI KWELI WAMEKIMBILIA KENYA?
Naye mzee Juma Kabari ‘Mapipa’ yeye alisema kuwa, anavyojua miaka ya nyuma kuna Mzungu aliwahi kumpoteza mbwa wake ndani ya mapango hayo.“Sasa katika kumtafuta hakumpata, baadaye akaja kuonekana Mombasa nchini Kenya. Ikagundulika kuwa, kuna pango moja ambalo linatokea Mombasa. Nina wasiwasi kwamba, hata hawa jamaa (wahalifu), huenda walipita chini kwa chini wametokea Mombasa, ndiyo maana hawajawakamata.

“Watu waliodaiwa kukamatwa juzi, siamini kama kweli ni miongoni mwa wale ambao walitoa upinzani kwa askari wetu Ijumaa iliyopita,” alisema mzee Mapipa.
 
kwahiyo tukio lilikua la kweli?
 
Endeleeni na hizo stori za kutunga, lakini mkae mkijua watu wa leo si watu wa miaka hiyo na si watu wa kudanganywa kirahisi hivyo
 
huu sasa ujings.pango lifike mpaaka kenya washindwe kulifuatilia hadi kujua linatokeza wapi?
 
I like Eric Shigongo he is agood writer east Africa! another director of 007! Ps Amboni it was affiction or cinema made by bongo movie? let as know bwana:eyebrows:
 
I like Eric Shigongo he is agood writer east Africa! another director of 007! Ps Amboni it was affiction or cinema made by bongo movie? let as know bwana:eyebrows:

acha tusubiri epsode inayofata labda tunaweza kujua starring ni nani katika hii series ya THE AMBONI TERRORIST
 
Back
Top Bottom