Siri gani ambayo imefichwa na Mungu katika damu ya binadamu na wanyama?

Siri gani ambayo imefichwa na Mungu katika damu ya binadamu na wanyama?

Kaunara

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
249
Reaction score
452
Wa JF habari zenu!!

Kuna jambo ambalo linanisumbua ambalo nahitaji ufafunuzi wenu hasa wale watu ambao wamejaliwa kupewa jicho la tatu katika imani ya dunia hii.

Hapa dunian kuna watu ambao wana Iman mbali mbali sana na Dini tofauti sana kwa hapa naongelea wale ambao wana Iman kuwa Mungu (Wakristu) yupo na wale wenye Imani kuwa kuna nguvu za giza ambazo nazo pia zinafanya kazi, Kama wewe ni mwana JF na kati ya izo Iman nilizo sema hapo juu huamini kama zipo basi hii topic haikuhusu, ni wale tu ambao wana amini kuna uwepo Mungu na nguvu za giza.

Nilichotaka kuuliza mimi kwa watu wenye imani hizi mbili nilitaka kujua kuna siri gan ambayo ipo ndani ya damu ya Binadamu na wanyama?

Nauliza hivi kwa kuwa Iman hizi mbili nimeona watu ambao wanatumia nguvu za giza hasa wanaoenda kwa waganga wa kienyeji au wanaofanya matambiko wanaambiwa wapeleke mnyama achinjwe atoe damu au atoe damu yake mwenyewe maana ya kupigwa chale ili lile jambo ambalo analitaka liweze kufanyika. Wengne wanatoa damu za binadamu wenzao ili waweze pia kufanikiwa.

Kwa upande wanaoamini Mungu yupo hasa Wakristu wanasema Yesu Kristu alimwaga damu yake ili tupate kukombolewa na kwakufanya ivyo bas ukiomba chochote kwa kupitia Yesu Kristu utapata na huitaji tena kulipia.

Nilitaka kujua kwanini damu imekuwa na thamani kubwa sana katika Imani hizi. Asanteni.
 
Mkuu damu ni ndo uhai wa kiumbe, kwa hiyo inapotumika kama sadaka au tambiko au agano fulani inakuwa na nguvu ya kuakisi au kutenda kile kilichokusudiwa, damu ni injini ya kiumbe hai, injini ikitoka gari, ndege, pikipiki au chombo chochote cha moto hakiwezi kufanya kazi, kwa hiyo ukitoa damu ktk mwili wa binadamu au kiumbe chochote kile inakuwa na nguvu ya ku reflect uhalisia wa kile kinachonenewa!

Ndo maana mtu yeyote aliyewahi kuua akili yake huwa kama mwendawazimu, damu huwa inalia na kudai, ukimuua mtu damu yake inakulilia maana ndo uhai wake! Hiyo ndo nguvu ya damu.

cc:mshana jr,pasco,rakims,mzizi mkavu.
 
Masharti nayo sio mchezo. Bennie 369 we unahusika hapa?
 
Last edited by a moderator:
Ukitaka kujua thamani ya damu imwagike japo kdogo 2 utaelewa!
 
Hata wewe ukijitolea damu yako,lazima CCM tuipige chini!.nadhani usha pata jibu.
 
Damu inathamani kubwa sana, hutumika kutakasa, au kuokoa. Kama damu ikitumiwa vibaya pia yaweza kuwa laana au mkosi hivyo sio vyema kumwaga damu pasipo kuwa na sababu. Nahata ikitokea unataka kuchinja kitoweo, mfano kuku au mbuzi n.k unatakiwa au unashauriwa kuifunika au kuitupa vyema damu kwani damu inanguvu sana kuliko tufikiriavyo.

Jesus Christ, the faithful witness, the first-born of the dead, and the ruler of the kings of the earth. To Him who loves us, and released us from our sins by His blood (Rev. 1:5). Damu inanguvu mno!

The blood is the life of the flesh (Lev. 17:11), and it is through the atoning blood of Christ that the believer receives redemption (I Pet. 1:18-19), forgiveness (Eph. 1:7), justification (Rom. 5:9), spiritual peace (Col. 1:20), and sanctification (Heb. 13:12)

Blood is not precious in its own right, but because it is equated with life. The principle conveyed first in Leviticus 17 is that "the life is in the blood." Pressing this matter further, then, we can safely conclude that God values life as precious. Blood is the instrument through which atonement is made, which spares the life of the sinner. Life is thus precious to God, as well it can be for it was God who created all life (Gen. 1-2).

If blood (and, as we have seen, life) is precious, then there are several areas of application. The first application is that God values all life. Let the abortionist take note! Let those who talk about "quality of life" beware. God is the giver of life; Satan, through sin, seeks to destroy it. Let us prove to be on God's side by seeking to save life, rather than to destroy it.
 
Wa JF habari zenu!!

Kuna jambo ambalo linanisumbua ambalo nahitaji ufafunuzi wenu hasa wale watu ambao wamejaliwa kupewa jicho la tatu katika imani ya dunia hii.

Hapa dunian kuna watu ambao wana Iman mbali mbali sana na Dini tofauti sana kwa hapa naongelea wale ambao wana Iman kuwa Mungu (Wakristu) yupo na wale wenye Imani kuwa kuna nguvu za giza ambazo nazo pia zinafanya kazi, Kama wewe ni mwana JF na kati ya izo Iman nilizo sema hapo juu huamini kama zipo basi hii topic haikuhusu, ni wale tu ambao wana amini kuna uwepo Mungu na nguvu za giza.

Nilichotaka kuuliza mimi kwa watu wenye imani hizi mbili nilitaka kujua kuna siri gan ambayo ipo ndani ya damu ya Binadamu na wanyama?
Nauliza hivi kwa kuwa Iman hizi mbili nimeona watu ambao wanatumia nguvu za giza hasa wanaoenda kwa waganga wa kienyeji au wanaofanya matambiko wanaambiwa wapeleke mnyama achinjwe atoe damu au atoe damu yake mwenyewe maana ya kupigwa chale ili lile jambo ambalo analitaka liweze kufanyika. Wengne wanatoa damu za binadamu wenzao ili waweze pia kufanikiwa.

Kwa upande wanaoamini Mungu yupo hasa Wakristu wanasema Yesu Kristu alimwaga damu yake ili tupate kukombolewa na kwakufanya ivyo bas ukiomba chochote kwa kupitia Yesu Kristu utapata na huitaji tena kulipia.

Nilitaka kujua kwanini damu imekuwa na thamani kubwa sana katika Imani hizi. Asanteni.

Hebu tafuta post yangu moja ya kiapo cha damu...au ngoja nikiipata nitakutag
 
Damu inadhaman kubwa kwa sababu binaadamu ameumbwa kutokana na pande la damu.

Na kuhusu ushirikina na uchawi inatumika km link ama connection of spirit milango inakuwa wazi.

Jengine damu inatumika km kinywaji ila damu ya binaadamu inadhaman kubwa ikitumika inaleta strong power na urahisi wa kufanyika mambo yao kiuchawi
 
Wa JF habari zenu!!

Kuna jambo ambalo linanisumbua ambalo nahitaji ufafunuzi wenu hasa wale watu ambao wamejaliwa kupewa jicho la tatu katika imani ya dunia hii.

Kwa upande wanaoamini Mungu yupo hasa Wakristu wanasema Yesu Kristu alimwaga damu yake ili tupate kukombolewa na kwakufanya ivyo bas ukiomba chochote kwa kupitia Yesu Kristu utapata na huitaji tena kulipia.

Mimi ni Mkristo, Mchungaji na Mwanasayansi. Hakuna lolote kwenye damu yeyote, nothing supernatural. Ni imani za watu tu.

Kitu chochote unaweza ukakifanya kuwa na nguvu ukiamini. Ndio mana wahindu wana Mungu wa kila kitu.

Ki uhalisia damu ni tishu (mkusanyiko wa seli) na hilo tu.
 
Mkuu Kaunara, nikianza kwny kuchanjw chale damu yko inatumika kuwek mkatab ni kam sahihi yako kwenye ulimwengu wa kiroho, damu yako ni uniq so kma unatak jambo lifanyike esp yale mazito au makubwa ya rohoni unatakiwa uthibitishe kwa kutoa damu kama ishara ya kulidhia.

Tukija kwenye kuagizwa damu za viumbe, kama ilivyo damu ni uhai na uhai una energy n energy hii ndiyo price inayokuwa requested na roho (jini, mzim n.k) ili iweze kufanya kazi yako.

Kuna kazi zingine ni ngumu , kubwa hapo hizo roho uhitj energy kubwa kukamilisha hivyo price huwa kubwa pia.

mshana jrkazia hapo.

Mtaniwia radhi kwa uandishi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom