Siri iliyo wazi ya hatari ya bitcoin: Sakoshi Nakamura anaweza/wanaweza kuiangusha fedha hii watu wakapata hasara.

Siri iliyo wazi ya hatari ya bitcoin: Sakoshi Nakamura anaweza/wanaweza kuiangusha fedha hii watu wakapata hasara.

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Makerekebisho katika chapisho (ERRATA):
Jina la creator wa bitcoin ni SATOSHI NAKAMOTO SIO SAKOSHI NAKAMURA kulikuwa na kosa la kiuandishi.
Credit to Ngondonyoni

Habari ndugu wana JF.

Heri ya mwaka mpya 2018.
Niende moja kwa moja kwenye maoni ya wadau mbali mbali kuhusu ukweli wa usalama wa sarafu ya kidigitali ya bitcoin pengine na nyingine maarufu.

Unajua kuna wimbi kubwa la matangazo ya hizi sarafu ambazo wanasema zinakupa uhuru wa kutobanwa au kushurutishwa au kuzuiwa na taasisi yoyote ya kifedha ukiamua kuhifadhi/kumiliki fedha zako kwenye mfumo wa bitcoin.

Lakini ukweli ni kwamba watu hawasisitizi sana kuufahamisha umma kuhusu hatari ya kuja kuanguka thamani ya hii pesa na ghafla watu walioinunua kupata hasara kubwa na pengine kufilisika kabisa.

Hatari iko hivi,
Muanzilishi au waanzilishi ni mtu au watu wanajiita jina lisilo halisi pseudo name SATOSHI NAKAMOTO.

Baada ya huyu muasisi ambae ni programmer kuweka whitepaper kuhusu wazo hili la bitcoin litakavyofanya kazi, akaweka kwenye mtandao program halisi inayowezesha hii kitu yaani block chain kwa ajili ya bitcoin mine na digital wallet.
Kisha akaweka iwe wazi kwa programmer yeyote kuijadili na kuongeza chochote ili kuiboresha.

Bitcoin ikapata mapokeo mazuri lakini wakati wote huu huyu Satoshi Nakamoto hakujulikana sura yake halisi ni nani na anatoka wapi au anaishi wapi.

Je huyu ni mtu mmoja au kikundi cha watu? Katika kutafuta utambulisho halisi wa huyu mtu/watu ilionekana kwenye ile whitepaper aliyorusha mitandaoni kuna misamiati na misemo (slang) za kiingereza kama cha Britain. Lakini hilo jina unaliona ni la kijapani.

Kwa hakika jambo moja tu lilifahamika kuhusu yeye au wao ni kwamba alikuwa mtu mwenye akili sana na ujuzi wa hali ya juu wa hisabati, masuala ya kifedha na utaalamu wa juu zaidi wa teknilojia ya mawasiliano hasa kwenye kubuni na kutengeneza mifumo yake.

Ukweli mwingine ni kwamba yeye/hao waliisaidia dunia kutatua changamoto kubwa itokanayo na hii mifumo yetu ya kifedha iliyopo.

HATARI INAKUJA WAPI?
Wakati wote ambao huyu mtu asiye julikana akiwa anatuma michango yake kuhusu bitcoin alifanikiwa kufanya mining ya kuchimbua hizi sarafu za bitcoin karibu 980,000 na kuzimiliki yeye peke yake (au wao peke yao) ambazo thamani yake ni wastani wa $5.8 billion.

Kuna siku moja HUYU ASIYEJULIKANA aitwae Satoshi Nakamoto alihamua ghafla kusitisha michango yake mtandaoni na kusema ameachana na masuala haya na kugeukia mambo mengine.
Tangu wakati huo jamaa ametoweka na hakuna anaejua yeye ni nani na yupo wapi.

Jambo la kuogofya ni kwamba siku anatoweka au potea hakuondoka bure, kaondoka na huu mzigo wake wa kutosha wa bitcoin hivyo siku akihamua kuziuza kwa uwingi kwa pamoja basi zitajaaa sokoni na kushusha kabisa bei au thamani ya hii sarafu.

Watu wa uchumi au biashara au sekta za kifedha wanajua athari ya uwingi uliopitiliza wa bidhaa fulani sokoni. Au athari za kuchapisha fedha nyingi ovyo.

Lakini ngoja niwasaidie ndugu zangu na mimi tusiosomea uchumi au biashara.

Unaona nini kinatokea wakati wa msimu wa matunda kama embe, nanasi au tikiti. Mwanzo bei inakuwa kubwa lakini zikiwa nyingi basi bei hushuka chini kabisa na wakati mwingine hukosa wateja na mkulima au mfanyabiashara wa hayo matunda hupata hasara kubwa. Tunakumbuka biashara ya nyanya mwezi wa sita hadi wa 9 mwaka 2016 zilijaa zikaleta kilio. Wengi tuliona malalamiko kwenye vyombo vya habari.
Vivyo hivyo Simu, TV zilipoingia zilikuwa zinamilikiwa na wachache na bei ilikuwa juu. Sasa zinazalishwa kwa wingi kiasi kwamba karibu kila mtu anamiliki hivi vitu na kusababisha kufurika sokoni na bei imeshuka sana.

MFANO MWINGINE WA UTAPELI WA BIASHARA YA SARAFU HAPA TANZANIA UFANANAO NA HATARI YA KUANGUKA BITCOIN (AU DIGITAL CURRENCY YEYOTE)
Kuna bishara moja ya kufurahisha na imefilisi wengi sana hapa nchini na muundo wake unafanana sana na hii bitcoin.
Biashara hii si nyingine bali ni fedha za Rupia za mjerumani.
Kuna matapeli hutangaza kuzinunua kwa bei nzuri na kweli mwanzo hufanya hivyo. Hununua kwenu mara kadhaa na kila awamu hupandisha bei.
Majanga yanafuata baadae ambapo mtu tofauti na yule mliye muuzia huja kuleta habari anazo rupia nyingi anaziuza lakini bei kubwa mara tano ya bei ya mwisho mliyouuza sarafu zenu.
Wakati huo huo yule mnunuzi wenu wa siku zote huja kutangaza anahitaji sarafu nyingi zaidi kwa bei mara 7 ya bei ya mwanzo kwa vile zimekuwa adimu na amepata mteja mzuri sana.
Ninyi kwa kutojua huyu ndio kikundi kimoja na yule alieyatangaza anazo mnakimbilia kwenda kuzinunua zote toka kwa huyu alietangaza anazo tena kwa mara tano ya bei mliyouza za kwenu mara ya mwisho.

Mkisha nunua na kurudi kumtafuta mteja wenu anawaambia mnunuzi wake hapatikani au yeye mwenyewe anatoweka. Huku ninyi mna sarafu isiyo na matumizi, naye anatoweka kusikojulikana na utajiri mkubwa aliovuna kitapeli toka kwenu. Anatoweka kama MTU ASIYE JULIKANA kama SATOSHI NAKAMOTO. Sijui utaenda kumuuzia nani.

MTAZAMO NA MAONI, USHAURI WANGU.

Digital Currency haikwepeki na ina faida kubwa sana kwa sasa kuliko hasara.
Lakini tusiwekeze uchumi wetu au rasilimali zetu zote kwenye hizi sarafu za kidigitali maana siku yeyote jambo lililosemwa hapo juu linaweza kutokea.

Pili hapo juu sikuzungumzia kuna uwezekano wa kuwa hacked na ukapoteza au kuibiwa fedha zako zote kwa sekunde moja tu.

Tatizo lingine ambalo hili lipo chini ya uwezo wako kulidhibiti au kulizuia ni kwamba kwa teknolojia ya cryptography iliyotumika ktk biticoin ili uweze kuitumia unapaswa kuwa private key yako. Hii ukiipoteza unakuwa umepoteza fedha zako moja kwa moja na hakuna tena msaada wa kukupa nakala nyingine. Au mtu akiisoma na kuitumia kabla yako basi unaikosa pesa yako kabisa na hakuna mahali watakusaidia kurejesha pesa yako.

Na ubaya wa hizi blockchain hakuna taasisi inayo control au kuwajibika hivyo hakuna wa kumlalamikia akakusaidia au kukurudishia fedha yako kama zifanyavyo benki chini ya taratibu zilizolazimishwa kisheria na banki kuu.

Kuna mfano wa taasisi ambayo ilikuwa hacked (kudukuliwa) na watu kupoteza bitcoin zenye thamani kubwa sana. Japo kwa sasa wamefanya marekebisho ya kuzuia isitokee lakini hiyo haifuti ukweli kwamba kuna siku nyingine itatokea tena.

MAKALA ITAENDELEA WAKATI MWINGINE na nitajikita ktk kuelezea faida zaidi na baadhi ya hatari au hasara zake na mifano halisi.

Kwa sasa naomba katafute documentary inayoelezea faida zaidi na changamoto chache.
Inaitwa Magic Money: The Bitcoin Revolution (2017).

Tukutane wakati ujao .....

Makala hii imeletwa kwa hisani ya vyanzo tofauti mtandaoni na uzoefu wa vurugu za mitaani za watafuta riziki.

Cc: ONTARIO Nyani Ngabu Pascal Mayalla Deadbody The bold
Behaviourist al watan The Boss Cicero avogadro
 
Kwa maoni yangu, hata huyo Satoshi akiibuka akauza hizo 980,000 bitcoins unazosema anazo kwa sasa athari haitakuwa kubwa sana kiasi cha kuangusha market.
Hatari ipo kwenye digital coins nyingine mfano XRP unakuta kwanza ni centralized, pili mmiliki ana like 60% ya coins zote.
 
mkuu upo unaangalia bbc nini? maana mada kama hiyo imepita last 1 hour
Oh, What a coincidence!
Sijaangalia mkuu imetokea tu.
Kwa hakika nilitaka kuandika tangu wiki mbili zilizopita.
 
Duuuh nilikuwa na mpango wa kununua bitcoin umenikata moto
 
nilipata kusoma sehemu mbalimbali kuwa wachumi wengi wanaamini jamaa(kama ni mtu mmoja) ni marehemu maana hajapata kuuza hata bitcoin moja mpaka leo pamoja na bitcoin kuwa juu sana kwa sasa.
 
Titicomb, nimesoma uzi wako. Mashaka yangu mengi sana... Kwanza ni Satoshi Nakamoto, na si Nakamura (Satoshi Nakamoto - Wikipedia). La pili kusema kwamba Blockchain ni hatari kwa sababu hakuna taasisi au control inaonyesha wazi kwamba bado huelewei Blockchain na pia utofauti wa Blockchain na Cryptocurrency. Mambo yote mawili ni mapya kwa wengi na si rahisi kuyaelewa lakini. Cryptocurrency inatumia Blockchain, lakini Blockchain inatumika kwa mambo mengi nje ya sarafu za kidijitali na itatumika kwa mengi zaidi, kuanzia sekta ya Uchumi, ya biashara, ya Bima, ya afya, ya usafirishaji, ya maendeleo, na kadhalika.

Nawaomba wote wenye moyo wa kujifunza mtofautiane Blockchain na cryptocurrency, na kujisomea zaidi. Mimi natumia sana www.blockchaincompany.info lakini tovuti zipo nyingi sana kwa kupata elimu ya kutosha. Jamani tutake tusitake Blockchain inakuja, na lazima tuwe tayari kuitumia ipasavyo. Na sarafu za kidijitali pia zitakwepo, hata kama sasa ni bubble na inabidi kuwekeza kwa uangalifu sana, lakini hatuwezi kuendelea kuishi kama tulipokuwa tunaishi zamani. Akili ni mali.
 
Bitcoin, kuna jamaa ananishawishi sana kuwekeza kwenye hii kitu kupitia VOTREX PROFIT.
Kama kuna mtu anaifahamu vizuri naomba kusahidiwa kuifahamu wakuu
 
Titicomb, nimesoma uzi wako. Mashaka yangu mengi sana... Kwanza ni Satoshi Nakamoto, na si Nakamura (Satoshi Nakamoto - Wikipedia). La pili kusema kwamba Blockchain ni hatari kwa sababu hakuna taasisi au control inaonyesha wazi kwamba bado huelewei Blockchain na pia utofauti wa Blockchain na Cryptocurrency. Mambo yote mawili ni mapya kwa wengi na si rahisi kuyaelewa lakini. Cryptocurrency inatumia Blockchain, lakini Blockchain inatumika kwa mambo mengi nje ya sarafu za kidijitali na itatumika kwa mengi zaidi, kuanzia sekta ya Uchumi, ya biashara, ya Bima, ya afya, ya usafirishaji, ya maendeleo, na kadhalika.

Nawaomba wote wenye moyo wa kujifunza mtofautiane Blockchain na cryptocurrency, na kujisomea zaidi. Mimi natumia sana www.blockchaincompany.info lakini tovuti zipo nyingi sana kwa kupata elimu ya kutosha. Jamani tutake tusitake Blockchain inakuja, na lazima tuwe tayari kuitumia ipasavyo. Na sarafu za kidijitali pia zitakwepo, hata kama sasa ni bubble na inabidi kuwekeza kwa uangalifu sana, lakini hatuwezi kuendelea kuishi kama tulipokuwa tunaishi zamani. Akili ni mali.
Mkuu kwanza ahsante sana kwa kunirekebisha kuhusu jina la huyo mtaalam asiyejulikana.

Sio Satoshi Nakamura bali Satoshi Nakamoto kama ulivyosema.

Nitarekebisha haraka sana sababu hilo kosa kubwa ktk uandishi wa habari zenye utata kama hizi.

Makosa hayo yanaweza kusababisha habari yote kuto aminika.

Kuhusu hatari ya huyo jamaa kuja kuishusha thamani bitcoin bado nasimamia msimamo huo.

Umuhimu wa hii sarafu au digital currency zingine nimekwisha sema ni muhimu na haikwepeki hata iweje.

Nimesema faida ni nyingi kuliko hatari na hasara. Nimesema faida ni kubwa kuliko hasara.

LAKINI PAMOJA NA UMUHIMU NA FAIDA ZOTE HATARI MBILI NILIZOSEMA BADO ZIPO PALEPALE.

Mwisho kwa kuonesha sizipingi nimeweka na Documentary Movie mpya kabisa inayoeleza au kusifia faida zaidi na kuacha kwa makusudi kuitaja hatari moja inayoweza kufanywa na SATOSHI NAKAMOTO any time (t) akihamua kuwaletea kilio watumiaji wa bitcoin.
Humo wametaja hatari ya kuwa hacked au ukipiteza private key yako kizembe.

Nimesema watu watumie hii fursa lakini wasiwekeze mzigo wote. Likitokea tukio baya wasiseme hawakujua au hawakuambiwa.

Ukoseaji wa jina unatokana na kulipenda sana jina la NAKAMURA mtaalamu maarufu aliye mkamata hacker maarufu nchini marekani. That is another story to tell. Na pia nilikuwa nimechoka sana akili nimetoka kukesha.

Ahsante tena kwa kunisahihisha jina.

Mod One , Mod Two naomba mnisaidie ku-edit title ya uzi iwe hapo kwenye Sukashi Nakamura isomeke Sukashi
Nakamoto.
 
Bitcoin ipo toka 2009
Ni kweli na itakuwepo angalau mpaka mwaka 2140 na bitcoin zinafaida zaidi kuliko hasara au hatari ya kufilisi watu. Lakini hii hai ondoi ukweli kwamba SATOSHI NAKAMOTO anaweza kuitingisha dunia la soko la bitcoin siku yeyote akiamua kufanya hivyo.
 
Usiwekeze kiasi kikubwa kwenye hii kitu ili hata ukipata hasara isikuyumbishe ukapata msongo wa mawazo , nmekumbuka msemo mmoja wa Kichina... "Don't put all your eggs in one basket"
 
Ni kweli na itakuwepo angalau mpaka mwaka 2140 na bitcoin zinafaida zaidi kuliko hasara au hatari ya kufilisi watu. Lakini hii hai ondoi ukweli kwamba SATOSHI NAKAMOTO anaweza kuitingisha dunia la soko la bitcoin siku yeyote akiamua kufanya hivyo.
Sure na JF imekua sehemu salama kwa kuelimishana


Cha msingi walio wekeza kwenye bitcoin wawe makini kwasababu mtu unawekeza milion 40 alf unakuja kuta bitcoin imepolomoka.
 
Hatari ya kweli hapo ni moja tu.. hacking, ambayo hutokea pia kny hizi fedha za kawaida kny mabenki.
Wanaposema nobody controls btc, maana yake NOT EVEN huyo mwanzilishi
Mkuu inabidi uende ukafikirie mara mbili juu ya ukweli huu au katafute msaada kwa wachumi waliobobea.
 
Back
Top Bottom