Siri iliyo wazi ya hatari ya bitcoin: Sakoshi Nakamura anaweza/wanaweza kuiangusha fedha hii watu wakapata hasara.

Asante sana. Ila nimeanza kucheka niliposoma "Mod One , Mod Two naomba mnisaidie ku-edit title ya uzi iwe hapo kwenye Sukashi Nakamura isomeke Sukashi Nakamoto.", maana unajaribu kurekebisha jina la Nakamura live Nakamoto na unaharibu kina la Satoshi kuwa sasa Sukashi hahahahaha. Leo kweli Blue Monday.
 
Mkuu acha tu. Nimekesha nikifanya kazi flani kichwa hakipo sawa kabisa.
Thanks again.
 
Huwezi pingana na matokeo na huwezi zuia technology kwa mkono...

Wakati watanzania wanasema bitcoin na crypto ni utapeli wazungu wanaendelea kupiga mapesa, sisi tupo tu!!

Blockchain is the future nigga!!
 
Hakuna shida. Bitcoin ni sarafu decentralised na ina faida na hatari zake. Mwaka Huu mwanzoni natabiri itaanguka lakini polepole itapanda tena mpaka mwisho wa mwaka itakuwa juu sana tena. Lakini kwa sasa tunahitaji correction na common sense Katika soko la digital. Umenifurahisha kweli, leo Blue Monday.
 
Control ipo lakini kwa nia ya consensus, maana transactions na utumiaji wa bitcoin na hata mining inahitaji makubaliano ya miners na engine wenye bitcoin nyingi, Katika protokali ya Proof of Work, Proof of Stake na kadhalika. Hakuna central bank, lakini Wapo wanaocontrol kwa consensus. Wakati mwingine inakuja fork maana bitcoin inagawanya na wale miners, na Bitcoin Nyingine kama BitcoinGold etc inatokea kama sarafu. Sarafu nyingine zinafanana na Bitcoin au na Ethereum. Zile zinazofanana na Ethereum zinaweza kuwa controlled Katika Private Blockchain au la. Kwa Kweli ulimwengu wa blockchain na ya sarafu ya kidijitali si rahisi kuelewa mara moja.
 
Huwezi pingana na matokeo na huwezi zuia technology kwa mkono...

Wakati watanzania wanasema bitcoin na crypto ni utapeli wazungu wanaendelea kupiga mapesa, sisi tupo tu!!

Blockchain is the future nigga!!
Soma habari vizuri kabla hujaweka comment kama hii.

Hakuna mahali nimesema teknolojia hii utapeli.

In fact nimesema hii haizuiliki na ina faida kubwa kuliko hasara au hatari.

Isipokuwa nimetoa tahadhari tu kwamba watu wasiwekeze pesa au rasilimali zao zote kwenye hizi kitu maana ikitokea hiyo hatari au janga nililosema wasipoteze kila kitu.

Na nimeahidi kuja kuelezea zaidi faida zake na nikaweka jina la documentary inayo sifia na kulezea zaidi faida za bitcoin au crypto currency yeyote.
Tena inaonekana kitaalamu itatusaidia sana sisi nchi masikini ambako watu wengine hawana vitambuliaho na hawana akaunti za benki. Kwa kuwa na smartphone basi anaweza kufanya biashara au kupokea na kutuma fedha popote duniani na kwa kiwango chochote bila kusumbuliwa na serikali(BOT) au FIU-Financial Investigation Unit yeyote duniani. (ANGALIZO: Sikusudii kufundisha au kuhamasisha ukwepaji wa vyombo vya sheria bali natoa elimu tu. Just doing this for education purposes only)

PAMOJA NA FAIDA ZAKE ZOTE HAIONDOI UKWELI WA HATARI NILIZOSEMA.

Tafadhari rudia kusoma. Sio kila kitu unawaza ubishani wenu kama wa FOREX TRADING.
 
Ni kweli na itakuwepo angalau mpaka mwaka 2140 na bitcoin zinafaida zaidi kuliko hasara au hatari ya kufilisi watu. Lakini hii hai ondoi ukweli kwamba SATOSHI NAKAMOTO anaweza kuitingisha dunia la soko la bitcoin siku yeyote akiamua kufanya hivyo.
raha ya bitcoin ni kwamba hata huyo SATOSHI wako akiamua kiziingiza hizo bitcoin zake zitashuka thamani kwa muda tu,,,baadae zitapanda,,,na kuna watu wanasubiri zishuke thamani wazinunue...bitcoin haina uthibiti na haiwezi kufa....kumbuka cryptoccurencies ziko nyingi hao wanaoipinga bitcoin either ni washindani wao au ni nchi zinazoogopa currencies zao zitadondoshwa na bitcoin
 
Huwezi pingana na matokeo na huwezi zuia technology kwa mkono...

Wakati watanzania wanasema bitcoin na crypto ni utapeli wazungu wanaendelea kupiga mapesa, sisi tupo tu!!

Blockchain is the future nigga!!
Fanya experiment ya kuweka jina la Blockchain kwenye description ya Linkedlin yako, kwa mfano ukiandika "I am a Blockchain enthusiast".... utaona mara moja wengi sana wataanza kukuomba uwe contact Yao...
 
www.coinmarketcap.com
www.blockchaincompany.info (actually Katika website unaweza kupata Bure channel la Bloomberg, na youtube nyingi kuhusu blockchain, na crypto coins, au documentaries, Kama Blockchain Company is a utility that connects everyone through media and technology to the ecosystem of blockchain)
Pia www.blackworld.com ni tovuti nzuri sana pamoja na habari nk unaweza kupata news channels bure, na documentaries.
Blackworld - Connecting the world with Africa and global communities.
Blackworld - Business - Helping change the world through connectivity!, etc...
lakini utahitaji network nzuri na laptop au pc, si tablet au phone kwa kuangalia video au channels
 
Probably you are right on this.
But for a prudent and wise man you should reconsider all posibilities from both sides, bad and good.

Mimi nahamasisha watu watumie lakini wasiwekeze akiba yao yote.

Mkuu wewe kama una umri mkubwa unakumbuka Y2K. Unaijua ilikuwa ndio nini?

Kwanini wajuzi wa technolojia hawa ku-renconsider ile problem wakati wana design?

Usimuwekee sana dhamana programmer anaweka backdoor ya kuja kuku-force uingie gharama tena.

Kama unafikiri vizuri jiulize maswali kwanini mgunduzi wa hizo crypto currency ameficha utambulisho wake?

Ukweli ulio wazi amegundua kitu muhimu sana na cha lazima kwa dunia ya sasa. Narudia tena hii haiondoi hatari zinazowezekana watu kupoteza fedha au kufilisika kabisa.
 
mkuu technologia yoyote mpya inapoingia inaleta mashaka fulani mku mpaka pale itakaposettle ndio watu wanaondoa mashaka......dunia sasa hivi inaelekea huko mkuu pesa ya cash ndio inaelekea kupotea hivyo inayokuja ndio hiyo crypo....!...huyo Satoshi anajulikana sema wameamua kumuweka invisible kwa sababu maalum.....hii bitcoin imeshakubalika worldwide ni ngumu sana kufa.....believe me kama US na CHINA wameikubali haitakufa kamwe!
 
Ukweli ulio wazi amegundua kitu muhimu sana na cha lazima kwa dunia ya sasa. Narudia tena hii haiondoi hatari zinazowezekana watu kupoteza fedha au kufilisika kabisa.
Hamna kisichokua na hatari mkuu, ukisema ukiinvest kwenye bitcoin ni hatari je wale ambao pesa zao zimepotea baada ya benk kufutiwa usajili unawaseaje?
 
Ila ripple anajulkana na yupo verified,tatizo bitcoin owner/satosh.

Crypto ni nzur SANAAAAAAA,kwa coin nyengne mbali na BTC
 
Ila ripple anajulkana na yupo verified,tatizo bitcoin owner/satosh.

Crypto ni nzur SANAAAAAAA,kwa coin nyengne mbali na BTC
Ripple si crypto ya kweli kama Bitcoin, ila ni kama token, ipo controlled na kampuni binafsi na inatumika kwa sababu maalum na kwa Kazi maalum, na si kama pesa kama bitcoin. Hata hivi investment si mbaya Ripple. Ripple iPo ndani ya Private Blockchains. Coins nyingi pia zitapotea baada ya muda kwa sababu hazina maana sana. Bitcoin itaendelea sana lakini.
 
Ni kweli mkuu.
 
Hamna kisichokua na hatari mkuu, ukisema ukiinvest kwenye bitcoin ni hatari je wale ambao pesa zao zimepotea baada ya benk kufutiwa usajili unawaseaje?
Usipotoshe kwamba fedha zimeenda moja kwa moja.
kuna utaratibu wa kuwarudiashia ingawa wenye fedha nyingi mlolongo ni mrefu na unaweza usipate zote.

Mbaya kama ile ilitokea Cyprus au Ugiriki.
 
Wewe ndio unapotosha, risk ziko kila sehemu na ukiona investment ambayo haina risk jua haina faida!
Mkuu hadi tukuwekee tangazo la serikali kuhusu benki zilizofungiwa au unapenda mabishano yasiyo ya kitaalamu kam ya vijiweni?

Hujaona pale watu walivyoelekezwa namna watakavyorejeshewa pesa zao ktk makundi mawili huku wewe unasema bank za kawaida ikifilisika unapoteza kila kitu.
Kama ni hivyo mimi najitoa hayo mabishano naona hayana uhalisia wala faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…