Siri iliyojificha kwenye Nafaka...

Fuqin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2018
Posts
306
Reaction score
625
Wadau nadhani mupo powa kabisa... mimi ni mdau wa biashara ya nafaka na leo nataka kushare nanyi kitu katika biashara ya nafaka ambapo hata nyinyi munaweza kufanya na mukapata pesa nzuri tuu, ni hivii...

Wakati biashara zinaenda kama kawaida kipindi cha mavuno bei huwa zinashuka sana mfano kunde waweza nunua sh. 800 kama una milioni 8 unapata tani 10... ukatafuta sehem ukaihifadhi ukapiga na dawa baada ya miezi 6 utakuja kuiuza kwa sh. 1500 mara tani 10 zako inapata milioni 15 ukitoa milioni zako 8 inabaki m 7 kama faida.... hii kitu hata mimi huwa nafanya na ndio kazi yangu na huku nina duka nauza kila siku bidhaa kwahyo napiga huku na huku
 
wadau nadhani mupo powa kabisa... mimi ni mdau wa biashara ya nafaka na leo nataka kushare nanyi kitu katika biashara ya nafaka ambapo hata nyinyi munaweza kufanya na mukapata pesa nzuri tuu, ni hivii... wakati biashara zinaenda kama
Hii ni idea nzuri Sana! hongera kwa kutokuwa mchoyo wa idea za kutoboa kama hizi. Ila kwa nyongeza sio lazima nafaka ukaipiga dawa ya kuhifadhia, tafuta viroba vile Maalum vya kuhifadhia vinaitwa kinga njaa kausha vzr nafaka zako kisha hifadhi humo, hakikisha unamdhibiti panya! humo hakuna mdudu mwaribifu ambae atadumu.
 
Naomba ufungue tawi huku nilipo niwe wakala wa biashara zako mkuu
 
Hiyo mifuko inauzwa bei kubwa ndugu ila cha musingi ni kununua mifuko ya kawaida na unatunza mazao yako vizuri ila lazima uwe na nyumba malumu ambayo hata kaa mtu unaweka dawa Fulani hivi ya vidonge inauzwa kwenye maduka yakilimo ni sumu panya hagusi humo akiingia anakufa na kukauka kabisa.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Japo ni kweli lakini sio rahisi kiasi hicho, zali nalo linatakiwa, mfano kwenye mpunga na mahindi watu wameumia sana kwenye miaka ya 2017-2021, ulikuwa ukinunua hata msimu wa mavuno, hadi mwezi wa tano tena, mavuno mpya yanaingia unakuta yameongezeka 10, 000 tu kwa gunia, kidogo mahindi kama 2019, ndio zali liliwadondokea.biashara ya mazao inahitaji sana bahati, na machale sana hasa hiyo ya kununua na kuweka store.
 
Mbona haujataja gharama ya usafirishaji, kulipia ghala, dawa ya wadudu, gunia za kuhifadhia, wapakizaji, ushuru, misururu ya vibali na gharama binafsi kama kula na malazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…