GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Habari iliyonifikia hivi punde kutoka katika chanzo changu kikubwa kabisa na ninachokiamini ndani ya Klabu ya Yanga kimenitaarifu kwamba kuna taarifa ambayo Wadau wa Michezo tunafichwa ila ukweli ni kwamba baada ya mechi ya Kirafiki ya juzi ya Yanga SC na Rhino FC katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Mkoani Tabora kulitokea ' Ngumi ' baina ya Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ' Cannavaro ' na Beki wa Kulia Ramadhan Kessy.
Sababu Kuu iliyopelekea kuwa na mpambano huo wa Ndondi usio rasmi na usio na mkanda ni pale ambapo Nahodha Cannavaro alipoamua kugawa ' Posho ' kwa Wenzie kwa kadri alivyokuwa akipanga Yeye hali ambayo iliondoa uvumilivu wa Beki Kessy ambaye aliamka na kutaka ajue kimepatikana Kiasi gani ndipo baada ya kutopata maelezo ya kutosha kutoka kwa Nahodha wake akaamua kumnyang'anya zile Hela ndipo Nahodha Cannavaro alipoamua nae kujibu mapigo wakapelekea ' Kudundana '.
Mara baada ya kutokea ' tafrani ' hiyo Viongozi wa Yanga FC na ' Benchi ' zima la Ufundi liliamua kulifanya hili Siri kubwa ili Mwandishi wa Habari yoyote asiijue lakini kumbe hapo hapo wakasahau kwamba GENTAMYCINE popote pale nina ' Vyanzo ' vyangu ambavyo huwa havinifichi kitu na hatimaye leo ' nimepenyezewa ' hii.
Aidha chanzo changu hicho Kikubwa kilichopo ndani ya Klabu ya Yanga kimeniambia kwamba kwa sasa hali ya Kiuchumi / Kipesa ndani ya Timu ni mbaya sana na kwamba Wachezaji wamekosa ' morale ' na wamesikitishwa mno na taarifa wanazozisikia kutoka katika Vyombo vya Habari mbalimbali kwamba aliyekuwa Mfadhili wao Manji amerudi wakati siyo kweli na kwamba Uendeshaji wote wa Timu kwa sasa unatokana na Timu Kukopa Pesa kutoka kwa Makampuni na watakatana taratibu na kwamba si kweli kwamba Yusuph Manji amerudi Yanga rasmi.
Haya sasa nimeleta hii taarifa huku nikimsubiri kwa hamu sana Msemaji wa Yanga FC Dismass Ten aikanushe kisha niweke ' hadharani ' bomu lingine ambalo linakaribia kupasuka ndani ya Yanga na ambalo naamini Wanachama wake wakilisikia sasa hivi hapo Kaunda Jangwani ' bakora ' zitaanza kutembea na ' Kitanuka '. Hakuna kinachoendelea au kitakachoendelea ndani ya Yanga GENTAMYCINE nisijue au nisikipate hivyo wana Yanga SC popote pale mlipo acheni kuwa na viherere na kuwashwawashwa mno na masuala ya Simba SC wakati nyie ya kwenu ni mengi na yanawashindeni.
Nawasilisha.