Siri katika uuzwaji wa data za whatsapp, Twitter na mitandao mingine

Dra Maxie

Senior Member
Joined
Dec 9, 2022
Posts
143
Reaction score
216
Habari zenu,
Jamani mimi ningependa kuuliza tu. Hivi wanaposema account zimedukuliwa na data za watumiaji zimeuzwa. Wanamaanisha nini?

Data gani? Wanauza wapi?

Wanaowauzia wanazitumia vipi?

Nakumbuka niliwahi angalia muvi fulani ya kizungu ilikuwa inahusisha kudukua account za watu sasa pia sikuelewa niliachwa njia panda.

Naomba leo mnieleweshe
 
Wao wananufaikaje?
Mfano ni rahisi mm naifuata facebook nakuweka dau ili ninunue data yako baada ya hapo ninaweza kutumia data hiyo kujua unafanya nini hasa unapokuwa mtandaoni kisha kuanza kukuletea matangazo kutokana na nn hufanya sana?.
 
Data ndio msingi WA Artificial Intelligence, kampuni yenye data nyingi za watu inapata uwezo mkubwa WA kuunda algorithms nzuri za AI.

Artificial Intelligence inaweza tumika maeneo mengi, mfano.
1. Ads targeting
2. Autonomous vehicles
3. Autonomous weapons
4. Precision Farming.
5. Facial recognition nk nk

Mfumo wenye AI unaleta urahisi WA kukuekea contents unazopendelea na matangazo yanayoendana na unachokipenda (upande WA mitandao ya kijamii na search engine).

Ndio maana ukiingia YouTube au Instagram unakutana na maudhui ambayo unayoyapenda Kwa asilimia kubwa.

Hii inatokana na ukusanyaji WA data zako na watu wengine kila unapoingia kitu kinachofanya kuwa rahisi kutabiri unachotaka kukitazama.

Kwa mfano, JamiiForums ina post zaidi ya milioni 40, hii idadi ya post inaweza ikaifanya jf kutengeneza speech recognition na natural language processing ya Kiswahili, na hata pia wanaweza unda automoderators zitakazotambua huyu mtu anastahili ban au la bila uwepo WA moderator binadamu na mambo mengine mengi.

Ndio maana USA anapinga vikali 5g kuundwa na kampuni za kichina.
 
USA ni wapuuzi tu wanataka wao ndiyo wawe wana tumia hiyo technology pekee yao
 
Back
Top Bottom