Data ndio msingi WA Artificial Intelligence, kampuni yenye data nyingi za watu inapata uwezo mkubwa WA kuunda algorithms nzuri za AI.
Artificial Intelligence inaweza tumika maeneo mengi, mfano.
1. Ads targeting
2. Autonomous vehicles
3. Autonomous weapons
4. Precision Farming.
5. Facial recognition nk nk
Mfumo wenye AI unaleta urahisi WA kukuekea contents unazopendelea na matangazo yanayoendana na unachokipenda (upande WA mitandao ya kijamii na search engine).
Ndio maana ukiingia YouTube au Instagram unakutana na maudhui ambayo unayoyapenda Kwa asilimia kubwa.
Hii inatokana na ukusanyaji WA data zako na watu wengine kila unapoingia kitu kinachofanya kuwa rahisi kutabiri unachotaka kukitazama.
Kwa mfano,
JamiiForums ina post zaidi ya milioni 40, hii idadi ya post inaweza ikaifanya jf kutengeneza speech recognition na natural language processing ya Kiswahili, na hata pia wanaweza unda automoderators zitakazotambua huyu mtu anastahili ban au la bila uwepo WA moderator binadamu na mambo mengine mengi.
Ndio maana USA anapinga vikali 5g kuundwa na kampuni za kichina.