Siri kubwa ya maisha nakupa wewe leo

BABA BOMBASTIC

Senior Member
Joined
Jul 10, 2024
Posts
146
Reaction score
246
Habari zenu wapendwa wa bwana.
Nimatumaini yangu wewe ni mzima wa afya,tupate mda wa kuwaombe wagonjwa na wenye shida mbalimbali,MUNGU awatangulie amen. Moja kwa moja twende kwenye mada huska niliyoiandika hapo juu.

Nimekuwa nikifanya uchunguzi wangu kwa mda mrefu sana na nimegundua hii siri kubwa sana ambayo wengine tumekuwa tukiipuuzia mashuleni pia mtaani.

Shuleni tumepewa hii elimu lakini wengi wetu tumeidharau sana COMMUNICATION SKILLS. Aisee hii ni bonge la elimu ukilitumia vyema maishani mwako itakuwa mteremko.

Kila kitu hapa duniani kimeshikiliwa na watu,makazini,mashuleni n.k kila sehemu utakapoenda utakuta kuna mtu ana hold kitu au position fulani,sasa kinachotakiwa wewe kufanya jifunze jinsi ya kucommunicate na watu vyema,hii inaingia kwenye shughuli mbalimbali iwe officine kwako mpaka kwa watu walioajiriwa jifunze jinsi ya kuteka watu kimaongezi.

Wabongo wengi hawachomoki kwa mtu anayejua kuzungumza vyema,hii nimefanya kwenye office yangu aisee sasa hivi nina wateja wengi mpaka wengine nawapangia siku za kuja officine,mara ya kwanza nilikuwa nina bad customer care nilikuwa sijali wateja,nawakaripia,siwasalimii,mda wote nimenuna,kwa kifupi sina mda na wateja nikisha muhudumia kapita hivi.

Baada ya kukaa chini nakusoma vitabu mbalimbali juu ya communication skills nikajifunza mambo mbalimbali. Mambo niliyojifunza jinzi ya kwenda sawa na watu wenye tabia mbalimbali,kuna watu wenye hasira na wapole,kuna wateja wababe na wapole,sasa nikajua jinsi ya kwenda nao sawa.

Mteja anaweza kuja dukani kwako kununua bidhaa ,akiwa na hasira sasa unatakiwa ujue jinsi ya kuondoa hizo hasira zake na kuondoka akiwa anacheka,hii nimeifanyia kazi dukani kwangu ukiingia kuna vicheko vya wateja,na kwa uchangamfu wangu wanajikuta wananunua vitu vingine hawakuvipanga akilini mwao hiyo yote ni ucheshi.

Pia nikajifunza utani mbalimbali,kwa mteja wa kiume kuna utani wake na wakikee kuna utani wakiume,mimi simuonii mteja aibu ata aweje.

Jifunze kuteka watu kiakili kuhusu mdomo wako,mwenyenzi MUNGU alitupa huu mdomo tuutumie vyema sio kutukana wengine na maneno mabaya juu ya wenzentu,hujawahi kuona kuna wachezaji hapa duniani wanakiwango cha kawaida sana ila fedha wanazolipwa ni kubwa sana kulingana na kiwango chao,wanajua kubargaini vyema juu ya mikataba yao.

Unaweza ukafanya kazi kubwa sana ambayo kipato chake kikubwa mnoo ila kwakuwa ujui kuongea vyema ukalipwa ujira mdogo,ebu waangalie wakina mwijaku,dotto magari,baba levo,perer msechu na wengine wengi hao wote wanatumia midomo yao kupata kipato.

Haijalishi mpoje kimuonekano,ila kama utautumia mdomo wako vyema kwenye hii dunia aisee utakuwa mtu wa tofauti sana kimaendeleo dhidi ya wengine,au hujawahi kujiuliza washikaji wenye maisha ya kawaida wanachukua mademu wa kali mtaani wenye pesa zao??hiyo yote ni midomo yao basi leo hii nenda katafute kitabu cha communication skills.

Soma Pia: Maisha ni safari kadri unavyosimama sana ndivyo unavyojiongezea kuchelewa kufika

Chochote unachokitafuta hapa duniani kimeshikiliwana watu sasa ni kazi yako kujua jinsi ya kukichukua kwake.

Pesa zipo mikononi mwa watu.
Kazi zipo mikononi mwa watu.
Hiii siri wanajua wachache sana,nakupa wewe leo ili uwe miongoni mwao.

.............ALUTA CONTINUA.............
.............BABA BOMBASTIC....

.
 
Umeanza vizuri ulipowaingiza kina Mwijaku thread yako imepoteza maana ni upuuzi mtupu.
 
Umeanza vizuri ulipowaingiza kina Mwijaku thread yako imepoteza maana ni upuuzi mtupu.
Fanya yako niliwaingiza hao kama mfano,sasa weweunaona kero basi wewe umefanya nini duniani nikufanye mfano??au unachokijua ni wivu tu acha nitoe credit pasuka kama unapasuka is up to you matola the farmer
 
Kuna wateja wanakeraa...anashika mali yako unayouzaa mfano,kiatu anakwambia hichi kiatu gani cha kuuza 15000,nikikupa sana elfu sabaa,uwaga nawambia siuzi.wewe umenunua 8000,anaanza kutoa kasoro kama zote.bro hii bali sijapewa bure au kuiba,kama bei ufiki nenda duka jingine.mteja asije na bei kichwani kwamba lazima ninunue kwa bei hii
 
Ila Jeifu banaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ ....mtoa mada kashikwa na kauli chafu kabla mada haijaenda viral πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…