KakindoMaster
JF-Expert Member
- Dec 5, 2006
- 1,356
- 88
uchumi wetu unashuka haupai tena, inlation rate imefikia 9% soma east african, shilingi ya kenya leo ilikuwa tshs 22 hapa moshi mjin. huyo gavana anaota ndoto za lowasa za ndege ya uchumi inayopaa. tusiwalaumu bure wananchi wanaoowapokea mafusadi huko vijini, mafisadi wananunua wananchi kwa cash na materials, mapokezi ya chenge tunaambiw akuwa ametumia angalua vijisenti kama 234m! we must address two issues in parallel, ufisadi na umaskini wa wananchi wetu, tukiweza kupambanakuushinda ufisadi na hali ya uchumi ikiimarika, wananchi wataweza sasa kuwa huru, hata wakishiriki uchaguzi watashiriki kwa utashi wao na wala si kwa njaa zao
Kweli inasikitisha jinsi kiongozi wa dini wa wadhifa wa Askofu (Laizer) alivyokubali kuwa mshirika katika hekaheka za kisiasa. Alipaswa kusoma upepo kwanza ili kujua kondoo wake wengi wako upande gani, upande wa MAFISADI au upande wa UZALENDO wa kupambana na kuukemea ufisadi. Kwa elimu na upeo wake alipaswa kujua kuwa kondoo wake wako upande wa UZALENDO. Tatizo anasumbuliwa na NJAA ya pesa bila jasho (kamanyola)!!!! Mwenyezi Mungu uibariki Tanzania na ushushe miujiza yako MAFISADI wazidi kuumbuka mchana kweupe. Twasubiri bunge la BAJETI ambapo yai la EPA litanguliwa na mafisadi wataumbuka na kuaabika zaidi!! Amen!!!
Kuna haja ya kuanzisha usalama wa taifa wenye nia halisi ya kulinda masilahi ya taifa la sivyo kuna vita kubwa inakuja tanzania kati ya wanatanzania wenye uchungu na mafisadi hawa wasio na haya hata kidogo.