The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
1. Malumbano kati ya Waziri wa fedha na Kamishina wa Mapato TRA.
Msimamo wa Kamishina kuhusu kero za wafanyabiashara ni kutekeleza sheria wala siyo maagizo ya wanasiasa wa ngazi yoyote.
Kamishina TRA amewaambia Wafanyabiashara mara kadhaa mkitaka tuache kufanya kazi ambazo nyie (Wafanyabiashara) mnaziita kero
Ongeeni na wanasiasa waondoe hizo sheria au wafanyie marekebisho hizo sheria,
Sisi tutatekeleza hiyo sheria,kama hawaondoi malalamiko yenu katika hizi sheria,sisi tunalazimika kutekeleza Sheria iliyopo tuh.
Wakati huo Waziri wa fedha mwenye dhamana na Sheria zote za fedha, hajawahi kupeleka mswaada mpya wala marekebisho ya sheria kwa mwaka wa pili sasa.
Ndiyo maana Wafanyabiashara wanajua maagizo ya kisiasa ya Waziri Mkuu au Waziri Kitila Mkumbo hayana nafasi mbele ya TRA.
2.Kukamatwa kwa Mfanyabiashara maarufu na mwenye ushawishi Kariakoo Bwana Erasto Rweimamu na Mwenyekiti wa Kijiwe cha "RAHA SQUARE" pale Kariakoo
Siku ya Jumapili ya 22 June 2024 ,Viongozi wa Wafanyabiashara Kariakoo, Walimuomba Mfanyabiashara maarufu na Mwenye ushawishi Kariakoo awasindikize Dodoma na akashiriki Kikao kilichoitishwa na Waziri wa fedha,Waziri wa Viwanda na biashara na Waziri wa Mipango siku ya Jumatatu ya tarehe 23 June 2024.
Lakini cha Kusikitisha Bwana Erasto Rweimamu akiwa njiani katika gari pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (kenedy Mast na Mbilinyi ambaye katibu wa wajumuiya)
Alikamatwa akiwa safarini Kuelekea Dodoma katika kikao alicho alikwa na Mawaziri kupitia Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo.
Jambo baya kabisa,Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo walioomba kwenda naye na na kumchukua akashiriki kikao Dodoma
Walishuhudia mwenzao akikamatwa,lakini walinyamaza Kimya bila kujulisha Wafanyabiashara wenzao Dar es saalam wala familia ya Bwana Erasto Rweimamu.
Baada ya Kikao cha Jana, baina ya Serikali na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, pamoja na serikali kutoa tamko la Kusitisha Operesheni za Kukamata Wafanyabiashara wasiotumia EFD Mashine Kariakoo
Wafanyabiashara kariakoo walikuwa wanasubiri tamko au maoni ya Bwana Erasto Rweimamu kuhusu makubaliano hayo,
wakijua ameshiriki kikao na Mawaziri kama alivyo aga Dar es saalam siku anaanza safari ya kwenda Dodoma.
Lakini wafanyabishara kariakoo walianza kupatwa na wasiwasi baada ya kuona simu za Bwana Erasto Rweimamu hazipatikani
Na Viongozi wakiulizwa Erasto Rweimamu yupo wapi hakuna majibu ya maana wanayotoa.
Kwa jambo hili la Kijinga ,Jana usiku Wafanyabiashara kariakoo waliazimia kuendelea na mgomo baada ya kuona serikali haina nia ya dhati ya kumaliza matatizo yao.
Hata hivyo baada ya Wafanyabiashara wa Kariakoo kupambana kumtafuta ndugu yao Erasto Rweimamu
Leo wamepata taarifa rasmi anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es saalam tangu siku ya Jumapili.
Akili ya kumkamata na kumshikilia Bwana Erasto Rweimamu wakati wakutaka kumaliza mgogoro na Wafanyabiashara imetafsiriwa kama serikali kupijipiga risasi katika mguu wake au kujihujumu yenyewe.
Mambo haya mawili yamekoleza zaidi mgomo wa wafanyabiashara na kusasabisha kuanza kuenea katika Majiji ya Mwanza na Mbeya.
Wafanyabiashara wamesikika wakisema wao siyo wajinga, kama kero za amezishindwa Waziri Mkuu kuzitatua iweje aweze Waziri wa Kawaida kama Kitila Mkumbo tena kwa kutoa ahadi.