Siri ya kasi ya mbegu za kiume yagunduliwa!

Siri ya kasi ya mbegu za kiume yagunduliwa!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363






Wataalamu wanasema wamegundua kwamba mbegu za kiume huanza kwenda kwa kasi wakati zinapofika karibu na yai la mwanamke, suala ambalo huenda siku zijazo likasaidia katika kupatikana dawa ya kuzuia mimba ya wanaume. Vitundu vidogo vilivyoko juu ya mbegu

hizo za kiume huziwezesha kubadilisha PH yake ya ndani, ambayo hufanya mkia wa mbegu hizo uanze harakati. Wataalamu hao wa Chuo Kikuu cha California huko San Francisco wanasema kuwa, ugunduzi huo unaweza pia kusaidia kuelezea kwa nini marijuana huwafanya wanaume wawe tasa na kwamba suala hilo litaleta mabadiliko makubwa katika kufahau suala zima la uwezo wa kuzaa wa mwanaume.

Kwa kawaida mbegu za wanaume hazianzi kwenda mbio baada tu ya kumwagwa, na ili kuweza kulifikia yai la mwanamke huhitajia kujiepusha na kasi hadi pale zinapokaribia yai. Wanasayansi kwa muda mrefu wamekuwa wakifahamu kwamba mwendo wa mbegu za

kiume umekuwa ukisimamiwa na PH ya ndani, na kuwa kwake katika hali ya asidi au alikali lakini walikuwa hawafahamu ni jambo gani hasa linalowezesha kubadilika PH hiyo. Wataalamu wamesema, sasa wamejua kuwa ili kuongeza PH ili iwe ya alkali, mbegu huhitajia protoni

zinaoitwa Jettison, na kwamba wamegundua vijitundu vidogo vilivyoko juu ya mbegu hizo ndio huruhusu mabadiliko hayo. Daktari Yuriy Kirichok aliyeongoza utafiti huo anasema, iwapo utafungua vijitundu hivyo, protoni inatoka nje, na wao wamefahamu molekuli ambazo

huruhusu protoni hizo zitoke nje. Anaendelea kueleza kwamba, vijitundu hivyo vilivyopewa jina la Hv1 proton Channels, hufunguka pale inapofikia wakati muafaka wa kufunguka na hutegemea kitu kingine kinachoitwa, anandamine. Anandamide ziko katika mirija ya uzazi ya mwanamke katika eneo ambalo ni karibu na yai.

Katika marijuana kuna mada inaitwa cannabidoid ambayo inaaminika kuwa inapunguza uwezo wa anandamide, suala ambalo sasa limeweza kuelezea ni kwa nini marijuana kusababisha ugumba kwa wanaume. Dk, Kirichok anasema kwamba, marijuana pia huzipa kasi

mbegu za kiume mapema, na huzifanya ziungue baada ya masa kadhaa. Watafiti hao wanatupa moyo kwamba, kwa kufahamu vyema masuala hayo, sasa ni wazi kuwa wanaweza kutafuta dawa ya kuzuia mimba kwa wanaume. Kwani kwa kuziziba molekuli hizo, pengine wakafanikiwa kuzuia na kutoruhusu mbegu isikutane na yai, na njia hiyo ikatumika kama dawa ya kuzuia mimba kwa wanaume.
Mashosti: Siri ya kasi ya mbegu za kiume yagunduliwa!
 
haya mzizi mkavu hii itakuwa janga kama vidhibiti mimba kwa wanawake vinaleta balaa je, hii nayo haitakuwa danganya toto kutupunguzia nguvu kwa waafrica ili tusizaliane?
 
Unachosema mkuu ni kweli kabisa. Side effects za madawa hayo zitafichwa kisha baada ya miaka mitano ndio zitaanza kujionyesha miongoni mwa watumiaji. Kwa wanaume hasa wa Kiafrika kutumia dawa hizi itakuwa ni vigumu sana.

haya mzizi mkavu hii itakuwa janga kama vidhibiti mimba kwa wanawake vinaleta balaa je, hii nayo haitakuwa danganya toto kutupunguzia nguvu kwa waafrica ili tusizaliane?
 
kwa suala la bangi na ugumba mmmh! Sina verification ila mbona bob marley alikuwa na timu nzima ya mpira wa miguu?
 
Back
Top Bottom