Siri ya Kuacha kazi na mafanikio ya mtu, hii imekaaje wakuu?

Rozela

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2024
Posts
845
Reaction score
2,235
Baada ya mahojiano ya watumishi wa Umma 83 wa kada za ualimu, uuguzi, ,aafisa kilimo na watendaji wa kata tumebaini kitu fulani ambacho kimetushangaza kidogo.

Hao 83 ni wale ambao wamefanikiwa sana katika biashara japo ni watumishi wa umma tuliwapata kama sampuli katika mikoa 15 ya Tanzania bara. (Tunajua wako watumishi wengi zaidi wenye mafanikio makubwa ambao hatuku wahoji)

Biashara wanazofanya hawa 83 ni
1. Ufugaji wa kisasa, hapa nazungumzia ufugaji sio majaribio ya ufugaji.
2. Mashamba makubwa na mitambo ya kilimo na kuchakata mazao.
3. Nyumba za kulala wageni zenye hadhi mbalimbali na restaurants.
5. Biashara ya maduka ya vifaa vya ujenzi.
6. Maduka makubwa ya vinywaji na vyakula.
7. Vituo vya afya na maduka ya dawa.

Kati ya 83 tulio wahoji, 22 waliwahi kuacha kazi zao serikalini kwa miaka kadhaa kisha wakarudi (zamani inaelekea hili lilikuwa jambo rahisi) na walipo rudi hawakushikika kimaendeleo.

Je, kuna uhusiano gani kati ya kuacha kazi na kufanikiwa mara baada ya kurudi kazini? Hawa 83 ni kwamba tulikuwa tunatafuta success story zao tukabaini 22 kati yao waliwahi kuacha kazi na kurudi tena.

Je, walipotoka nje ya mfumo waliona nini ambacho kiliwarudisha kwenye mfumo? Au ndiyo wale watu wa mfumo ambao hupaswi kuwaiga? Wao wanadai walirudi sababu ya changamoto za maisha ila kwanini waliporudi walifanikiwa sana?
 
Sijaelewa bado?!!!

Kwa nini hukuwauliza wao ukaamua kubaki na kushangaa kwako?
 
Ungetuambia why waliamua kurudi kazini in first place
 
Sijaelewa bado?!!!

Kwa nini hukuwauliza wao ukaamua kubaki na kushangaa kwako?
Wengi wao wanadai maisha ndio yaliwarudisha sasa kwanini walivyorudi walifanikiwa kuliko walio waacha?
 
Kuajiriwa nikwasababu ya kukosa mtaji wa kuaminika.
Ukiwa na mtaji ondoka kwenye mnyororo wa utumwa
 
Kwenye maisha kama hakuna formula ya kufanikiwa na wengi wetu tutakufa tu tukiwa hatujafanya chochote cha maana 🐼
 
Kwenye maisha kama hakuna formula ya kufanikiwa na wengi wetu tutakufa tu tukiwa hatujafanya chochote cha maana 🐼
Hahahaa, maneno yanaumba mkuu, futa kauli yako. Sema mimi ni tajiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…