SiRI YA KUDUMU KWA NDOA

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,412
Wanaume Wanaowasaidia Wake Zao Kazi za Nyumbani Ndoa Zao Hudumu

Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wanaowasaidia wake zao kazi za nyumbani ndoa zao hudumu Friday, May 21, 2010 2:52 AM
Wanaume ambao huwasaidia wake zao kazi mbalimbali za nyumbani kama vile kupika, kuosha vyombo na kuwaogesha watoto, ndoa zao hudumu muda mrefu kulinganisha na wale wanaosubiria kufanyiwa kila kitu na wake zao. Utafiti uliofanywa na watafiti wa chuo cha London School of Economics (LSE) cha Uingereza umeonyesha kuwa wanaume wanaowasaidia wake zao kazi za nyumbani ndoa zao hudumu muda mrefu kulinganisha na wanaume ambao hawependi kuwasaidia kazi za nyumbani wake zao.

Utafiti huo ulisema kuwa ndoa ambazo mke na mume wote wanafanya kazi huwa katika hatari kubwa ya kuvunjika iwapo mume hamsaidii mkewe kazi za nyumbani.

Utafiti huo uliopewa jina la "Men's Unpaid Work and Divorce" ulihusisha familia 3500 za Uingereza.

Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa wanaume ambao waliwasaidia wake zao kazi za nyumbani kama vile kwenda sokoni, kuosha vyombo, kupika na kuwaangalia watoto ndoa zao zilionyesha kuwa imara zaidi.

Hata hivyo utafiti huo ulisema kuwa ndoa za watu wa zamani zilidumu sana kwa kuwa mke alikuwa hafanyi kazi akijishughulisha na kazi za nyumbani pekee wakati mume alifanya kazi kutafuta chakula kwaajili ya familia.
 
1.huo ni utafiti wa uk. Je africa au tz?
2.ili ndoa idumu mwanamke anahitaji mambo mengine muhimu sana, zaidi ya kumsaidia kukuna nazi.
3.upendo,kuvumiliana,kusameheana,kutoshelezana,kuheshimiana,kuthaminiana,kutunzana ni muhimu.
4.utasugua misufuria weeeee,ila kimoja tu kati ya hivyo vya hapo juu no 3 kikikosa ndoa itavunjika tu.
 
Jamani reseachers hebu ingieni sehemu kama Tandale ; Magomeni na Sinza hapa bongo; studies za ughaibuni na maisha yetu wapi na wapi?; Njooni mtuambie kwanini Juma anamrukia Asha wa chumba cha pili ilihali Mwanahamisi mkewe ni mzuri tu na amejaaliwa kila kitu kiasi kwa Abdalah muuza duka anammezea mate ya uchu!
 
Msi copy na kupaste mambo ya ulaya jamani ni tofauti na Africa kwa ujumla. though inapaswa umsaidie ubavu wako!!!!!!
 
That is european reference and it may not apply in africa
 
Bonge la utafiti ila kuna kitu kinahitaji critical analysis, exactly comparative, kati ya ndoa za zamani na za sasa
 
Ulaya ulaya na Afrika ni Aafrika it may not be applicable kwetu kwa kweli!
To us ni zaidi ya kumsaidia mkeo kazi za nyumbani
 
we ijaribu kwa wanawake wa tanzania ukimaliza ndo utoe majibu ya reseach yako unacheza na wanawake wa bongo eeh
 
ya riyt na huo utafiti tena inaleta mashamsham kidogo kwenye mambo yetu kwa wale wana ndoa wenzangu
 
ya riyt na huo utafiti tena inaleta mashamsham kidogo kwenye mambo yetu kwa wale wana ndoa wenzangu

Dah! imekula kwangu. Kumbe ushaolewa tayari? Haidhuru, mpe pole mumeo kama kweli anakusaidia kupika.
 
huku bongo akija mamkwe au wifi amkute mr jikoni si ndo maneno yataanza or kamlisha limbwata, na akija shoga akamkuta shem wake anaosha sufuria ndo ofc nzima watajua! ila inapendeza sana pale mzee mzima anapoamua kuingia jikoni au hata kumchange mtoto tu mwanamke unajisikia ati!
 
tafiti nyingi za ndoa mi naziona nadharia tu!

unaweza kusaidia hadi kumsuka mama, halafu bado akakwambia hata mechi ya liverpool usiangalie! na bado akakutosa kwamba huna mvuto au challenge; the issue of marriage is compliacted and there is no "one size fits all solution".

i think it doesn't matter what you, there are three basic ingredients;

  • Love
  • trust
  • security [this is both ways kuanzia financial, security, information, privacy and dedication
unaweza ukakata vitunguu hadi machozi ya damu yatoke lakini kama ni punga na mkeo anajua, basi mambo yako hayatakaa vizuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…