SoC02 Siri ya kukua kwa uchumi nyuma ya mabadiliko ya teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition

pac dady

New Member
Joined
Sep 11, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Katika nakala hii nta jaribu kuelezea nini siri kubwa ya kiuchumi iliyo jificha nyuma ya mabadiriko ya mifumo ya kiutendaji kazi yaani teknolojia. Dunia yetu ya leo ime kua na mabadailiko makubwa sana katika teknolojia na mabadiriko haya huathiri nyanja mbalimbali kama kiuchumi,kijamii na hata kisiasa ila binafsi ntajikita zaidi katika nyanja ya kiuchumi, kabla hatuja fika mbali nivema tujiulize swali kwanini mabadiriko haya yana watajilisha wachache? Au mataifa machache?

Kwanini wengine hatunufaiki? Kwa mtazamo wa haraka unaweza jipa jibu kama wasomi ndio wana nufaika, au mataifa makubwa ndio wana nufaika lakini kupata ukweli wa jambo hili nilazima watu tuelewe sifa na tabia za mabadiriko yoyote ya ki teknolojia.

Kuweka wazi sifa hizo ntapenda kutumia mifumo kadha ambayo kugundulika kwake kuliathiri nyanja nyingi kwa kuanza na ugunduzi wa magurudumu (matairi)huu nimoja kati ya mifumo ya muhimu iliyo wai kugunduliwa miaka mingi iliyo pita na jamii ya watu wa mesopotamia ambayo kugunduliwa kwake kulileta fulsa nyingi sana kwa jami kwani ili saidia katika shughuri za kilimo cha kisasa, ili hitaji wataalam wa kutumia mfumo huu, kuboresha na wa kutengeneza pia ilichangia kwa kiasi kikubwa kwenye usafirishaji hizo ni baadhi ya fulsa zilizo anzishwa kutokana na mfumo huo mfumo mwingine ni wa ugunduzi wa magari ambao ulifanyika na mjerumani karl benzi mwaka 1886

Pia ugunduzi wa magari ulikuja na fulsa nyingi sanaa kama vile uliongeza matumizi ya vyuma kuna wale watu walijikita na uzalishaji wa vyuma,uli hitaji matumizi ya mafuta kuna wale walo jikita kwenye kuzalisha mafuta au nishati mfumo ulihitaji maboresho mengi ndio mana kuna wale watu waliwekeza nguvu zao katika kugundua dosari zilizopo na kugundua vitu mbalimbali ili kuboresha mfumo huo basi kupitia mifumo hio michache tunaeza kugundua sifa na tabia za teknolojia mpya sifa ya kwanza ni mifumo mingi inayo gunduliwa huja haija kamilika ina hitaji maboresho na wataalamu japo sio rahisi kuona kama haija kamilika ,huja ikiwa na thamani ndogo sana na kukua kila watu wanavyozidi kuitegemea ,pia inakuja na. Desturi ya kurahisisha ugunduzi wa mifumo mingine,huja ikiwa na wawekezaji wachache kwani hua haiaminiwi na watu wengi mpaka watakavyo ona manufa yake sasa kwa kutumia tabia hizi ndio tunaweza kujitengenezea kipato.

Ukijaribu kuchunguza mifumo mingi mikubwa iliyo gunduliwa hivi karibuni basi utaona wanufaika wake niwale walio wekeza mapema kabla mifumo haijakua na thamani kubwa, wale walio wekeza nguvu zao kutafta maarifa ya utumiaji wa mifumo hio,pia kuna wale walio jikita kugundua dosari zake na kuboresha au hata kugundua mifumo mingine bora zaidi na je kwanini tuziamini sifa hizi chache kama zitasaidia kukuza uchumi binafsi?

Nta thibitisha hoja hii kwa kutumia mfumo uliogunduliwa na mtanzania mwenzetu Benjamin ferinandez (Nara) kutoka kweny moja ya mohojiano yake alieza namna gani watu walidharau wazo lake na kukata kuwekeza kwake hii ina sadiki kama mfumo wowote unavo anza hua na thamani ndogo sana hivyo hua ngumu kushawishi wawekezaji kuwekeza hapo ila kwa wale walio kua na uthubutu leo hii wana nufaika sana na sio tu wawekezaji walikata bali hata wataalamu wenye taaruma zao za ufanyaji kazi walikua wachache kwani wengi hawakuona thamani yake,vile vile nina amini japo yeye binafsi hajawai sema ila kama kilicho msaidia kugundua mfumo hu ni kutumia mapungufu ya mifumo iliyo kuepo.

Hivyo basi ni mapendekezo yangu kwa vijana hasa wakitanzani kuchakata na kuhakikisha wanakua wanufaika wa mifumo mbali mbali ya kiteknolojia nita shauri mfumo mmja na ntachambua kwa ufupi.mfumo wa Blockchain mfumo hu nimfumo ambao unakua kwa kasi sanaa basi tujitaidi kutafuta fulsa zilizopo haijarishi uwe ume soma au raha kwani kama una kipatio kikubwa na huna elimu basi jitaidi kuwekeza kwenye mfumo huu pia nivyema kuendelea kutafuta sehemu ambao bado hauja kamilika ili kuuboresha zaidi pia kuendelea kugundua fulsa nyingine ambazo hazija gunduliwa lakini zitatumika kutokana na mfumo huu kama ilivyo tokea mwaka 2021 ambapo watu waligundua michezo ya cheza ulipwe ambayo ina wezeshwa na misingi ya blockchain na huo nimfano tu kwani fulsa zipo nyingi zitakazo zalishwa na mfumo huu hivyo basi ni vema kuuzunguka kila upande ili kujua upande ulio kua hauja jikamilisha vile vile kwa kuutazama mfumo huu miaka kadha kutoka hapa utakua umeteka sana dunia hivyo nivyema kuendelea kujitaftia maarifa ili kuto kuteswa na madadiliko haya,

Pia mfumo mwingine ambao unakua na ni vyema kuutazama kwa namna ya pekee ni ukuaji wa matumizi ya roboti katika ufanyaji kazi na kama vijana tunapaswa kuuzungukunguka mfumo huu kila pande kwani bila kufanya hizo hatuta kua wanufaika wa mfumo huu mbinu chache za kuweza kuuzunguka nikwa kuji anda kitaaluma namna ya kutumia mfumo huu,pia kufatilia na kuwekeza kwenye makampuni ambayo ya na maleng chanya na mikakati bora ya uzalishaji wa mitambo hio kwani pindi ikianza kutumika basi thamani ya hisa ya makampuni hayo itakua kubwa sana vile vile kama vijana tuna paswa kuendelea kuchunguza mapungufu yanayo weza kuji tokeza pale mitambo hio ikianza kufanya kazi ili kutatua mapema ili pale itakapo wasili basi tuweze ku tumia kama fursa kwetu na mifumo mingine inayo kua kwa kasi ambayo ninge shauri watu wa jikite nayo ni mifumo ya ulinzi dhidi ya miamala ya mitandaoni au udukuzi wa namna yoyote ile ili tuwe wanufaika lazima tukubali kwamba miaka michache ijayo dunia yetu ita fanya mambo yote kwa asilimia kubwa kutumia mitandao na komputa kwa maana kwamba hata uharifu basi utahamia sana kwenye mifumo io itapelekea ongezeko kubwa la uhitaji wa watu wenye uelewa wa kupambana zidi ya waharifu hao.na cha muhimu katika hili nikwamba wata takiwa wale wenye mbinu za peke ,uelewa wapeke na kuweza kua na sifa hizo ni lazima uwe umegundua dosari na mapungufu ya mbinu zingine hivyo mifumo yote ita sadiki sifa na tabia nilizo zieleza .
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…