SoC02 Siri ya Kunasa Wateja kwenye Biashara yako yafichuka

Stories of Change - 2022 Competition

Vividola

Member
Joined
Jul 6, 2022
Posts
5
Reaction score
0
UTANGULIZI
Mfanyabiashara ni mtu anayeuza bidhaa au huduma katika soko fulani. Mfano soko la mifugo la Vingunguti. Lengo kuu huwa ni kuuza, na kuuza ni lazima apate wateja wanaohitaji bidhaa au huduma yake na wana uwezo wakununua.

MAANA YA KUUZA
Kuuza ni kitendo cha kubadilishana hisia kati ya muuzaji na mnunuaji. Hivyo muuzaji lazima awe na hisia ya kuuza ili kumuambukiza mnunuaji na ndipo anunue bidhaa au huduma unayotoa.

Katika andiko hili, nitaangazia katika ulimwengu wa leo mfanyabiashara anatakiwa kuwa namna gani ili kupata wateja wengi kwa mda mfupi na gharama nafuu. Nitaangazia taaluma ya “Copywriting”, Nitaangazia nini anatakiwa kufanya na wapi kutangazia biashara yake. Pia nitaangazia mambo ambayo anatakiwa ayafahamu pale anapokuwa na biashara.

SABABU YA WAFANYABIASHARA KUHANGAIKA KUPATA WATEJA.
Wafanyabiashara walio wengi wanakosa sifa zifuatazo;
  • Hawajui biashara yao inamlenga nani na pengine mlengwa ana tatizo gani.
  • Hawajui mteja wao anapatikana wapi. mfano bidhaa za wazee umri kuanzia miaka 70 kisha unatangaza bidhaa hizo Instagram ambako wazee wengi sio wapenzi wa mtandao huo na hivyo sio rahisi kuuza.
  • Hawaelewi namna gani ya kutangaza kupata wateja wengi, kwa gharama ndogo na kwa mda mfupi.
  • Hawatoi ofa kwenye biashara zao ili kumuaminisha mteja ubora wa bidhaa au huduma zao.
PEMBE TATU ZA SOKO MFANYABIASHARA ANATAKIWA KUZIFAHAMU
1. Soko (market)
– Hapa ni kwamba unamlenga nani kwenye biashara yako? Kuna msemo unasema "huwezi muuzia nyama mtu anayekula mbogamboga hata kama nyama yako ni tamu kiasi gani". Mfano Daktari Bigwa wa Mifupa yeye analenga watu wenye matatizo ya mifupa tu. Tayari anakuwa amebobea kwenye kundi maalumu la wagongwa, au kuuza nguo kwa ajili ya watoto tu n.k.

2. Ujumbe (Messege) – Lazima ujumbe wako uwe mzuri na uwafikie walengwa hasa. Na kinyume chake ni kwamba kama una ujumbe mzuri lakini umewafikia walengwa ambao sio sahihi kwa soko lako hautapata wateja. Mfano wa mtu anayekula mbogamboga na wewe unataka umuuzie nyama ata kama nyama yako ni tamu sana na tangazo lako ni zuri sana, kwa vile uliyemlenga sio sahihi basi utakuwa unapoteza muda tu.

3. Jukwaa (Medium) – Kumbuka kila soko huwa lina jukwaa lake, mfano ukitaka kulenga wazee wa miaka kuanzia 70 au 80 basi jukwaa kama WhatsApp au Facebook linaweza lisiwe sahihi kuwanasa wazee hawa kama wateja kwa bidhaa au huduma zako ila TV na Magazeti yaweza kuwa jukwaa sahihi kwao.

Swali la kujiuliza kila siku ni je soko lako (walengwa wako) wanapatikana katika jukwaa gani? Je ni Facebook, au ni YouTube au ni magazeti, au Instagram.

MFANYABIASHARA ANATAKIWA AWEJE ILI KUNASA WATEJA WENGI
Wafanyabiashara wengi hujiona kama ni watu wa kuuza bidhaa kuliko kujiona ni watu wa masoko (Marketer).

Mfano kama mtu anamiliki clinic ya tiba asili asijione kama ni mmiliki wa clinic badala yake ajione ni mfanyabiashara wa kutangaza tiba kwa njia ya asili. Au ajione yupo katika biashara ya kutangaza namna ya kupendeza ikiwa anamiliki duka la nguo. Kwa lugha rahisi bidhaa au huduma anayoitoa ni jambo la pili sio tena jambo la kwanza.

Kwahiyo ili kupata wateja na kwa mazingira ya kileo mfanyabiashara anatakiwa kujiona ni mtu wa matangazo zaidi kuliko kujiona ni mtu wa kutoa bidhaa au huduma fulani.

NB: “Kuna msemo unasema kama hutangazi kila siku huna haki ya kumiliki biashara” maana yake huna haki ya kupata wateja.

TAALUMA YA “COPYWRITTING” KWENYE MATANGAZO
Copywriting ni taaluma ya kuandika matangazo ambayo mtu yeyote akisoma mfano tu kichwa cha habari lazima avutiwe kusoma kilichomo ndani, na hivyo mstari wa kwanza lazima umvutie kusoma mstari wa pili na wa tatu n.k. waweza kujifunza taaluma hii hapa The Gary Halbert Letter au www.swipped.com

Mfano wa tangazo lenye mtindo wa copywriting ni kama hivi; “SIRI YA KUNASA WATEJA KATIKA BIASHARA YAKO YAFICHUKA”. Kisha unaendelea na maelezo ya kuendelea kumvutia mteja asome tangazo lako mpaka mwisho. Kuna msemo unasema “A PERSON WHO BOUGHT A DRILL DID NOT WANT TO BUY A DRILL, HE WANTED TO MAKE A HOLE. SO IF YOU WANT TO SELL A DRILL ADVERTIZE HOW TO MAKE A HOLE”. Kwa hiyo ukitaka kumuuzia mtu mfano dawa ya vidonda vya tumbo, mfundishe namna ya kutibu vidonda vya tumbo.

AINA YA MATANGAZO
Kupata wateja wengi, biashara ni lazima itangazwe. Wapo watu wenye bidhaa na huduma nzuri sokoni lakini hawauzi sana kwa sababu ya kukosa kutangaza ama kutangaza biashara zao visivyo.

Danny Kennedy anasema “The business owner who spend more money in advertising is the winner in the market”. Kwahiyo ukiwekeza kwenye matangazo kuliko washindani wako utakuwa mshindi wa soko kwa kupata wateja wengi zaidi hata kama bidhaa zako sio bora kama zao.

AINA MBILI YA MATANGAZO;
1. Institutional Advertising au huitwa Branded Advertising au ME Advertising
– Hii ni aina ya Matangazo yanayozungumzia na kusifu bidhaa au huduma unayotoa au kusifu kampuni.

Mfano: Matangazo yanayosema njoo ununue bidhaa zangu ni nzuri n.k faida yake ni kwamba kama una budget kubwa basi watu watazoea brand na bidhaa zako na kuiamin biashara japo imani hiyo hujengeka kidogo kidogo.

Kwa biashara ndogo, aina hii ya matangazo inaweza kuua biashara yako kwa kuwa matangazo yake huwa ni gharama. Mfano matangazo ya kwenye TV juu ya bidhaa au huduma Fulani.

2. Direct Response Advertising au huitwa YOU Advertising - Hii ni aina ya matangazo yanayolenga kuzungumzia shida na utatuzi wa matatizo ya mteja wako.

Mfano kama una dawa ya kupunguza unene badala useme PATA DAWA BORA YA KUPUNGUZA UNENE, unaweza sema JINSI YA KUPUNGUZA KILO 5 NDANI YA SIKU 5 BILA KUFANYA MAZOEZI. Kisha unamuelekeza namna ya kutatua changamoto yake ya unene (Value) kabla ya kuzungumzia bidhaa au huduma unayotoa.

Mara nyingi baada ya kutoa elimu (Value) mteja wako huanza kukufahamu, kukuamini, na anaanza kukupenda kitu ambacho unapomwambia juu ya biashara yako huwa ni rahisi sana kununua.

Matangazo ya YOU Advertising huwa ni ya gharama nafuu na huokoa mda. Angalia mfano wa tangazo linalovutia wateja hapa Anti-Wrinkle Cream Ads Using The Same “Reduce Up to 56%” Hook » Swipe File Archive » Marketing & Copywriting Examples

HITIMISHO
Mara nyingi taaluma hii ya copywriting haifundishwi sana darasani, hivyo bas nashauri wafanyabiashara watafute maarifa haya kwa wataalamu wa masoko nje ya wale waliosomea darasani na kusoma vitabu kama kitabu cha Sell Like Crazy cha Sabri Suby (Amazon.com) au Makala kama za Gary Halbert (The Gary Halbert Letter).
 
Upvote 3
UTANGULIZI
Mfanyabiashara ni mtu anayeuza bidhaa au huduma katika soko fulani. Mfano soko la mifugo la Vingunguti. Lengo kuu huwa ni kuuza, na kuuza ni lazima apate wateja wanaohitaji bidhaa au huduma yake na wana uwezo wakununua.

MAANA YA KUUZA
Kuuza ni kitendo cha kubadilishana hisia kati ya muuzaji na mnunuaji. Hivyo muuzaji lazima awe na hisia ya kuuza ili kumuambukiza mnunuaji na ndipo anunue bidhaa au huduma unayotoa.

Katika andiko hili, nitaangazia katika ulimwengu wa leo mfanyabiashara anatakiwa kuwa namna gani ili kupata wateja wengi kwa mda mfupi na gharama nafuu. Nitaangazia taaluma ya “Copywriting”, Nitaangazia nini anatakiwa kufanya na wapi kutangazia biashara yake. Pia nitaangazia mambo ambayo anatakiwa ayafahamu pale anapokuwa na biashara.

SABABU YA WAFANYABIASHARA KUHANGAIKA KUPATA WATEJA.
Wafanyabiashara walio wengi wanakosa sifa zifuatazo;
  • Hawajui biashara yao inamlenga nani na pengine mlengwa ana tatizo gani.
  • Hawajui mteja wao anapatikana wapi. mfano bidhaa za wazee umri kuanzia miaka 70 kisha unatangaza bidhaa hizo Instagram ambako wazee wengi sio wapenzi wa mtandao huo na hivyo sio rahisi kuuza.
  • Hawaelewi namna gani ya kutangaza kupata wateja wengi, kwa gharama ndogo na kwa mda mfupi.
  • Hawatoi ofa kwenye biashara zao ili kumuaminisha mteja ubora wa bidhaa au huduma zao.
PEMBE TATU ZA SOKO MFANYABIASHARA ANATAKIWA KUZIFAHAMU
1. Soko (market)
– Hapa ni kwamba unamlenga nani kwenye biashara yako? Kuna msemo unasema "huwezi muuzia nyama mtu anayekula mbogamboga hata kama nyama yako ni tamu kiasi gani". Mfano Daktari Bigwa wa Mifupa yeye analenga watu wenye matatizo ya mifupa tu. Tayari anakuwa amebobea kwenye kundi maalumu la wagongwa, au kuuza nguo kwa ajili ya watoto tu n.k.

2. Ujumbe (Messege) – Lazima ujumbe wako uwe mzuri na uwafikie walengwa hasa. Na kinyume chake ni kwamba kama una ujumbe mzuri lakini umewafikia walengwa ambao sio sahihi kwa soko lako hautapata wateja. Mfano wa mtu anayekula mbogamboga na wewe unataka umuuzie nyama ata kama nyama yako ni tamu sana na tangazo lako ni zuri sana, kwa vile uliyemlenga sio sahihi basi utakuwa unapoteza mda tu.

Mara nyingi taaluma hii ya copywriting haifundishwi sana darasani, hivyo bas nashauri wafanyabiashara watafute maarifa haya kwa wataalamu wa masoko nje ya wale waliosomea darasani na kusoma vitabu kama kitabu cha Sell Like Crazy cha Sabri Suby (Sell Like Crazy: How To Get As Many Clients, Customers and Sales As You Can Possibly Handle: Sabri Suby: 9780648459903: Amazon.com: Books) au Makala kama za Gary Halbert (The Gary Halbert Letter)

Asante
 
Back
Top Bottom