Siri ya kupenda kukaa kaunta sisi wanywaji

Hilo eneo kukaa sababu kuu ni moja, siku hiyo una mood ya kuongea sana,
na hata kutongoza Msupa yeyote atakae kuvutuia.

Si unajua hata kutongoza inategemeana na mood, siku ukiwa vibaya kichwani hata akipita demu ukampenda huwezi kumsemesha.
 
Siri Ni: Napenda kuona kinywaji changu kinatokea wapi kinaandaliwaje na napewaje kisha sipendi Shobo Mdundo!.

Also, I'm not good at waiting especially when am thirsty. Cheers πŸ₯‚πŸ»πŸ€
 
Mimi naona watu wenye hela huwa hawakai kaunta.
Ila wale wenye hela za kuvizia ndiyo huwa wanapenda kukaa mbele pale waonekane na wenyewe wamo.
Watu wenye hela zisizo za mawazo hupendelea zaidi kukaa pembeni huku.
 
Ukinikuta nimekaa Kaunta basi ujue hiyo bar ina Wahudumu wazembe wazembe
 
Huku Kwetu Kwamtogole, land Lord akishakusanya pesa anakwenda bar kuchukua bia zake mbili na anatoa kochi barazani na stool yenye kitambaa, kila anaepita anamuona kuwa yeye ni mtu wa vizibo na si wa matapu tapu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…