Na, Mwl.Pasaka Osunga
Leo ningependa kukumbusha msemo ambao Ken Levine aliwahi kusema-“We all make choices, but in the end our choices make us.” Akimaanisha kuwa wote tunaweza kufanya maamuzi lakini mwisho wa siku maamuzi ndiyo huamua aina ya maisha tunayokuwa nayo.Huu ndio ukweli wa mambo katika maisha yetu,kwa popote tulipo sasa na chochote tulichonacho kwa sasa ukweli ni kwamba vimetokana na maamuzi ambayo tuliyafanya huko nyuma kwenye maisha yetu.
Hata hivyo watu wengi sana wamekwama kwenye maisha yao kwa kushindwa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati kuhusiana na maisha yao na yale wanayoyataka kuyapata.Ukweli ni kuwa kudumaa kwingi ambako watu wamekutana nako kwenye maisha yao kunatokana haswaa na tabia ya kutopenda kufanya maamuzi katika maisha yao.Hii ndio maana Mark Twain alisema miaka ishirini kuanzia leo utajutia zaidi mambo ambayo hukufanya zaidi ya yale uliyofanya.Kama kweli unataka kufanikiwa katika ndoto za maisha yako basi ni lazima ufanye maamuzi thabiti katika maisha yako kuhusiana na mambo muhimu.
Kabla hatujaangalia ni aina gani ya maamuzi tunayotakiwa kuyafanya kama tunataka kufanikiwa katika maisha yetu ni muhimu kujua kuwa bila kuwa na mwelekeo thabiti(focus) wa kitu ambacho unataka katika maisha yako basi itakuwa ngumu sana kwako kuweza kufanya maamuzi sahihi.Hivyo basi jambo la kwanza kabla haujaendelea kujifunza aina na namna ya kufanya,ni lazima ujiulize-“Hivi mimi nataka kupata nini kwenye maisha yangu”.Kadiri unavyokuwa “clear” kwenye mwelekeo wa maisha yako ndivyo unavyopata urahisi zaidi wa wewe kufanya maamuzi kila wakati inapobidi.
Ili ufanikiwe utahitajika kufanya aina mbili zifuatazo za maamuzi katika maisha yako:
Amua Kuwajibika Kuhusu maisha Yako.
Mafanikio huanza na kutambua kuwa kila hali uliyonayo ni wajibu wako kuibadilisha na sio mtu mwingine yoyote yule.Ni lazima ufike sehemu ambayo unaamini kwa dhati kuwa “Hatima ya maisha yako iko mikononi mwako”.Kila wakati unapoanza kulaumu mtu,serikali,bosi wako,wazazi,marafiki,maadui ama bahati mbaya ulizowahi kuzipata katika maisha yako hapohapo unapoteza nguvu ya kubadilisha maisha yako.
Haijalishi nani alikufanyia nini kibaya,yaliyopita ni historia-Kuanzia hapo ulipo unao uwezo wa kutengeneza historia mpya.Lazima ufanye maamuzi hayo leo na uyafanye sasa hivi.Amua kuwasamehe wote waliokukosea katika maisha yao,amua kuwa unazo nguvu na uwezo wa kufanya kitu kizuri kuanzia wakati huu,amua kuwa unaweza kabisa kuanza upya.Fanya maamuzi ya kuwajibika na maisha yako.
Jambo lingine katika kuwajibika na maisha yako ni kutokubali kuwa mtu ambaye kila wakati unawaza-“Hivi watu watasemaje nikifanya hivi?”-Haujaumbwa kuwaridhisha watu umeumbwa kutimiza kusudi la maisha yako.Usiendelee kuishi maisha ya kuumia ili mradi tu kuna watu unawafurahisha na unaogopa eti ukichukua uamuzi fulani watasemaje.Kuna watu leo wapo kwenye kazi wasizozipenda kabisa ila wanaogopa kuacha na kutafuta kazi nyingine kwa sababu tu wanahofia watu watasemaje,kuna watu leo wako kwenye mahusiano ambayo wanaumia kila siku na wanakosa ujasiri wa kusema ama kuchukua hatua eti wanaogopa watu watasemaje?Usikubali kuishi maisha yako yote kwa kuumia eti ili mradi tu unawaridhisha watu wengine.Maisha yako ni yako mwenyewe.Usiishi maisha ya kutafuta “hadhi” ishi maisha ya kutimiza “lengo”.Don’t live to GAIN a STATUS but live to FULFILL your PURPOSE.
Amua kufanikiwa katika malengo makubwa sana
Napenda msemo ambao Les Brown aliwahi kusema-“Shoot the Moon because even when you fail,you will land on the stars”(Lenga Mwezi kwani hata ukikosa kuupata utaangukia katika nyota”.Kama kweli unataka kupata mafanikio ni lazima uwe na malengo makubwa sana katika maisha yako.Malengo madogo hupelekea mafanikio madogomadogo sana ambayo huwa hayawafikishi watu mbali.
Kila wakati ninapowaza kuhusu malengo huwa nawaambia watu waweke kitu kinaitwa “Breakthrough goal”-Lengo kubwa moja ambalo ukifanikiwa kulipata basi litakupa hadhi mpya katika maisha na utakuwa umefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.Hili ni lengo ambalo siku likitokea basi kila mtu atajua umefanikiwa ikiwemo na wewe mwenyewe pia.
Hebu fikiria sasa unataka kuweka lengo gani-Kuna mwingine atataka kushinda medali katika michezo ya olimpiki,mwingine kujenga nyumba,mwingine itakuwa kuandika kitabu na kuuza kopi elfu kumi,mwingine kurekodi albam yake n.k Kila mmoja anayefanikiwa ni lazima huwa anaweka lengo la namna hii.Ukifanikiwa katika malengo ya namna hii yatakupa ujasiri wa kuweka malengo mengine makubwa zaidi.
Najua unajiuliza mbona nikiweka malengo makubwa nitafeli-Kumbuka kile alichosema Bill Cosby "In order to succeed, your desire for success should be greater than your fear of failure." Ili ufanikiwe ni lazima shauku yako ya kufanikiwa iwe kubwa kuliko hofu yako ya kushindwa.Usihangaike na hofu ya kushindwa,jenga hamu yako kubwa ya kufaulu katika jambo unalotaka.Uwe kama mtu ambaye hajui kuogelea aliyetupwa kwenye maji-Hivi kama ndio wewe haujui kuogelea ukitupwa kwenye maji,utasema ngoja tu nife kwa sababu sijui kuogelea?Bila shaka hapana.Utajitahidi kadiri unavyoweza kujiokoa.Ndivyo ilivyo,unapojiwekea malengo makubwa unajikuta unafanya bidii kuyafikia kwa kila namna.Kinachowafanya watu wasifanikiwe katika malengo makubwa ni kwa sababu huwa wanaweka malengo madogo na sio kwamba hawawezi kufanikiwa katika malengo makubwa.
Hivyo baada ya kuamua lile lengo kubwa ulilonalo katika maisha yako:Hebu jiulize,hivi kuna vitu gani/mambo gani natakiwa kuyaacha ili kuweza kutimiza lengo ninalotaka kulifikia?.Kama ulivyotumia muda kuweka “breakthrough goal”.Tumia muda pia kuandika mambo gani unatakiwa kuyaacha ili kuweza kutimiza lengo lako.
Tutaendelea wakati ujao na siri ya mafanikio sehemu ya pili............
0756231744.