Siri ya Moyo: Acha kabisa kumpenda mtu ambaye umeshagundua na kujithibitishia kuwa moyo wake haukukubali

Siri ya Moyo: Acha kabisa kumpenda mtu ambaye umeshagundua na kujithibitishia kuwa moyo wake haukukubali

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
SIRI YA MOYO

Katika Maisha Yetu Duniani nimegundua kwamba tunatumia muda mwingi kujirekebisha ili tuonekane wazuri, warembo, na ma-handsome 😍😎 β€” wajanja na watu makini.

Lakini nimegundua mambo mawili:

1: Nimegundua kuwa wale watu wanaotupenda kwa dhati, huwa hawatutazami kwa macho yao zaidi, bali mioyo yao ndio hufanya kazi kubwa katika kutupenda. Ndiyo maana, pamoja na uzuri wa sura na maumbo yetu, haipingiki kwamba tunayo madhaifu mengi sana ambayo macho yao ya kawaida huyatazama.

Lakini mioyo yao iliyotudhamini na kutuamini hujua kwamba siku moja tutabadilika. Wachache wetu hubadilika, na wengine wetu hatuwezi kubadilika kabisa 😎😎😎.

Ndiyo maana mtu ambaye amependwa kwa moyo, kumchomoa ndani ya moyo huwa ni ngumu sana. Ni juhudi inayoweza kuchukua miaka na miaka. Wazungu huita First Love.

Ndiyo maana binti au kijana unaweza kukutana naye kwenye mahusiano 😎... lakini ukawa wewe si mtu wake aliyempenda sana.

Kuwa makini sana unapokutana na binti mwenye maumivu ya kuachwa au kutendwa. Mbaya zaidi ni yule anayekuambia, "Yaani ninamchukia fulani ambaye ni ex wangu..." 😎

Hizo zote ni ishara kwamba huyo mwamba ameshaweka alama kubwa moyoni kwa binti. Inawezekana hata kamwachia mtoto 😎😎😎.

Hivyo, ukikaa vibaya, unaweza kutumika kama chombo cha kumkomoa ex, au chombo cha kupooza maumivu 😎😎.

Siku akipona, huyo atapeperuka tena. Cha mtaani kuna siku hurudi mtaani kusalimia πŸ˜‹πŸ˜ŽπŸ˜Ž.

Hivyo, pointi yangu Dogoli Kinyamkela, ni kwamba wanaotupenda hufumba macho yao kutazama madhaifu yetu na hufungua mioyo yao kutupenda tu kama tulivyo. πŸ₯ΈπŸ₯ΈπŸ₯ΈπŸ˜ŽπŸ˜Ž β€” Ndiyo mapenzi yalivyo.

2: Jambo la pili nililoliona ni kwamba wale wasiotupenda sisi, wana macho yanayoona kabisa matendo na juhudi zetu. Wanaona kabisa muda mwingi tunaoutumia kwa ajili yao. Wanaona kabisa jinsi tunavyopigana vita vikali kwa ajili yao, pengine hata kwa ajili ya familia na watoto wao. Wanaona kabisa jinsi tunavyoumenya uchumi wetu kwa ajili yao πŸ₯΄πŸ˜Ž.

Lakini mioyo yao imekumbwa na uziwi na upofu β€” haiwezi kutuona na wala haiwezi kutusikia πŸ₯ΈπŸ₯ΈπŸ₯ΈπŸ˜ŽπŸ˜Ž.
Hivyo, haiwezi kutuheshimu hata siku moja.

Kwa maana hiyo, moyo wa mtu ukigundua haukukubali kabisa 😎, acha kupoteza muda wako kwenye huo mgodi uliotekwa na watu wengine. Huo ni mgodi usio na madini kwa ajili yako. Utapoteza fedha nyingi hapo, jasho, na wakati mwingine hata machozi πŸ₯Έ.

HITIMISHO:

Acha kabisa kumpenda mtu ambaye umeshagundua na kujithibitishia kuwa moyo wake haukukubali.
Maana hutanufaika katika hilo shamba πŸ€ͺ. Utapanda na hutavuna 😎. Utaposa na watakaozalisha ni wengine.

Ahsante kwa kusoma na kunielewa

Content created by: Dogoli Kinyamkela
 
Back
Top Bottom