Siri ya serikali 2: kwanini haziepukiki

Geeky

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
307
Reaction score
179
KWA NINI SERIKALI 2 HAZIEPUKIKI?:

Uchumi Zanzibar unategemea Bara
---------------------------------------------------------
Sehemu ya mji wa Zanzibar
WAKATI Bunge Maalum la Katiba likisuasua katika kuunda kanuni za kuongoza wajumbe wake, taarifa zinaonesha katika muundo uliopo wa serikali mbili, mbali na kuimarisha umoja na mshikamano wa Taifa, pia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imekuwa ikinufaika nao kiuchumi.

Taarifa hizo za kiuchumi, zinaungana na taarifa za kisiasa na kijamii kusisitiza umuhimu wa muundo wa Muungano wa serikali mbili, tofauti na wa serikali tatu uliopendekezwa na rasimu ya Katiba mpya, zilizokwishatolewa na baadhi ya wasomi na viongozi mbalimbali katika jamii.

Viongozi hao, akiwemo Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycapy Kadinali Pengo na Profesa Bonaventura Rutinwa wa Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamebainisha kuwa umoja na mshikamano wa Watanzania unalindwa vizuri na muundo wa serikali mbili, kuliko itakavyokuwa na serikali tatu.

Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Hamphrey Moshi, katika sura aliyoandika katika kitabu cha Katiba Bora Tanzania, amebainisha kuwa katika muundo uliopo, SMZ imekuwa ikipata huduma za mambo ya Muungano bila kulipia, huku baadhi ya madeni yake yakilipwa na Serikali ya Muungano tofauti na itakavyokuwa katika muundo wa serikali tatu.

“Kama muundo huu (serikali tatu), utakubalika, SMZ lazima ijitegemee katika kugharimia shughuli zake za kinchi na kwa kuwa Zanzibar itakuwa sawa na Tanganyika, haitakuwa na maana Zanzibar kuacha kulipia ghama za Muungano sawa na idadi yake ya watu,” amebainisha Profesa Moshi katika kitabu hicho kilichochapishwa hivi karibuni.

Gharama za Muungano
--------------------------------------
Kwa mujibu wa Profesa Moshi, tangu kuasisiwa kwa Muungano, takwimu zinaonesha SMZ imechangia gharama za shughuli za Muungano mara tatu tu.

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka wa fedha 1964/1965, ambapo takwimu zinaonesha kuwa gharama za mambo ya Muungano zilikuwa Sh milioni 107 na SMZ ilichangia Sh milioni 10, sawa na asilimia tisa ya gharama za uendeshaji.

Mwaka wa fedha 1965/1966, takwimu hizo zinaonesha gharama za mambo ya Muungano ziliongezeka na kuwa Sh milioni 153, na mchango wa SMZ uliongezeka na kufikia Sh milioni 12 ingawa tafsiri yake ni kwamba mchango huo ulipungua na kuwa asilimia nane ya gharama hizo.

Takwimu za mwisho za mchango wa SMZ katika shughuli za Muungano, zimetajwa kuwa ni za mwaka wa fedha 1966/1967, ambapo gharama zilikuwa Sh milioni 176 na mchango wake ulipungua zaidi na kuwa Sh milioni 8.1, sawa na asilimia tano ya gharama hizo.

Profesa Moshi amebainisha kuwa hakuna takwimu zaidi zinazoonesha mchango wa SMZ katika shughuli za Muungano baada ya mwaka wa fedha 1966/1967, wakati gharama hizo zikiongezeka mara dufu.

Kwa mfano mwaka 2000 Bajeti ya mambo ya Muungano iliyotolewa na Serikali ya Muungano, ambayo sasa inashutumiwa kuwa ni Serikali ya Tanganyika iliyovaa koti la Muungano, imetajwa ilikuwa Sh bilioni 474 wakati mwaka 2006, mambo ya Muungano yalichukua Sh bilioni 556.1.

“Kwa wastani kwa miaka mitano kati ya 2005 mpaka 2010, Tanzania Bara imekuwa ikitenga asilimia 22 ya Bajeti yake kugharamia shughuli za Muungano.

Inaonesha kuwa Zanzibar imeshindwa kutoa mchango wowote katika miaka hii mitano. “Pamoja na Zanzibar kuonekana kushindwa kuchangia gharama za shughuli za Muungano, jambo ambalo linapingana na Ibara ya 133 ya Katiba iliyopo, hakuna ushahidi kwamba SMZ imewahi kuitwa kujieleza kwanini haitoi mchango wake,” ameeleza Profesa Moshi.

Jaribio la Kurekebisha

Kwa mujibu wa Profesa Moshi, mwaka 1977 Kamati ya Shelukindo, ilitakiwa kupendekeza fomula ya haki na ya wazi ya mchango wa SMZ katika gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano.

“Mapendekezo yalikuwa Zanzibar ilipe asilimia 3.9 ya matumizi yote ya shughuli za Muungano. Hata hivyo, inavyoonekana hili halijawahi kutekelezwa. “Mbali na Kamati ya Shelukindo, mapendekezo kama hayo yalitolewa kwa mara nyingine ili kutatua kero hiyo na Tume ya Nyalali (1992) na Tume ya Kisanga (1998),” amefafanua Profesa Moshi.

Hisa za Zanzibar

BoT Tofauti na ilivyo kwamba Zanzibar imekuwa ikishindwa kutoa mchango wake katika gharama za Muungano, Serikali ya Muungano kupitia Benki Kuu (BoT), imekuwa ikitoa gawiwo la hisa za Zanzibar kwa SMZ la asilimia 4.5 kila mwaka.

Hisa hizo zinatokana na kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo Zanzibar na Tanzania Bara zilikuwa nchi wanachama na wanahisa katika Bodi ya Fedha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACB).

Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya, Zanzibar haikupata hisa zake asilimia 11.05, zilizokuwa zikionesha umiliki wake katika EACB na kugeuka kuwa sehemu ya kero za Muungano.

“Hata hivyo mwaka 1994, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), lilishauri Zanzibar ipate asilimia 4.5 ya gawiwo kutoka BoT,” ameeleza Profesa Moshi.

Kiwango hicho cha gawiwo kimekokotolewa kwa kuzingatia sehemu ambayo Zanzibar inachangia katika uchumi wa Tanzania na idadi ya Watanzania, ambayo ni wastani wa asilimia tatu.Profesa Moshi amebainisha kuwa tangu 1995, SMZ imekuwa ikipata gawiwo hilo kutoka BoT.

Madeni
------------
Profesa Moshi ameeleza kuwa uwezo wa SMZ kukopa ni mdogo, kwa kuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ndiye mwenye mamlaka ya kukopa kwa niaba ya serikali zote.

“Hii maana yake ni kwamba SMZ, haina mamlaka ya kutafuta mkopo kwa ajili ya matumizi yake na kama inataka mkopo, lazima iombe kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano. “Serikali ya Jamhuri ya Muungano baada ya kupokea maombi ya Zanzibar, itaomba mkopo kutoka nje na ikifanikiwa, itatoa sehemu ya mkopo huo iliyoombwa na Zanzibar na kuipa SMZ,” ameeleza Profesa Moshi.

Ameeleza kuwa kwa juu juu, inaonekana kuwa Zanzibar inaumizwa kiuchumi, lakini uchambuzi wa ndani unaonesha namna SMZ inavyonufaika katika mfumo huo.

Yasiyolipika
-------------------
Kwa mujibu wa Profesa Moshi, kwa kuwa mikopo ya Zanzibar inadhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, mpaka mwaka 2002 utaratibu ulikuwa SMZ ikishindwa kulipa deni, linalipwa Serikali ya Muungano kwa niaba ya SMZ.

Kuanzia mwaka wa fedha 2001/2002, Profesa Moshi amebainisha kuwa SMZ imekuwa ikiruhusiwa kukopa kwa kuuza hati fungani kupitia BoT.

Hata hivyo kwa mujibu wa Profesa Moshi, BoT ililazimika kuunda akaunti maalumu, ili SMZ iliposhindwa kulipa deni, benki hiyo ilipe na kukata katika gawiwo ambalo linapaswa kutolewa kwa SMZ.

Pamoja na madeni hayo ya kiserikali, Zanzibar pia imetajwa kuwa na madeni makubwa ya kibiashara, likiwemo la Shirika la Umeme (Tanesco) kwa Shirika la Petroli Zanzibar (ZSFPC).

“Ingawa ZSFPC imeandaa mpango wa kulipa deni lake kwa Tanesco kwa miaka 15 mpaka 2018/19, uzoefu wa nyuma unaonesha kuwa Serikali ya Muungano huenda ndiyo itakayolipa deni hilo,” ameeleza Profesa Mushi.

Maoni CUF
------------------
Akizungumzia uchambuzi huo wa Profesa Moshi, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Julius Mtatiro, alisema uchambuzi huo si wa kweli na mfumo wa serikali mbili unaonesha Tanganyika inajikomba kwa Zanzibar.

Alitoa mfano wa Sekta ya Utalii, kwamba kungekuwa na muundo mzuri wa Muungano, Zanzibar wangekuwa na ushirikiano na nchi za kimataifa na kufanya mambo makubwa.

“Tuwaachie walipe polisi wao wenyewe, wanajeshi wao wenyewe wataweza kwa kuwa wao ni wachache…Tume mbalimbali zimeundwa zimeshauri serikali tatu, hata Tume ya Mabadiliko ya Katiba ina wazalendo waliofunzwa na Mwalimu Nyerere, wameona hilo,” alisema Mtatiro.

Alisema ndio maana Katiba ya Zanzibar imeonesha kutangulia kutoka uhuru wake, lakini Tanzania Bara imekuwa iking’ang’ania Zanzibar kuwa ni sehemu ya Tanzania,” alisema.

HabariLeo
 
Ngoja twende kwenye kutunga katiba kwanza haya yote yatakuwa bayana watanzania ndiyo watakao amua aina ya muungano wanao taka acheni kubashiri bashiri.
 
Hivi kumbe mtatiro ni naibu katibu mkuu zanzibar we jamaa vipi.
 
Je kwa nini hawataki kulipia?

Visiwa hivi vitandeleaje kuwa sehemu ya Muungano wakati hawalipii gharama?

Hawa waanyakazi wote wa Muungano toka Zanzibar kwa hiyo hulipwa na kodi za Bara kwa miaka hii yote?

Sasa Bara waafaidi nini?
 
Ngoja twende kwenye kutunga katiba kwanza haya yote yatakuwa bayana watanzania ndiyo watakao amua aina ya muungano wanao taka acheni kubashiri bashiri.
Hiyo mnayotunga ipo mifukoni kwenu,ni katiba ya ccm siyo ile tuliyompa Mzee warioba ailete dodoma.
 
Mimi nimekuwa nikihisi pengine kuna maagano ya kiimani waliyofanya wazee wetu walioasisi muungano kiasi kwamba kwa yoyote atakayethubutu kuvunja muungano atakutwa na mabalaa.

Nimekuwa nikijiuliza sana kwa nini wenye kukemea sana utenganifu wa muungano huu wawe CCM pekee?
 
Uyo Prof Mushi mlimnusa mdomo?
...
1 ikiwa serikali mbili zinapelekea maendeleo ya kiuchumi Zanzibar, kwa nini Wazenj wawe mstari wa mbele kukataa Muungano? Kwaiyo wale Uamsho hawana akili, mwenye akili yeye tu?
...
2 anaposema Zbar imeacha kuhudumikia Muungano mwaka 67, jee anamaanisha kuanzia 68 hadi leo, hakuna makato ya Z'bar kwenye Muungano? Jee wewe unakubaliana na hili?
...
Elimu ya Tz ni ya ajabu sana!
Yaani Profesa anaongea pumba kiasi cha kukrashiwa na mtoto wa kidato cha pili tu!
 
Ngoja twende kwenye kutunga katiba kwanza haya yote yatakuwa bayana watanzania ndiyo watakao amua aina ya muungano wanao taka acheni kubashiri bashiri.

kupitia rasimu ya katiba wananchi tumeamua kuwa tunataka serikali 3.
serikali 3 haiepukiki.
 
Ngoja twende kwenye kutunga katiba kwanza haya yote yatakuwa bayana watanzania ndiyo watakao amua aina ya muungano wanao taka acheni kubashiri bashiri.

Mkuu

Maoni ya 61% ya watanzania kwenye rasimu ni serikali tatu,kama kweli kazi ya bunge la katiba ni kufanya marekebisho madogo tu kwenye rasimu hiyo wamepata wapi jeuri ya kutuchagulia na kuturudisha kwenye serikali mbili?

Watanzania walishaamua aina ya muungano wanaoutaka nao ni SERIKALI TATU,hizo nyingine wanazijua wenyewe walipozitoa.

Msiwafanye watanzania wajinga!
 
Kushindawa kuchangia sio issue!!! Mbona Tanzania mpaka Leo ni ombaomba na inategemea misaada kuendesha serikali?? Kama ndiyo hivyo kulikuwa hakuna maana ya kupigania uhuru..... Hawa ndo maprofesa ambao elimu yao sijui imewasaidiaje??
 
Hao wote ni wanadamu wenye hisia zao ambazo zinaweza kusheheni matarajio fulani ya kisekta.
 
Je kwa nini hawataki kulipia?

Visiwa hivi vitandeleaje kuwa sehemu ya Muungano wakati hawalipii gharama?

Hawa waanyakazi wote wa Muungano toka Zanzibar kwa hiyo hulipwa na kodi za Bara kwa miaka hii yote?

Sasa Bara waafaidi nini?

Bara ndio nchi gani?muakilishi wenu ni nani kwanye bunge la katiba?
 

Yakhee kumbe gharama za muungano zishalipiwa yakhee !! If Hali halisi ndio Kama ilivyobainisha hiyo tafiti, then kuna dhulma ambayo inafanyika dhidi ya Watanganyika waziwazi.
 
Tunataka tnganyika yetu tu!
Hayo mengine ni mbwebwe tu!
 
Ni kweli Zenji inaichuna sana Tanganyika kwani Zenji ni Kisiwa kidogo lakini kina Matumizi makubwa sana kwenye Serikari yake baada ya kulundika wafanyakazi wengi sana idadi Kubwa ya watu Zenji hawajui mambo ya Ndani jinsi Uchumi unavyokwenda Ndio Maana hawaishi kulalamika wakiwemo hao Uamsho hawafahamu undani wa Gharama inazoingia Tanganyika kuusujudia Muungano Kaa Ukijua Kuwa Muungano bila Tanganyika njaa lazima ibishe kwa wazenji wahamiaji wa Enzi ya Utumwa wa kiarabu ambao sasa wamesahau asili Yao wamebaki wakiwatusi watanganyika
 
Amini usiamini Siku ikitokea Muungano Ukaparanganyika tu hapo hapo Wazenji wataurejesha Ukoloni wa Kiaraabu na kuishangaza Dunia kwani hawajazoea kujiendesha wenyewe wamezoea kubebwa tu .kwa upande wa Tanganyika yenye madini mbuga na Rasilimali Nyingi sana itakuwa Nchi Tajiri sana kwani Fedha inayotumika kubembeleza Muungano itasalia Hazina na kuinua Uchumi kwa kasi ya Ajabu sana vitaibuka vyanzo vingi vya mapato ambapo sasa Zenji watalipia Viza na vibali vya kuishi Tanganyika Umeme chakula nk watauziwa kwa Dola na Hakuna kulundika Deni yaani muungano huu kwa hakika anayefaidi matunda kwa sasa ni Zenji kisha akishiba anavurumisha Vuvuzela ili kuwapumbaza watanganyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…