Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Katika utafiti wangu juu ya chanzo cha muungano wa Tanganyika na Zanzibar na mapinduzi 'matukufu' au matukutu au mavamizi ya mwaka 1964, nilibahatika kusoma andiko la mtafiti James R Brennan lenye kichwa
Lowering the Sultan’s Flag: Sovereignty and Decolonization in Coastal Kenya (2008) ambapo mtafiti anasema kuwa hapo tarehe 5 Oktoba, 1963 Katibu wa makoloni wa kiingereza Duncan Sandys, Sultan Jamshid.
Waziri mkuu wa Kenya wa wakati huo mzee Jomo Kenyatta na Waziri mkuu wa wakati ule wa Zanzibar Shehe Mohamed Shamte walisaini makubaliano ya kuipa Kenya Zanzibar. Hivyo, Nyerere alipoona hivyo, akawashawishi akina Karume na ASP kuiangusha serikali ya sultan na kuunda muungano wa Tanzania huku akiwapa Zanzibar madaraka na maslahi makubwa kama kishawishi mbali na kuondoa hofu ya akina Karume kupinduliwa.
Hivyo, tunachoambiwa kuhusu mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania si ukweli wote. Kimsingi, Zanzibar ilipaswa kuwa koloni la Kenya kibaraka mkubwa wa Uingereza kwenye ukanda wa Afrika Mashariki. Wenye macho waone na wenye masikio waelewe.
Hizi ndizo siri walizoondoka nazo akina Nyerere, Karume, Jamshid, Shamte, Kenyatta na malkia wa Uingereza. Tuanzie hapa.