The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
Karibu binti na mwana wa Mama Afrika.
Moja ya Vitu ambavyo vinatafutwa na watu wa dini tatu maarufu ya Ukristo, uislamu na uyahudi, ni vibao viwili vya amri kumi za Mungu.
Kwa sababu Maandiko yanadai, vibao hivyo viliwekwa ndani ya sanduku la Agano, vikiwepo fimbo ya harun yenye maua na birika la mana.
Watu wanafanya bidii kutafuta huu ushahidi wa kiimani katika mazingira harisi.
Wachunguzi wanaifukunyua biblia ili kujua mala ya mwisho, masimulizi ya hivi vitu yaliishia wapi ili wachunguze kwa kina maeneo husika lakini imekuwa ni mtihani.
Wengine hudai vitu hivyo viliwekwa palipojengwa msikiti wa Maka, Pale ilipo Kabbha, hivyo kufanya iwe ngumu kuchimbua ili kuthibitisha. Na kwa uhakika hata wakichimbua huko watakuta patuuupu.
Wana na binti wa mama afrika, narudia tena na tena maandiko ni mafumbo ya kiimani na si ya wenye kusambaza hizo imani.
Naanza na vinavyoonekana hivyo usishangae nikisema vibao vya pili.
Vibao vya pili ni mikono yako na maandishi yenye kumaanisha ni amri za mungu ni michoro au alama zilizopo katika viganja vyako.
Kila kidole kimoja kina alama Zenye utofauti na kingine na vyote vinakubaliana na alama za kiganja ili kuunda sheria kumi za kimungu ndani yako.
Kamwe alama za mkono wako hazina mahusiano na mtu mwingine, kwa kuwa ni utambulisho wako wa kipekee.
Waangaza nuru wanajua hili ndiyo maana wanakomaa na alama za mikono sababu haziingiliani.
Siri iliyopo katika alama za mikono ndiyo, kiwango cha wewe ni nani, inatakiwa ufanye nini hapa duniani.
Huko ndiko kumebeba siri ya bahati zako za maisha.
Ndiyo maana Kipimo kikubwa cha kujua damu na afya yako hufanyika katika mkono.
Ikiwa na maana ndiko kuna taarifa za mwili wako.
Pia walio na ujuzi wa kudhuru hatima ya mtu hutumia mkono kuchukua taarifa za mtu.
Wenye kujua hili ni ngumu kusalimiana kwa mkono na kila mtu.
Kwa kuwa kila mkono wako una sheria tano( tizama vidole vyako ), Ukiunganisha mkono wa kulia na kushoto unapata sheria kumi. Kwa lugha ya Kimungu ni sheria kumi kwa ajili ya jamii inayokuzunguka.
Kwa lugha harisi zama za Musa zilianza kwa Musa kuwafundisha watu sheria harisi za kimungu.
Sababu watu hao walikuwa hawajui njia harisi za Mungu, sawa na kizazi hiki, wengi wanaabudu na kutenda kwa njia isiyo ya kimungu.
Hizo sheria zimewekwa na Mungu mwenyewe , sawa na kuandikwa ma Mungu mwenyewe, ni kanuni ambazo huwezi kuzibadirisha, ni za lazima, Utake usitake, ni sheria zinazokuhusu wewe mwenyewe.
Ndiyo maana zikaitwa sheria au amri kumi Za Mungu. Kazi yako ni kuzitii au kuziishi.
Ni amri ambazo unaweza kujipangia mwenyewe sababu zinahusu mahusiano yako na watu wengine Kwa upana wa amri kumi zilizoandikwa kwa kila mmoja
Sheria za kwanza ni Sheria au kanuni zilizowekwa tangu unaumbwa/unazaliwa.
Ni sheria au amri zilizowekwa katika dhamiri na dhamira moyoni mwa kila mtu. Hizi ndizo mfano wa kisa cha Musa kuzivunja sheria baada ya kukuta wana wa israel wanaabudu ndama wa shaba.
Na maandiko yanaposema Musa alirudi kwa Mungu na akamuandikia upya ina maana Musa naye aliitikia kanuni na utaratibu wa watu kuabudu walichoabudu hata baada ya kuijua kweli ya sheria za Mungu baada ya kufanya meditation kwa lugha ya kupanda mlimani.
Wanaofanya meditation na kupata uwezo wa kujua kanuni na sheria za Mungu wataungana na mimi kukiri kwamba bado wanajihusisha na mambo ambayo roho wa Mungu kawafunulia kama ni uongo.
Wanabudu vilevile, wanalazimika kuwa na majibu yaleyale kuhusu Mungu.
Hiyo ni sawa na umevunja sheria za Mungu mikononi mwako kwa kuona watu wanaabudu ndama/ visivyo Mungu.vibao hivi vilivyomo ndani ya mioyo ya kila mtu, hutoa kalipio kabla ya kutenda jambo au baada ya kutenda, kwa hali ya kujihukumu mwenyewe kwa dhamira.
Ndiyo maana kabla hujafanya lolote, kuna dhamira mbili zinakinzana, moja inakwambia fanya kwa sababu kuna moja,mbili,tatu.
Lakini dhamira nyingine itakwambia usifanye kwa sababu moja, mbili tatu.
Ikiwa na maana sheria zilizowekwa na Mungu, zinasomwa katika uwanja wa akili yako, kukuacha utii au usitii.
Sheria hizo zimewekwa ndani ya sanduku la agano ambalo ni moyo wako.
Ndiyo maana huwa nasema kila kitu katika maandiko kipo ndani yako na muhisika ni wewe.
Musa ni wewe, sanduku la agano ni wewe, fimbo ya haroni ipo ndani yako pia birika la mana lipo ndani yako.
Mungu ni wewe, kwa kuwa ndiye uliyebeba sheria, utofauti ukiwa wewe si Mungu muumbaji.
Kwa wanaosoma maandiko utaona Maandiko yanakili Musa aliona upande wa pili wa Mungu, lakini hakumuona Mungu.
Ikiwa na maana alijua njia za Mungu lakini si kwamba alikutana na Mungu moja kwa moja.
Sawa na wewe uliye na kawaida ya kumeditate, unajua tu upande fulani kuhusu Mungu lakini si kumaanisha umemuona Mungu.
Tuwe pamoja.
Sisi ni Afrika sisi tu Umoja.