Siyo kirahisi hiiivyo kama unavyosema. Kwanza wale walitoka porini moja kwa moja kwa hivyo mazingira yake halisi (kama vile mahitaji ya chakula na kadhalika) yalikuwa hayaeleweki vizuri na ilibidi wataalamu watumie muda na fedha nyingi kufanya studies tafauti mpaka kupata uelewa wa ecological requirements zao. Kwa hivyo siyo kitu cha kusema tu unawaondoa hapa na kuwaweka pale na mambo yatakuwa sawa.
Pili Wildlife Conservation Society ya USA imetumia fedha nyingi hapo awali katika kufanya hizo studies, pamoja na kupeleka wataalamu Marekani ili kwenda kujifunza mambo mbali mbali kuhusu uhifadhi wa vyura hawa.
Unadhani serikali ya Tz ingeweza kuwapa wataalamu wetu mapesa hayo kwa ajili ya kufanya utafiti wa chura? Hata hizo captive breeding facilities zilizojengwa UDSM na Kihansi ni fedha za World Bank.