Siri ya wafanyabiashara wa Tz wanaofanikiwa ni hii

Siri ya wafanyabiashara wa Tz wanaofanikiwa ni hii

lucky sabasaba

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,656
Reaction score
1,204
Kwa wafanyabiashara wengi wanaosafiri na kuingiza mzigo hapa nchini uwa wana siri moja...USHIRIKIANO..wanaposafiri pamoja wengi ufikia hotel moja na chumba kimoja(sehemu kama Dubai..China..Thailand nk)uwa kuna hotel maalumu kwa wafanyabiashara ambapo chumba kimoja uwa na vitanda kama viwili au vinne kwa ajiri ya ku share..mfano dubai chumba cha bei ya chini ni tsh 150000/kwa usiku mmoja hivyo kama mpo watatu ina maana mtalipa 50,000/ kwa siku nadhani kwenye sehemu ya kulala nimeeleweka.

Kwa upande wa kununua mzigo kila mtu ananunua kivyake lakini kumbuka ushirikiano mzuri uwa kwa wale wanaofanya biz ya aina moja maana wakienda sehemu kununua mzigo mkubwa bei upungua sana wanauziwa bei ya kiwandani..sasa baada ya kununua mzigo inafata issue ya kuutuma kumbuka ukiwa peke yako sana sana utanunua mzigo wa kutosha maboksi sita sasa kwenye meli watapima ukubwa wa mzigo wako(CBM) gharama itakuja $900 lakini kwakuwa mpo watatu mtataka container ili container hulinunui yule anayekutumia mzigo atakupatia na utaliacha bandarini pindi mzigo wako ukifika..

Sasa gharama ya container lenye futi 20 toka dubai mpaka dar ni $2100 sasa kwakuwa mpo watatu itakuwa $700..faida ya kuchukua container ni kwamba gharama ni ndogo..usalama ni mkubwa..utoaji wake bandarini dar ni rahisi maana halichelewi kama mzigo utaoweka kwenye boksi nia ushuru wake utakuw chini..TRA wakitoa gharama ya kodi ya mzigo ktk container kuwa ni milioni 3 maana yake mtachanga na kila mmoja wenu atatoa 1ml..

Vijana wa wahindi na wanaigeria wanaungana na wanafanya hivi..ukishakuwa kwenye kundi ata la vijana watatu mlio serious kufanikiwa ni rahisi ..baada ya mtaji kuwa mkubwa sana kila mmoja atakuwa na uwezo wa kujisimamia kivyake ..ni hesabu ileile aliyofanya mwanamziki beyonce alikuwa kwenye kundi la destiny child alipokomaa na kupata exp akaanzisha biz yake..vilevile michael jackson etc...baada ya mzigo kutoka bandarini kila mtu atachukua mzigo wake na kutafuta soko kivyake..

Ndio maana unaona mfano watu wanaokwenda china kufuata nguo,nguo zao wanazokujakuuza nyingi ufanana maana wanakwenda pamoja na kununua sehemu moja..kiufupi ni kwamba wame share gharama za hotel..gharama za kusafirisha mzigo..gharama za ushuru bandarini..juzi kuna mtu aliandika hapa JF kuwa anaomba advice anataka kwenda china kuleta nguo za biz..ni lazima ujue soko zuri la nguo China lipo wapi..hoteli za kufikia za bei rahisi ni wapi..cargo rahisi ya kutumia mzigo utaonunua nk..lakini si vibaya uungane na wazoefu..vijana muungane mtafanikiwa +971504374387 dubai
 
Kwa wafanyabiashara wengi wanaosafiri na kuingiza mzigo hapa nchini uwa wana siri moja...USHIRIKIANO..wanaposafiri pamoja wengi ufikia hotel moja na chumba kimoja(sehemu kama Dubai..China..Thailand nk)uwa kuna hotel maalumu kwa wafanyabiashara ambapo chumba kimoja uwa na vitanda kama viwili au vinne kwa ajiri ya ku share..mfano dubai chumba cha bei ya chini ni tsh 150000/kwa usiku mmoja hivyo kama mpo watatu ina maana mtalipa 50,000/ kwa siku nadhani kwenye sehemu ya kulala nimeeleweka,kwa upande wa kununua mzigo kila mtu ananunua kivyake lakini

Mkuu kilo saba saba, unataka tuungane kwenye nini?? Biashara gani?? Weka wazi watu waamue kukutafuta!!!
 
Ni ushauri mzuri, labda jinsi ya kupata hao wafanyabiashara ni lazima mtoke wote huku ie utafute watu kabisa kabla ya kwenda ama mnaeza kukutana huko huko na mkafanya hayo uliyosema.
 
Kwa wafanyabiashara wengi wanaosafiri na kuingiza mzigo hapa nchini uwa wana siri moja...USHIRIKIANO..wanaposafiri pamoja wengi ufikia hotel moja na chumba kimoja(sehemu kama Dubai..China..Thailand nk)uwa kuna hotel maalumu kwa wafanyabiashara ambapo chumba kimoja uwa na vitanda kama viwili au vinne kwa ajiri ya ku share..mfano dubai chumba cha bei ya chini ni tsh 150000/kwa usiku mmoja hivyo kama mpo watatu ina

Ahsante!!!
 
Nimejaribu kufuatilia Shauri za huyu mtu zimekaa kifaida zaidi kuliko kihasara!!! Hongera toka kwangu MAHESABU asiyesomeka kwa jicho moja!
 
Huu ni ushauri mzuri sana bwana Lucky.
Ila tatizo letu kubwa baadhi ya sisi Wabongo ni wajuaji sana kupita kiasi. Hii system inaweza kufanya kazi iwapo hao wengine unaotaka kushirikiana nao kuokoa gharama ni watu mnaofahamiana na kuheshimiana tokea nyumbani TZ.
Maana mifano ya ujuaji wetu Wabongo huwa tunakutana nao mara kwa mara katika kusafiri miji tofauti duniani.
 
Nimejaribu kufuatilia Shauri za huyu mtu zimekaa kifaida zaidi kuliko kihasara!!! Hongera toka kwangu MAHESABU asiyesomeka kwa jicho moja!

Ushauri anaotoa mkuu lucky sabasaba ni mzuri lakn its not easy as it seems. Inabdi watu wa namna hyo muwe mnaheshimiana na kuwa karibu sana i.e a close relative/friend or sibling vinginevyo sio rahisi.
 
Hiyo ni kweli lakini ushirikiano ni kwa faida ya wote..wapo wanaofanya hivyo mimi uwa nawaona bila kushirikiana ukisema usimame peke yako ni lazima uwe na mtaji mkubwa hasa kwa biashara ya kusafiri tiketi ya ndege kwenda na kurudi..hoteli..usafirishaji mzigo na ushuru bandarini nk,kwa mtu mmojammoja ni kazi sana...

Vijana wenzetu wa kinaigeria wanafanya hivi sana,hata watanzania wanaosafiri wengi hufanya hivi ktk hili hakuna biashara iliyofichika maana watu wakichangia container kila mtu anajua chake ni kipi..ushuru wa tra ukija mnalipia kwa pamoja baada ya kutoa container bandarini kila mtu anachukua mzigo wake na anapeleka kwenye market yake..mbona mambo yapo wazi sana,wale wafanyabiashara wa magari,nguo,hardware nk uwa wanajuana..kujisimamia mwenyewe kila kitu na ushuru wetu bandarini ulivyo ni kazi kupata faida
 
Hiyo ni kweli lakini ushirikiano ni kwa faida ya wote..wapo wanaofanya hivyo mimi uwa nawaona bila kushirikiana ukisema usimame peke yako ni lazima uwe na mtaji mkubwa hasa kwa biashara ya kusafiri tiketi ya ndege kwenda na kurudi..hoteli..usafirishaji mzigo na ushuru bandarini nk,kwa mtu mmojammoja ni kazi sana...vijana wenzetu wa kinaigeria wanafanya hivi sana,hata watanzania wanaosafiri wengi hufanya hivi ktk hili hakuna biashara iliyofichika maana watu wakichangia container kila mtu anajua chake ni kipi..ushuru wa tra ukija mnalipia kwa pamoja baada ya kutoa container bandarini kila mtu anachukua mzigo wake na anapeleka kwenye market yake..mbona mambo yapo wazi sana,wale wafanyabiashara wa magari,nguo,hardware nk uwa wanajuana..kujisimamia mwenyewe kila kitu na ushuru wetu bandarini ulivyo ni kazi kupata faida

Ahsante sana kwa ushauri wako mkuu endelea kutumwagia ma ujuzi huku JF na kama una connections za dealers tofauti tofauti pia inakua vizuri zaidi ikifika wakat maalum nakucheck for your assistance/guidance. #Barikiwa !!
 
Senior boss hakuna aja ya kwamba lazima mwe na undungu ili uweze fanya huu ushirikiano...mwaka jana nilikutana na mzee mmoja toka TZ alikuwa amefanya manunuzi ya vifaa vya garage pamoja na car washing equipments..kama ujuavyo ni vizito na vikubwa,tatizo lililokuja ilikuwa ni kuvituma cargo wakamwambia $1750 mimi nilimwambia hasitume bali aende sehemu ya kutumia mizigo atafute mtu yoyote anayetaka kutuma mzigo kwenda dar alishtuka kidogo maana alisema hawezikuchangia namtu hasiyemjua, baada ya kumshawishi sana alikubali,akapata vijana wawili,nilimwambia wachange ili wapate container kila mmoja akatoa $700 waliweka vitu vyao na nafasi ikabaki,walipanda ndege tofauti kwenda dar kila mtu akiwa na copy ya BL,bl ni kifupi cha bill of lading ni doc ambayo utampatia agent ili akutolee mzigo pale bandarini..

Hii doc unaweza ku track ata kwenye simu yako kujua meli iliyobeba mzigo wako ipo wapi ata kama meli imetia nanga libya utajua,hii doc itakuonyesha namba ya container lako..jina la meli iliyochukua mzigo wako lini imetoka dubai na lini itafika dar,ni kitu kilichowazi kabisa..baada ya kufika dar walitafutana wakatafuta agent ili awatolee container lao...ushuru wa TRA ulipotoka walichanga na kutoa mzigo wao kila mtu alichukua chake..

Sasa hapo hakuna mazingira ya wizi au kudhurumiana ata kidogo hao watu walikutana siku moja tu..faida ni kwamba utumaji wa container ni cheaper kuliko mojamoja na ata process za bandarini pamoja na tra ni nafuu sana kama una container,yule mzee alinipigia simu kwamba ame save zaidi ya 4.2ml kwa kushirikiana na wale jamaa,kwa wanaofanya biz za kusafiri watanielewa vizuri..hakuna wasiwasi wa kuzungukana maana unajua mzigo wako upo kwenye meli gani..lini umetoka china..upo kwenye container namba gani..lini itafika dar nk..so jaribuni
 
Senior boss hakuna aja ya kwamba lazima mwe na undungu ili uweze fanya huu ushirikiano...mwaka jana nilikutana na mzee mmoja toka TZ alikuwa amefanya manunuzi ya vifaa vya garage pamoja na car washing equipments..kama ujuavyo ni vizito na vikubwa,tatizo lililokuja ilikuwa ni kuvituma cargo wakamwambia $1750 mimi nilimwambia hasitume bali aende sehemu ya kutumia mizigo atafute mtu yoyote anayetaka kutuma mzigo kwenda dar

Wazo lako ni zuri...Swali langu ni kwenye kulipa ushuru TRA. Taratibu zinakuaje ? Wanacharge vp ? Haitaweza tokea katika kulipa ushuru mtu atakua amewalalia wengne dat yeye akalipa kiasi kdgo/kingi kulingana na mzigo wake. Au on this case it happens that kusafirisha na container all in all its very cheap ukilinganisha na means zingine ??
 
Lucky Sabasaba, post zako zinanifungua sana kuelewa mambo ambayo nlikuwa siyaelewi. Kama tungepata watu wengi kama wewe ambao hawana choyo ya maarifa Tanzania yetu ingesonga mbele.

Endelea kutujuza bila choyo na Mungu atakuongeza..
 
Kwa Tanzana tatizo ni Umimi, n si kwene Kuagiza mizigo tu, bali ni kwenye sekta nyingi sana, nakumbuka hata Mkapa akiwa Raisi aliwahi kuliongelea hili swala la Watanznia kila mtu kufaight kivyake, nalionambali sana,

wa kifupi Bila Umoja watanzania hauwezi kushindana na kampuni za Nje kutoka kwenye Mataif kama, China, South Africa, USA,INDIA, UROPA na hata Kenya, Kampuninyingi sana za hizi nchi wana Mitai mikubwa sana na ni ndoto za Mchana kupambana nao kw sababu Watzanai hatuna Competetitive adavantage ya kushindana na haw watu,

Chukulia Mfano wa Maduka ya Shoprite, hawa jama si wakushindana nao kabisa na Vi min supermarket vetu ambayo now day imekuw ni fasheni kila mtu anataka kuwa na chakwake,

Njoo kwenye Mahoteli, Makampuni kama Serena, Sopa na zinginezo ni kamapun kubwa kabia na hakuna Mtanzania hata mmoja anaye weza kushindana kihotel na kampuni kama ya Serenahotel,

Njoo kwenye Ujenzi, hpa ndo balaa, kuna utitili wa kampuni za ukandarasi za kufa mtu, na hakuna hata moja yenye uwezo wa Kushindana na za Wachina au wajerumani kwa sasa kapuni za Ukandarasi za Kibongo imebakia kulalamika tu na kuambulia tenda za Kutengeneza Barabara za Vijijini, Ila hawa jamaa hawatki kabisa kusiki kabisa kitu kuungana,

So Ishu sio Kuchangia kontena tu bali ni katika nyanja nyingi, Bila hivyo tutabakia kuilaumu Serikali tu,

SO DONT COMPETE IF YOU DONT HAVE A COMPETETIVE ADAVATAGE
 
Nimejaribu kufuatilia Shauri za huyu mtu zimekaa kifaida zaidi kuliko kihasara!!! Hongera toka kwangu MAHESABU asiyesomeka kwa jicho moja!

Kihasara Kivipi? Tatizo wabongo tunapend sana kuonenaka yaani mtu asifiwe na Ndugu, jamaa na Marafiki kwamba anaweza agaiza mzigo pekee na hana share na mtu, yaani kwa anzani mtu kuto kuwa na share na mtu ni sifa wakati kwa wenzetu huu ni ujinga
 
Luck Sabasaba uko wapi bro umeadimika kaka Elimu yako hapa jf inakomboa wengi mno kaka usipotee kiivo
 
Back
Top Bottom