Siri yafichuka wachezaji wa Yanga wamemchoka Zahera Mwinyi

Siri yafichuka wachezaji wa Yanga wamemchoka Zahera Mwinyi

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
822
Reaction score
2,095
Wachezaji wa Yanga wamesema waligoma kufanya mazoezi ili kumuonyesha kocha hasira zao baada ya kumtimua Kanavaro.

Wamesema walikuwa na uwezo wa kuvumila matatizo ya klabu ila walichokataa ni Mwinyi kujigeuza Mungu mtu katika klabu hiyo.

Wamemvumilia kuwafanya Kama watoto wa Shule ya msingi na Kama amewakamata mashabiki na viongozi wa klabu hiyo wao hawatakubali kufanywa Kama misukule.

Aidha nyuma ya pazia Kuna tetesi nyuma ya wachezaji Kuna kundi la wanachama wa klabu hiyo wanaojitambua na kutambua thamani ya klabu yao.

Na ndio waliowashawishi wachezaji wagome ili kuhakikisha kocha huyo anaondoka wajenge klabu yao upya.

Wanachama hao wanasema ni bora Yanga ipoteze kila kitu msimu huu ila irudi mikononi mwao na sio kumwachia kila kitu mcongoman huyo.

Wachezaji wametumiwa Kama chambo tu Ila nyuma yao kuna kundi kubwa nyuma yao ambalo linaona klabu yao imeporwa na mkongoman huyo anayeongea Sana na vyombo vya habari.

Aidha wanachama hao wametamka bayana Kama Kuna chochote kocha huyo anaidai klabu akatafute aliyemkopesha amdai ila wao hawatambui deni lolote ambalo aliikopesha klabu.

Hivyo hawako tayari kumlipa chochote kwani hawana mkataba wa kukopeshwa na mwajiriwa wa klabu. Tunachoweza kuzungumzia ni mshahara wake tu. Hayo mengine sisi hayatuhusu.
hajismanara-20190426-0001.jpeg
 
Nasikia na Leo wamegomea mazoezi Zahera anaandaa kikosi B ndo kipo hapa kurasini wanapasha sasa sijui ni mbinu ya kumbomoa azam j3 au kweli kuna mgomo maana kuna kiongozi mmoja kasema yameisha na leo saa 5 wanaanza mazoezi lakini hadi dk hii sijaona mchezaji wa kikosi A
 
Kuna hatari ya lile jengo pale jangwani karibu na lile bwawa kupigwa mnada ili kugharamia deni na mshahara wa papaa "zapesa".
 
Na za chini ya kapeti ni kwamba Zahera ameshasajili wachezaji watano Sasa wachezaji wanashangaa why anasajili wkt hela hamna so km mbwai mbwai..
Naona simba inaendelea kuwahujumu yanga
 
Kama nikweli nawasihi wachezaji wasi mgomee kocha, Yanga ina historia ya kutimua wachezaji mastaa bila kupepesa macho, Mwaka 1976 Mastaa walifukuzwa Yanga, Mwaka 95 walifukuzwa Nyota wote , wakina Godwin aswile, Mohammed husen, Said Mwamba n.kwakaenda Simba. Walikua nyota kwelikweli awa wasasa hawafikii ata nusu ya uwezo wakikosi cha 1995 Lunyamila alikwenda Malindi ya Zanzibar.Wakapabdishwa wakina Maalim Salehe, Silvatus lbrahim, Nonda Shaban , Anur Awadh n.k . Nawaomba wachezaji wasasa wasijaribu kugoma, Yanga wakisha amua jambo huwa hawarudi Nyuma. Watafukuzwa wote na Wataanza mmoja.
 
Nidhamu ya Mpira wachezaji wa Tanzania hawana na ndiyo sababu hawapati mafanikio . Namuunga mkono Zahera 100% anavyosimamia nidhamu. Canavaro sawa ameichezea Yanga kwa mafanikio lakini kwanini Aruhusu wachezaji usiku kutoka kambini kwenye maandalizi ya mechi muhimu bila kumtaarifu Kocha haya mambo ni ya kibongobongo tu nchi nyingine hakuna. Na viongozi wa Yanga wakiingia kwenye mtego waliowekewa wa kumuona zahera ni mbaya na kumfukuza hawatapata Kocha mzuri kama zahera. Zahera ni Kocha msaidizi wa DRC ambayo ni timu kubwa Afrika kwa viwango na historia. Hizi timu zetu za afrika hasa Tanzania zinatakiwa zifundishwe na mwafrika mwenzetu mkali anaevumilia mambo ya ubabaishaji wa kiafrika na mkali wa kuzingatia nidhamu. Wanachama wa Yanga wengine ni Mamluki wa kulinda maslahi yao na ya waliowatuma . Ikiwezekana fukuza wachezaji wote na canavaro wakaunde pan african nyingine. Canavaro alipaswa kuomba msamaha yaishe sio kuleta vurugu
 
Wanafukuzwa na kupewa stahiki zao then wanasajiliwa kwingine... Acha vitisho kwenye maisha ya watu.
 
Uongozi unajifichia kwenye nidhamu. Lipeni hela wachezaji wana familia
Hata mimi nashangaa watu humu wanafikiri soka ni kalata... Unashindwa kulipa mishara tu je utaweza kuvunja mikataba yao eti uwatimue.
Lipeni watu bhana.. Nidhamu wanayo, wanavumilia mengi.
 
Aisee migogoro ndo huwa inanisikitisha Yanga. Zahera kakosea kuwatimua wafanyakazi.
 
Nidhamu ya Mpira wachezaji wa Tanzania hawana na ndiyo sababu hawapati mafanikio . Namuunga mkono Zahera 100% anavyosimamia nidhamu. Canavaro sawa ameichezea Yanga kwa mafanikio lakini kwanini Aruhusu wachezaji usiku kutoka kambini kwenye maandalizi ya mechi muhimu bila kumtaarifu Kocha haya mambo ni ya kibongobongo tu nchi nyingine hakuna. Na viongozi wa Yanga wakiingia kwenye mtego waliowekewa wa kumuona zahera ni mbaya na kumfukuza hawatapata Kocha mzuri kama zahera. Zahera ni Kocha msaidizi wa DRC ambayo ni timu kubwa Afrika kwa viwango na historia. Hizi timu zetu za afrika hasa Tanzania zinatakiwa zifundishwe na mwafrika mwenzetu mkali anaevumilia mambo ya ubabaishaji wa kiafrika na mkali wa kuzingatia nidhamu. Wanachama wa Yanga wengine ni Mamluki wa kulinda maslahi yao na ya waliowatuma . Ikiwezekana fukuza wachezaji wote na canavaro wakaunde pan african nyingine. Canavaro alipaswa kuomba msamaha yaishe sio kuleta vurugu

Ushasikia ni nchi gani kubwa wachezaji wanaishi kambini eti kwa ajili ya maandalizi ya mechi?
 
Back
Top Bottom