Siri za Familia ama Ukoo!

Siri za Familia ama Ukoo!

VUVUZELA

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2010
Posts
3,103
Reaction score
798
Nimekuwa nasikia kila kona watu wakiongelea kichinichini kuhusu siri za familia ama ukoo ambazo huwezi kuzijua hadi ukioa ama ukiolewa huko, ama mtu wa karibu sana akwambie.
Je ni kweli kuwa kila familia ama ukoo una siri zake? Je katika ukoo wenu ama familia yenu kuna siri ambazo wanafamilia tu ndio mnazijua? Je ni zipi?
Shukrani kwenu wote!
 
achilia mbali familia,at individual level hakuna binadamu asiye na siri ambayo ataingia nayo kaburini,au we mtoa mada huna?
 
mleta thread kwenye ukoo wako hakuna siri yoyote? tufungungulie dimba tafadhali
 
Tambua kuwa siri inaanzia katika ngazi ya mtu binafsi, familia, ukoo hadi taifa. Bila siri ngazi zote hizo haziwezi kudumu. Katika famila yetu na ukoo wangu kuna siri nyingi tu, lakini sikwambii kwa kuwa wewe sio mwanafamilia au ukoo wetu.
 
kwa kweli sihitaji hata kuzijua, coz sina kifua cha kuzibeba. Na ziendelee kuwa siri kwa kweli.
 
Don't even dig there. Aisee, ukianza kuchimbua hukawii kuambiwa uliokotwa kwenye machaka ya umang'atini huko na mzee wa ukoo wa kimasai and u landed where u ar. I don't burst my bubble, nakushauri nawe pia,lol!

Ni kweli kabisaaa.....! Siri zipo ila sio kila ukoo/familia wanazo. Vitu vingine ni better left untold maana wanandugu hawachelewi kushikana mashati,bifu la kujiapiza kwenye ukuta..
 
Sisi Ukoo wetu lazima tuoe wake wengi na madada zetu ndoa zao huwa hazidumu - lazima waachike!

kwahiyo nakushauri kwa dhima na taadhima usije kwetu kutafuta wachumba!

Baba_Enock
Nyantakubwa/Ibisabagenyi
Sengerema
 
Kwetu kama kuna siri basi hata mimi siijui
 
Nimekuwa nasikia kila kona watu wakiongelea kichinichini kuhusu siri za familia ama ukoo ambazo huwezi kuzijua hadi ukioa ama ukiolewa huko, ama mtu wa karibu sana akwambie.
Je ni kweli kuwa kila familia ama ukoo una siri zake? Je katika ukoo wenu ama familia yenu kuna siri ambazo wanafamilia tu ndio mnazijua? Je ni zipi?
Shukrani kwenu wote!

sema siri ya kwenu na mimi nitasema ya kwetu.
 
Ha ha ha, koo zenu zina siri hadi nyie hamzijui? So silly
 
kila familia ina mapungufu na madhaifu yao hivyo si kwamba ni siri ila ni mapungufu hivyo hawawezi kujisifu kwa mapungufu kam sehemu ya siri
 
ushasema ni siri, sasa tukizitaja tena hapa siri si itakuwa imefichuka??
 
Mwenzangu hapo wala usiguse manake tukianza kuyasema mambo ya ukoo sidhani kama pata tosha.
 
Nimekuwa nasikia kila kona watu wakiongelea kichinichini kuhusu siri za familia ama ukoo ambazo huwezi kuzijua hadi ukioa ama ukiolewa huko, ama mtu wa karibu sana akwambie.
Je ni kweli kuwa kila familia ama ukoo una siri zake? Je katika ukoo wenu ama familia yenu kuna siri ambazo wanafamilia tu ndio mnazijua? Je ni zipi?
Shukrani kwenu wote!
kwa hiyo wewe unataka tutoe siri zetu sio..!??
 
Ndio maana zamani ndo zilikuwa zinaratibiwa na ukoo ili mtu asije akaoa kutoka ukoo amabao ni wezi,wachawi, wazinzi au hata wenye magonjwa ya kurithi
 
we mwenyewe umesha sema ni siri.Kwahiyo hatuwezi kuziweka hadharani mkuu ila kama wataka zijua lazima ungie kundini kama ulivyo tangulia sema wewe mwenyewe
 
Back
Top Bottom