Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Mnatulaumu bure sisi Makomandoo wa Yanga. Hakukuwa na lojiki yeyote kuwaruhusu Simba waingie uwanjani wakafanye mazoezi gizani. Wao walikuwa hawajatoa taarifa kwa mamlaka ya uwanja ili uwanja uandaliwe na taa ziwashwe, na generator ya dharula iwe tayari ikiwa umeme utakatika. Na wala hawakutupa taarifa sisi wenyeji wao Yanga kwamba wanataka kutumia uwanja muda fulani kwa mazoezi. Unaendaje kumtembelea mwenyeji wako bila taarifa na kumlaumu asipokupokea?
Kanuni zinasema timu ngeni inaweza kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi, lakini kanuni haisemi wataamua muda wowote au kuja bila taarifa. Na kufanya mazoezi kwa timu ngeni sio lazima. Wanaweza wafanye au wasifanye. In fact, Simba walipaswa kutoa taarifa kwetu Yanga kama wenyeji wao ili sisi tutoe taarifa kwa mamlaka ya Uwanja wa Mkapa. Wangetoa taarifa kwa mamlaka ya Uwanja bila kutuambia wenyeji wao bado tungekuwa na haki ya kuwakatalia kuingia uwanjani.
Sasa kwa ajili ya usalama wao tukaona haiwezekani waingie uwanjani, maana wakiumia au kuhujumiwa wangesema ni Makomandoo wa Yanga walituumiza gizani. Hakukuwa hata na wafanyakazi wa Uwanja wa Mkapa walioandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kiko sawa. Sasa sisi tungewaruhusuje katika mazingira hayo na sie ndio wenyeji wao?
Hii Kamati ya Ligi Kuu wanajichekesha tu hawajui wasemalo wala waamualo. Inapaswa kuvunjiliwa mbali kama wanakuwa wazembe kiasi hiki katika maamuzi. Kabla ya kutoa tamko la kuahirisha mechi walipaswa kutoa tamko la kuchunguza jambo hili katika mapana na marefu yake, sio kuwa na kiherehere cha kutoa matamko kabla ya kuwa na facts zote na zikaainishwa na taratibu za ligi.
Halafu mjue sisi Makomandoo wa Yanga hatujasajiriwa na TFF wala Mambo ya Ndani eeh? Yaani tupo lakini hatupo rasmi kwa hiyo huwezi kusema tumekuzuia kutumia uwanja. Hivyo Yanga kama timu haihusiki na sakata hili la Simba kuzuiwa kuingia uwanjani kufanya mazoezi. Msimwambie mtu lakini.