Uchaguzi 2020 Sisi ni mashahidi, tutapiga kura kumchagua tena

Uchaguzi 2020 Sisi ni mashahidi, tutapiga kura kumchagua tena

Joined
Sep 8, 2020
Posts
67
Reaction score
133
SISI NI MASHAHIDI, TUTAPIGA KURA KUMCHAGUA TENA
1.
JPM alipotangaza kufufua shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua Ndege mpya kwa ajili ya usafiri wa anga tulikua hapa #FikraHuru tukicheka kwa dharau. Zikanunuliwa ya kwanza hadi ya nane, usafiri ukaboreka, ATCL ikarudi sasa inapasua anga. Sisi FIKRA HURU ni mashahidi#TutamchaguaTenaJPM!!

2. JPM alipotaganza vita ya kufa na kupona dhidi ya wahalifu wa Amboni Tanga na Kibiti Mkuranga tulikua hapa #TanzaniaNiYetuSote tumejikunyata kwa ukiwa na hofu kuu. Akasema Tanzania inapaswa kutulia mara moja, tutawashughulikia. Kauli ya Amir Jeshi Mkuu ikatoka, ikasikika, utekelezaji ukafuata. Kazi ikafanyika sawasawa, mashaka yakaondoka, maisha yakarudi tena Kibiti na Amboni, nchi ikatulia. Amboni is NIL, Kibiti is NONE. Sisi # TANZANIA NI YETU SOTE ni mashahidi Tutamchagua tena Amiri Jeshi Mkuu!!

3. JPM alipotangaza Serikali kuhamia Dodoma, tulikua hapa #Vijana & Siasa Tanzania tukizozana. Haikuaminika ni kwa namna gani jambo aliloshindwa Baba wa Taifa, akashindwa Mzee Mwinyi, Hayati BWM na Mzee Kikwete lingaliwezekana kwa Chuma JPM. Sisi VIJANA & SIASA TANZANIA ni mashahidi sasa Serikali yote ipo Dodoma, Maendeleo yanachanganya kasi huko. Miundombinu imeboreshwa zaidi, tunayo stendi ya kimataifa, Soko la kimataifa, Uwanja wa Ndege wa kimataifa unakaribia kumalizika na uwanja wa michezo wa Kimataifa uko mbioni kuanza. Ndoto za Baba wa Taifa zimetimizwa na JPM. Bravo Mzee Baba, kwa ushuhuda huu#TutakuchaguaTena!

4. JPM alipotangaza kujenga Bwawa la Umeme la Stiegler's gorge tulikua ni watu wazima wenye meno vinywani hapa#BungeHuru. Hatukuamini, tulisikia kwa masikio na sasa tunashuhudia kwa macho yetu. Baada ya muda mfupi tutakua na umeme mwingi zaidi kwa matumizi yetu na ziada kwa ajili ya kuuza. Hakika sisi BUNGE HURU ni mashahidi,#TutamchaguaTenaJPM!!

5. JPM alipotangaza kujenga reli ya kisasa ya mwendo kasi (SGR) tulikua hapa hapa #Breaking News. Tulibeza na kushadadia kuwa haiwezekani. Sasa tunashuhudia reli hiyooo Makutupora. Muda si mrefu nitaamka asbh nyumbani kwetu Mwanza halafu nitakula lunch nyumbani kwangu Dar. Haya ni maajabu ya CHUMA JPM. Sisi BREAKING NEWS ni shahidi,#Tutapiga kura kumchagua tena JPM!!

6. JPM alipotangaza kujenga barabara za juu Darisalama na njia NANE hadi Pwani tulikua hapa #Siasa za Dar es salaam tukipiga soga na kubeza. Sasa Darisalama watu wanapita HEWANI kama Ndege, njia NANE zinaelekea Mlandizi. Daslamu is SAFE, ni kama ULAYA tu, usiku inawakawaka yote. Sisi Wana-SIASA ZA DAR ES SALAAM ni MASHAHIDI #Tutapiga KURA kuchagua CHUMA CHA PUA JPM!!

7. JPM alipotangaza msimamo wa Serikali juu ya janga la korona tulikua hapa #SIASA, MAISHA NA UCHUMI tukifokeana. Nusu nitoke wazimu kila niliposikia kuwa Nchi haitofungwa, shughuli zitaendelea kwa ajili ya uchumi wa nchi yetu. Nilipinga asubuhi, mchana na jioni. Leo sisi SIASA, MAISHA NA UCHUMI ni mashahidi, kwa msimamo ule madhara ya korona yamepungua ama hayapo kabisa na maisha ya nchi yanaendelea, uchumi wa nchi umeimarika. Kwa ushuhuda huu tutamchagua tena Rais mwenye msimamo na asiyeyumbishwa. #Tutapiga KURA kwa JPM.

8. JPM alipotangaza kujenga daraja la Kigongo Ferry Busisi tulikua hapa #Global Politics Tanzania. Tuliona ni ndoto za alinacha, ni kwa namna gani mambo haya yatawezekana Tanzania, wale wa home sweet home wananielewa vzr. Kigongo na Busisi sio kama Kigamboni na Posta, pana urefu wake. Sasa tunashuhudia ujenzi ukiendelea, miaka mitatu ijayo Wasukuma tutakua tunapita juu ya maji kwa magari, pikipiki, baiskeli na miguu. Na'hene baghosha, Sisi GLOBAL POLITICS TANZANIA ni mashahidi tutakaomchagua tena JPM!!

9. JPM aliposema kuwa atajenga Meli kubwa ziwa Victoria, Nyasa na kukarabati zingine tulikua hapa WhatsApp, Facebook, Twitter na Instagram tukipinga kila kitu. New Victoria sasa inachana mawimbi ziwa victoria huku MV. MBEYA II ikikata sokomoko la ziwa nyasa. Watu wanasafiri kwa raha mustarehe, salama salmini. Ni JPM huyo!
Sisi Wana- Mitandao yote ni mashahidi, tutamchagua tena kiboko ya Maendeleo!!

10. JPM aliposema Tanzania sio shamba la bibi tena tulikua Bungeni na mitaani tukimcheka na kumzodoa kwamba hatoweza kushindana na wazungu. Salamu zake sasa zimefika Ulaya hadi Marekani. Walipofunga safari kuifuata WIN WIN situation tulikuwa hapahapa. Sasa Tanzania inaheshimika Duniani, ni maskini jeuri. JPM ni mtu sana, ametekeleza Ilani ya Uchaguzi hadi ziada.

Amefanya mambo mengi makubwa kwa kipindi kifupi mno. Inahitaji moyo wa kikatiri sana kumnyima KURA mtu mwema huyu, mimi siko tayari kwa dhambi hiyo. Na wewe usiwe tayari kwa dhambi hiyo, sisi ni mashahidi tutakaomchagua tena Oktoba 28.
#MitanoTenaKwaJPM.

MenukaJr.
 
Back
Top Bottom