bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Hakika Yanga wamejipambambanua kama jitu kubwa sana, jitu zito, jitu lililoshindikana chini ya uongozi vijana wahuni wahuni tu kama wanavyowaita wachambuzi wa kibongo na huku uhuni wao ukizid kuwatesa wapinzani wao.
Hata sisi Simba tumeanza kuonja joto ya jua, tumeanza kuonja mishale ya Yanga na inasumu kweli ukiangalia timu yetu ya Simba ni kama imekosa agenda kwa sasa hawana Dira tumebaki kuumia na mafanikio ya Yanga,tumesahau hata kama kuna usajili, tumesahau kwamba timu yetu inahitaji maboresho makubwa na tukikubali kucheza ngoma za Yanga.
Tumekua tunasubiri Yanga wakosee au kugeuza topic kila kinachofanywa na Yanga huku tukisahau nyumba yetu hali tete, tukiendelea na haya sio ajabu yanga ikatawala soka la nchi hii kwa miaka 50 ijayo.
Mwisho wa siku tutaanza kulia ooo Yanga wananunua mechi kumbe wakati wao wanafanya mambo yao sisi tupo tunashangaa kombe lao jipya.
Tubadilike wana Simba.