Sisi Simba tumekubali kucheza ngoma za Yanga

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Hakika Yanga wamejipambambanua kama jitu kubwa sana, jitu zito, jitu lililoshindikana chini ya uongozi vijana wahuni wahuni tu kama wanavyowaita wachambuzi wa kibongo na huku uhuni wao ukizid kuwatesa wapinzani wao.

Hata sisi Simba tumeanza kuonja joto ya jua, tumeanza kuonja mishale ya Yanga na inasumu kweli ukiangalia timu yetu ya Simba ni kama imekosa agenda kwa sasa hawana Dira tumebaki kuumia na mafanikio ya Yanga,tumesahau hata kama kuna usajili, tumesahau kwamba timu yetu inahitaji maboresho makubwa na tukikubali kucheza ngoma za Yanga.

Tumekua tunasubiri Yanga wakosee au kugeuza topic kila kinachofanywa na Yanga huku tukisahau nyumba yetu hali tete, tukiendelea na haya sio ajabu yanga ikatawala soka la nchi hii kwa miaka 50 ijayo.

Mwisho wa siku tutaanza kulia ooo Yanga wananunua mechi kumbe wakati wao wanafanya mambo yao sisi tupo tunashangaa kombe lao jipya.

Tubadilike wana Simba.
 
Siku mkija kushituka tutakua tume waacha mbali nyie si mmekalia umbea na majungu kazi yenu kuiponda Yanga mkisaidiwa na wachambuzi uchwara mfano sasa hivi Kazumari ana waanimsha Mayele ni overrated na dhihaka nyingi, kifupi ni kwamba viongozi wenu wana enjoy sana wanapo waona hamuhoji mambo yenu mpo busy na kiatu mara kuponda kombe la loser mara kesi ya Feisal mkajitia kimbelembele tena Ahmed Ali anatumika kuwapeleka huko ili msahau mambo ya msingi. Hivi kweli afisa habari wa timu kubwa kama Simba anapata wapi nguvu kuongea habari za kiatu ilihari timu ime ambulia patupu?
 
🚮
 
Kuna ulimbukeni tu ndani ya YANGA, promo nyingi ni kujaribu tu kufikia gap lao la SIMBA
 
Kuna ulimbukeni tu ndani ya YANGA, promo nyingi ni kujaribu tu kufikia gap lao la SIMBA
Mkuu Yanga hakuna promo ni action tu, tumefika fainali CAF Shirikisho, jumatatu tunacheza fainali Azam Federation cup, Sisi ni mabingwa NBC premier league msimu wa pili mfululizo.

Nafikiri dish limeyumba kidogo ila si hatari sana maana ni sahihi kwenu kupoteza network coz hamna Cha kujivunia msimu huu labda Saidoo tu mliempa magoli Ili afanane na Mayele Huku mkisahau wa mbili havai moja Mayele ni next level anapiga magoli bongo na Africa nzima!
 
Utopolo ubingwa mumeshachukua na ubwabwa wa ikulu mumekula mbona mnazidi kuweweseka kama hamjiamini vile.
 
Watakuelewa kweli!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…