" SISI sio SISI "

" SISI sio SISI "

Tanki

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
538
Reaction score
246
Leo, nitawasimulia hadithi ambayo hamkuwahi kuhadithia. Kama ilikuwa ni siri basi nimeshindwa kuitunza🙏.

************************************
Kumi na moja jioni majira, ilionekana gari mpya, nyeupe, aina ya Harrier toleo jipya ikikatiza kwenye mitaa ya Tegeta. Baadaye gari ile ikaonekana tena kwenye mitaa ya Mikocheni, tena ni Mikocheni yote, yaani Mikocheni A na B. Haikutosha gari ile ikaendelea kuipasua mitaa hadi ikafika maeneo ya Msasani na Masaki na baadaye ikaonekana kwenye viunga vya ushuani kule panapoitwa Osterbay na mwishowe ikaja kuonekana ikipita kwenye ile barabara ya rami iliyo jirani na Coco beach na kuelekea ueleleo wa kule ilipo hospitali ya Ocean road.
Dereva wa ile gari haikujulikana kwamba alikuwa akitafuta kitu gani hasa, maana alionekana akiiendesha gari ile huku macho yake yakiangalia zaidi kushoto na kulia. Ila, kitu cha kushangaza ni kwamba, gari ile ilienda kusimama katikati ya daraja la Tanzanite, daraja la kisasa lililokatiza baharini.
Magari ya wapitanjia wengine yalionekana tu kulipita gari lile pasipo kujali chochote. Aliyekuwa akiiendesha gari ile alionekana akiwa ameulalia usukani. Hii ikawafanya baadhi ya watu waamini kwamba yule dereva atakuwa amezidiwa na pombe au wengine huiita Masanga au Monde au Maji ya mende.
Basi! muda nao ukazidi kwenda matiti. Yalikuwa yameshapita masaa yenye dakika na sekunde zake kadhaa.Tayari ilikuwa imeshatimia saa tatu na dakika hamsini na tisa na sekunde arobaini na tatu.
Ndipo ikasimama gari aina ya coaster ambayo pale mbele kwenye kioo palikuwapo maandishi mekundu
yaliyosomeka " SISI SIO SISI " arafu kwenye kioo cha nyuma palikuwapo maandishi mengine ambayo hayo yenyewe
yalisomeka " TANZANIGHT F.C "
.Waliokuwa ndani ya gari hiyo walihitaji kufahamu kwanini gari ile ( Harrier) iwe pale muda ule tena ni katikati kabisa ya barabara?. Ndipo wakashuka watu wapatao kumi na saba. Idadi hii ilijumuisha hadi na dereva wao. Watu hao walionekana kuwa ni vijana wenye umri kati ya miaka 19 hadi 28 isipokuwa tu dereva wao ambaye yeye kwa makadirio miaka yake haikuwa chini ya 45 na wote walikuwa maalbino. Basi!, vijana wale na dereva wao wote wakaisogelea ile Harrier, kisha dereva wao akasogea hadi kwenye upande alipo dereva wa ile Harrier kisha akagonga kwa mkono kwenye kioo ili kumshtua, lakini hata hivyo dereva yule wa harrier hakushtuka. Ndipo alipojaribu kuufungua mlango wa gari ile, na uzuri ulifunguka. Akamshika begani na kumtingisha, ila bado tu hakushtuka. Hapo, ikabidi apige simu polisi kutoa taarifa ikiwa ni pamoja na kufuatwa kwa taratibu zote za kiusalama na hatimaye mtu yule akafikishwa hospitalini kwa matibabu.
" Triiii triiii triiii, triiii triiii triiii " .Ni saa sita usiku, simu ya Zamaradi ilikuwa ikiita, hata hivyo haikupokelewa. Alipigiwa mara nne pasipo kupokea. Namba ile ile iliyokuwa ikimpigia Zamaradi ikaenda kuita kwenye simu ya Steve Meng'ere, ambaye wengi humuita Steve Nyerere. Huyu alipigiwa mara saba pasipo kupokea. Hata hivyo mpigaji hakuonyesha kuchoka, alipiga tena namba nyingine. Ilikuwa ni namba ya Joseph Kusaga. Huyu alipigiwa mara sita na yeye pia hakupokea. Aliyekuwa akiwapigia watu hao alikuwa ni Dr.Flavius ambaye namba yake ilikuwa ni +255 676......2317. Kilichofanyika kabla ya kupigiwa watu hao ni
kwamba, wakati akipatiwa huduma mtu yule aliyefikishwa hospitalini pale, Dr.Flavius aliichukua simu ya mtu
yule kisha akaenda kwenye kumbukumbu ya simu alizopiga na kupigiwa. Kwa bahati ni kwamba, simu ile ilionekana kuwa ni mpya kabisa na ilikuwa bado mtu yule hakuwa ameweka Password wala pattern. Hivyo, Dr.Flavius alipoenda kwenye faili la kumbukumbu ya simu alizopiga au kupigiwa, huko ndiko alikobaini kwamba hao watu watatu (Zamaradi, Steve Nyerere na Joseph Kusaga ndio watu ambao mtu yule aliwasiliana nao kwa siku ile kwenye masaa 12 yaliyopita, na ile ndio siku ya kwanza kwa simu ile kuwekwa laini na kwenda hewani. Hata hivyo licha ya kuwa simu ile ilikuwa mpya, ila cha ajabu muda ule ule simu ile
ikazima chaji.Dr.Flavius akiwa ofisini kwake hospitalini pale, mara pasipo hata kubisha hodi wakaingia madaktari wawili,
Dr.Kimei na Dr.Nombo, tena huku wakionyesha kwamba ni watu waliostaajabishwa na kitu. Dr.Flavius ikabidi awaulize kulikoni?, na Dr.Nombo akajibu kwamba......" Tumegundua vitu visivyo vya kawaida kwenye mwili wa huyu mgonjwa mpya. "
Dr.Flavius akashtuka kidogo, kisha akauliza .....
" Ni vitu gani hivyo? "
Dr.Nombo akageuka na kumuangalia usoni Dr.Kimei, kisha akarudisha macho yake kwa Dr Flavius na kusema ........" SISI SIO SISI "

************************************
Swali la kujiuliza! Kwanini KUMI NA SABA???
Na hivi " SISI SIO SISI " ndio nini???
Na ni vitu gani hivyo visivyo vya kawaida walivyovigundua madaktari wale kwenye mwili wa mtu yule???? Na je mtu yule ni nani???? Amekufa au mzima???


Vipi iendelee ?????
 
Back
Top Bottom