Sisi wana yanga tunalaani jambo hili kwa nguvu zetu zote

MUSHEKY

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
2,812
Reaction score
2,760
Awali ya yote niwasalimu nashabiki wenzangu wa kijani na njano

Bila kupoteza muda nichukue fursa hii kwa niaba ya wazee wa jangwani na mashabiki wote watiifu wa wananchi kuulaani uongozi wa juisiemu ukiongozwa na raisi wetu injinia hersi saidi kwa kufanya mambo yanayoigharimu timu pakubwa

Injinia amempa Nandi na Bilnenga zawadi ya milioni tano kwenye harusi yao iliyofanyika Mlimani city usiku wa kuamkia juzi.

Hivi wanayanga wenzangu pesa zote hizo kama zingeongezwa kwenye bajeti ya prisizoni si tungefunga safari tukaenda hata Burundi kuweka kambi kuliko kuwatesa wachezaji wetu na baridi la kule Kimbiji?

Ashakumu si matusi injinia kwa hili umetukwaza kwa kua tunatambua dhahili shahili huyo Nandi na Nenga uliowapa mpunga wote huo hawana mchango wowote kwenye timu yetu ambayo ofisi za makao makuu yake zimeliwa na maji kwa kua zimejengwa kwenye eneo la mabondeni.

Mwisho lakini si kwa umuhimu milioni tano hizi ungeziingiza kwenye bajeti ya machapati pale kambini kwakua imevuja kwamba chakula kikuu cha wakongomani ni machapati na kiuhalisia ndio chakula kikuu cha watu wa Kimbiji tulipoenda kuweka kambi kwa ajili ya prisizoni.

Wasalaam

" Yanga nyuma mwiko mble mwiko"
 
Huu moto wao wa mbele mwiko nyuma mwiko umeniacha hoi kabisa [emoji23][emoji23]
 
Milioni tano hizo labda za maji ya kunywa tu...kumbuka hiyo ninauli ya mtu mmoja kwa ndege kwenda dubai tu...
 
Ukiendekeza hii tabia yako mbovu ya kuhoji matumizi ya hela za watu wasio kuhusu, na pia kufuatilia maisha yao! Basi utaishia mahali pabaya.

Na kama una jinsia ya kiume, jiandae kuvishwa kanga.
 
Ukiendekeza hii tabia yako mbovu ya kuhoji matumizi ya hela za watu wasio kuhusu, na pia kufuatilia maisha yao! Basi utaishia mahali pabaya.

Na kama una jinsia ya kiume, jiandae kuvishwa kanga.
Kumbuka hii ni timu ya wananchi, hapa nahoji uwajibikaji wa kiongozi

Jitahidi kuelewa maandiko utaolewa
 
Kumbuka hii ni timu ya wananchi, hapa nahoji uwajibikaji wa kiongozi

Jitahidi kuelewa maandiko utaolewa
Kwa hiyo ukiwa rais wa Yanga huruhusiwi kuhudhuria harusi na kutoa zawadi! Au alikuambia hiyo hela aliitoa kwenye akaunti ya timu!

Au unataka kutuaminisha huyo Herci Said hana uwezo wa kutoa hiyo hela kutoka mfukoni mwake!

Eti uwajibikaji wa kiongozi!! Huna lolote wewe. Wivu tu ndiyo umekujaa.
 
Hiyo hela ni kwake binafsi sio ya timu, kwaio huwezi kumlaumu kwa kuitumia hivi au vile. Halafu kwani timu haina hela mpaka muanze kutaka viongozi watoe hela zao mifukoni kuchangia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…