Sisi Watanzania ni wapole au waoga?

muokotamatunda

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
1,614
Reaction score
1,202
Ndugu zangu,

Ukiangalia nchi za wenzetu utaona jinsi watu wao ambavyo hawataki masihara. Jambo dogo tu wanaamka na kukomaa vibaya mno, lengo ni kutaka serikali ilifanyie kazi ama laa sauti zao zisikike.

Hapa kwetu Tanzania aisee, watu wamepoa sana, je, ni upole uliopitiliza au uoga? Na madhara ya hii kitu utaona viongozi wanajiibia mali hovyo hovyo.
 
Nchi yetu ya Tanzania ni kisiwa Cha amani Duniani, ndio nchi pekee katika Bara la Afrika inayo heshimika kwa kutunza amani na utulivu.

Ndio nchi pekee barani Afrika Ina utulivu wa uhakika

Ndio nchi pekee barani Afrika inawatu waungwana na wastaarabu, matatizo yetu tunayatatua kwa njia za kistaarabu sio mandamano wala fujo.

Sio uoga Wala ujinga bali uungwana na ustaarabu wetu ndio umetufanya tuendelee kuwa kisiwa Cha amani na utulivu.

Vurugu, fujo na maandamano sio kielelezo Cha werevu bali ni ujuha na ujasiri wa kijinga.
 
Wewe ndio muoga mkubwa...umeacha kufanya juhudi kwa vitendo unakuja kufichama huku halafu unatuuliza sisi khah...

Sisi tumelizika kuibiwa kama unaona roho inakuuma kawashitaki mahakamani,mwoga mkubwa
 
Sisi wazanzibar ni Watu tuliostaarabika sjajua watanzania wote๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 
Ujinga waweza kuwafanya watu kuwa wapole au waoga.
 
Jibu ni moja tu watanzania ni Waoga...
 
Mimi binafsi sio muoga, ila nina roho ya kutokujali. Nilishakaa nikajichunguza, nikatambua kwamba kama nami ningekuwa kwenye mkondo wa asali, ningekuwa mlamba asali mzuri tu. Au laiti kamba yangu ingefanyika kurefushwa, nisingeogopa kula kwa urefu wa kamba yangu. Naomba hiyo kazi tukuachieni waadilifu wa moyo
 
WAOGA....
 
Sisi tumefunzwa uoga ,tokea enzi za mwalimu Nyerere, uoga umeingia kwenye DNA, uoga umekuwa ugonjwa wa kurithi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ