kamwendo
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 900
- 1,923
Wengi wetu tunafahamu madhara ya kiafya ya baadhi ya wadudu kwa binadamu.
Tangu shule tulifundishwa baadhi ya jamii tofauti tofauti za wadudu na madhara yake iwe kiafya na hata kimazingira.
Kwa muda mrefu nimeshindwa kujua huyu mdudu "Sisimizi" ana madhara gani kwetu sisi wanadamu.
Kipindi flani nikiwa shule boarding kuna mwanafunzi mwenzangu alikuwa hata akimuona sisimizi kwa bahati mbaya kwenye glasi ya maji ya kunywa au kwenye sahani ya wali yeye alikuwa hajali anamla pamoja na chakula au pengine anaweza kunywa maji yalio na sisimizi.
Kwa kipindi kile nilistaajabu sana, Nikaona ni kitu cha hatari sana kwa afya yake. Lakini hakuna chochote kibaya kilichomtokea tulisoma vizuri na hatimaye tukamaliza salama.
Jana nimemuona sisimizi kwenye chai ya mgeni wakati nahangaika kumtoa na kijiko na hatimaye nikafikia muafaka nikaimwage ile chai ili nimmiminie nyingine, kwa bahati nzuri yule mgeni aliniona akasema niache tu, Nikaacha ila nikampa kijiko ili ajalibu kumtoa yule sisimizi.
Hakumtoa aliinywa ile chai vile vile huku namuona kwa kumuibia maana alikuwa kwenye maongezi. Nilipanga badae akiondoka nimuulize ila ilishindikana maana kuna sehemu nilikuwa nahitajika so nikamuacha.
Wakuu, naomba kwa yeyote mwenye kufahamu juu ya huyu mdudu sisimizi atuelezee hapa maana kila siku wengi wetu lazima tumuone, Isitoshe nimesikia mengi kuhusu sisimizi kuna wanaosema ni dawa,anaongeza bahati,kuongeza siha njema,kutoa nuksi n.k
Katika yote niliyoyasikia hakuna kinachokubaliana na kichwa changu.
Kwa wenye kujua tafadhali naomba atujuze kwa faida yetu sote.