Sitaamini wanawake tena than my mom

Sitaamini wanawake tena than my mom

DOOKY

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
370
Reaction score
50
N i kisa cha kweli imenitokea leo.

Huyu binti, anasoma hapa katikati ya jiji,
mara kwanza nilikutana naye alikuwa amevaa kimtego, nikaomba namba akasema hana simu.

Hivyo tukawa tunawasiliana na simu ya ndugu yake nyumbani kwao, nikamnunulia simu ya ukweli ili tuwe hewani.

baada ya muda akanipiga mzinga kwa Pasaka nikampa, tukaonana, nikamtokea akakubali ombi langu.\

Kisa chenyewe

Baada ya kuona, ninaweza kumsaidia mambo madogo madogo, akawa ananipiga mizinga ya hapa na pale nikadhani ya kawaida. binti kila tumepanga kuonana anasema hana muda anaumwa.

Siku kadhaa rafiki yake akasema huyo demu ameibiwa simu hivyo anaogopa kuniambia, nimpe pesa yeye akamkabidhi ili akanunue simu.

Leo akasema hayuko chuo yuko nyumbani kwao ana birthday yake nikasema poa tumeet kwao akadai nisienda coz hakuna sherehe yoyote zaidi ya keki, hibyo anaomba pesa ya keki, sikukubali kama nitatuma....

tukawa tunachat na kusema hayuko chuo hivyo nimtumie pesa ya keki, mara ikaingia sms ikisema "niko chuo" (simu ya rafiri yake wa chuo anatumia yeye alishaibiwa niliyomnunuliwa kwa madai yake).

Mchana wakati natoka kwenye kikao nipo na gari nikamuona amesimama akitokea chuo, anasubiri gari yangu ipite ili avuke.... nikampigia simu nikamwambia uko wapi ili kuhakikisha kama yuko homu bado.

Akajibu niko nyumbani, siko chuo..... nikamwambia mbona nakuona unasubiri gari uvuke barabara.... simu ya rafiki yake ikakatwa... nikamtext ni shetani mkubwa ambaye sijawahi kumuona maishani. Akajibu Nikome kumwita shetani mimi na familia yangu ndiyo shetani.........


stori ndefu lakini hapo nimefupisha....nimefuta namba yake, na kuanza kumsahau kidogo ingawa mood ya kufanyakazi haipo kabisa leo.....


Sitaamini wasichana tena...... Nawasilisha
 
ID ya DOOKI inawakilisha Mwanamke. au ulitaka akusage, au ulitaka umsage yeye?

Mods!
Pelekeni hii habari MMU inatuchefua hapa
 
Mmoja akikutenda, usiichukie Dunia Nzima..

Anyway in life expect the unexpected, na ukitenda wema usitegemee kutendewa wema.., ila kutokutendewa wema kusikufanye uache kutenda wema.

Binadamu we are weak am sure hata wewe mwenyewe kuna mambo huwezi kujiamini 100% (temptations n.k.) hivyo basi hata kwa mwenza wako ni vile vile, na mara nyingi tukikosewa kama action yetu huwa inakuwa ya kuja juu defense ya aliyekosa inaweza pia ikaja juu

(ulimita shetani akakasirika na yeye akajibu kwamba wewe ndio shetani, am sure hakumaanisha kwamba wewe ni shetani)
 
pole jamani
mzinga wa keki tyu ndo umwite mtu shetani?
keki sh ngapi bwanaaa... BY THE WAY
kwa nini wanaume wengi wakimuomba binti no ya simu akisema hana simu mnapenda kutoa hela ya kwenda kununulia simu?
kwani mwasiliano lazima yawe ya simu?
wengi walishakula sana izio hela zenu
sio huyo tu
taratibu jameni
 
Si binti ni wa katikati ya jiji? ulitegemea nini.
 
Ulikutana naye tu njiani ukaanza mawasiliano naye. Ulijua dadako huyo? Ndiyo huwa tunajikuta tunaoa majini hivi hivi.
 
Pole sana,
Kwa namna ulivomuingia huyo mdada naye kakupokea kwa style hiyo hiyo,

Jaribu kumjua mtu kwanza na kupata uhakika wa kuwa nae,bila kujionesha km unazo na ni mtoaji ndio uanze kumwaga mihuduna!
 
hapo ndipo wanaume wanapokosea....
Jinsi unavyomtokea msichana ndivyo utakavyopokelewa.........
Na aina ya wasichana pia muiangalie, si kila msichana anaweza kuwa mke/mpenzi na si kila mwanaume anafaa kuwa mume /mpz.

Nakumbusha jinsi utakavyomtokea mwanamke ndivyo utakavyotreat-iwa, ukijifanya unazo atazitumia kweli
 
You were getting played like a dummy and you couldn't tell? Double SMH
 
Mapenzi ni bahati nasibu, endelea tu kujaribu usikate tamaa. Pole sana.
 
hapo ndipo wanaume wanapokosea....
Jinsi unavyomtokea msichana ndivyo utakavyopokelewa.........
Na aina ya wasichana pia muiangalie, si kila msichana anaweza kuwa mke/mpenzi na si kila mwanaume anafaa kuwa mume /mpz.

Nakumbusha jinsi utakavyomtokea mwanamke ndivyo utakavyotreat-iwa, ukijifanya unazo atazitumia kweli

vikionesha ubahili tangu awali tunawaperceive hawajali. Vinjemba vya watu sijui viwe vinajilipua vipi.
 
Pole sikupi kwa sababu hujasema ulimpenda kwa ajili ya kumuoa au ulikuwa unafanya naye umalaya tu. Mshahara wa dhambi ndivyo unavyokua na mwisho ni mauti kama atakuwa amekuambukisha ukimwi. Tenda kama Mungu anavyotaka, amekuumba kwa mfano wake na kukupa akili na utajiri ulionao, maana kwa ulivyojieleza mizinga uliyopigwa na usafiri unao inaonyesha jinsi Mungu anavyokupenda kwa kukupa vijisenti sasa wewe badala ya kuwasaidia wenye shida unazitoa kufanyia umalaya. Muogope Mungu.
 
Huyu bado yai, hata hajaatamiwa.

Mtu una gari? Kwa maisha ya kitanzania ili umiliki gari lazima unafanya kazi/

Sasa hadi umeanza kazi ulikuwa hujawahi kuhonga?

Maajabu.

Ur still young with wanawake ww....
 
Pole ndugu,inamaana huwajui wasichana wa vyuo kaka. Mm vilaki laki vyangu vinaniuma sn aise...ndo niliwajua vzr sasa, naiman nawe umeshawafahamu uzuri hvyoo...
 
kinachokuuma nshajuwa ni kwamba bado ulikuwa hujamla mzigo so unawaza pesa zako,najuwa inaumaga kimoyomoyo,,,,ila nawe ulichemsha approach,ntaku pm nikupe maujanja
 
Back
Top Bottom