Pretty
JF-Expert Member
- Mar 19, 2009
- 2,577
- 565
Na Bahati Mwiko, Bariadi
28 October 2009
MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge amesema hakuna mtu anayemsaka kwa ufisadi na kama yuko amfuate Bariadi amkamate.
Vile vile Bw. Chenge amewataka wapiga kura wake kuwapuuza wanasiasa aliosema wanaeneza uvumi huo kwa madai kuwa ni wanasiasa uchwara, waliofilisika kisiasa.
Mbunge huyo aliyelazimika kujiuzulu uwaziri wa Miundombinu Aprili 20, mwaka huu baada ya akaunti yake ya nje kwenye Kisiwa cha Jessey kubainika ina zaidi ya sh. bilioni moja zinazodaiwa kupatikana kwa rushwa ya rada, alisema kuwa yeye ni safi na pia mbunge wa vitendo.
"Ndugu zangu nataka niwaambie kitu kimoja, wapo wanasiasa uchwara hasa hawa wa chama cha (UDP) wenye chama cha ukoo, wanasema eti mie siwezi kuja kwenye jimbo langu. Ni waongo mimi sitafutwi, msiwasikilize wana nia ya kuwalaghai muwape kura, kama natafutwa wakawambie niko Bariadi waje wanikamate," alisema Chenge.
Bw. Chenge aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Bariadi alipokuwa akihitimisha kampeni za wagombea wa uongozi katika Uchaguzi wa Serikari za Mitaa uliofanyika Jumapili iliyopita.
Aliwalaumu Mwenyekiti wa UDP, Bw. John Cheyo na mdogo wake, Bw. Isack Cheyo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 2005 kabla ya kiti hicho kuchukuliwa Bw. Chenge, kuwa wanaeneza maneno ya uongo kwamba yeye (Bw. Chenge) hawezi kufika jimboni hilo kwa sababu anatafutwa na makachero wa Uingereza.
Bw. Chenge anachunguzwa na Taasisi ya kuchunguza Rushwa ya Uingereza (SFO) kama alihusika na rushwa ya rada iliyoligharimu taifa zaidi ya sh bilioni 40. kutoka kwa Kampuni ya kuuza zana za kijeshi (BAE Systems) ya Uingereza.
Chanzo gazeti la majira.
Sio mpenzi wa siasa, lakini baada ya kuona hii habari imenitouch kwa kweli. Hivyo nimependa kushare nanyi watu wa jukwaa hili.