Does it make any sense kununua dawati?
Kwangu mimi gharama ya elimu ni kubwa kuliko dawati. Kama mwanafunzi hapati dawati, hiyo elimu anaweza kuipata? Sio ajabu majibu yakawa mepesi tu kuwa matokeo mabaya ya kidato cha nne na huko tuendako cha sita siyo sababu ya shule za voda faster kama alivyosema waziri.
Hebu Tanzania tuwe na vipaombele vitatuwezesha kusonga mbele kwa kasi ya ajabu tofauti na hii itizamo ya kisiasa zaidi.
Mfano: 1. Sikuridhika na stimulas package- Ile hela (zaidi ya Trilioni) italiwa na wachache, ingeweza kuondoa tatizo hili
2. Mabilioni ya JK yangeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo hili, kuliko kwenda kuwekeza sehemu ambazo hazina maandalizi kwa sababu za kisiasai zaidi. Elimu ndio itakayomkomboa Mtanzania na sio kumnunulia Tshirt na Kofia zenye picha nzuri za wagombea walionenepeana kwa rushwa!